Kafulila: Rais Magufuli amesahau uchumi wa mnyonge

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
SOMA UCHAMBUZI WA KAFULILA KUHUSU UCHUMI MADA MOTO C.TEN JANA.IJUMAA 06,JAN,2017

Nikweli Serikali imejisifu kwa ukuaji wa uchumi wa asilimia7% , na nikweli kiasi hicho ni miongoni mwa rekodi ya juu ya ukuaji Afrika na dunia kwa ujumla kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kimataifa.

Hata hivyo ifahamike kwamba rekodi hii imekuwepo na imendelea kuwepo tangu awamu ya Mkapa. kwani hotuba ya mwisho ya Awamu ya tatu, Bajeti ya 2005/06,ukuaji wa uchumi ulikuwa asilimia 6.9%. na imendelea kuwa hivyo miaka yote kwamba uchumi wetu unakua kwa asilimia 6%-7%.

Tatizo kubwa la ukuaji huu umeshindwa kupunguza idadi ya maskini.kwani maskani wanaongezeka kila mwaka.ndio sababu wasiojua nadharia za uchumi wanakataa kuamini kuwa uchumi unakua.

Ukuaji wa uchumi sio lazma upunguze umaskini. inategemea sana usimamizi wa uchumi huo.Kwenye uchumi kuna dhana mbili, UKUAJI WA UCHUMI na MAENDELEO YA UCHUMI. ukuaji wa Uchumi unapimwa kwa vigezo vya ongezeko la uzalishaji ndani ya mwaka katika nchi husika, bila kujali uzalishaji huo unahusisha watu wangapi, bila kujali ni wenyeji kiasi gani wanahusika.unapimwa kwa vigezo kama Kiasi cha uwekezaji, Mfumko wa bei, Mauzo nje, Manunuzi nje, Kiasi cha akiba(saving), Matumizi ya serikali, nk.

Maendeleo ya Uchumi yanapima ubora wa maisha ya watu. vigezo vyake ni kiasi gani mazingira ya uchumi yameboresha maisha ya watu, kama afya, elimu, maji, umeme, uwezo wa kumudu mahitaji, nk

Mkapa alikabidhiwa nchi ikiwa na mazingira magumu sana ya kiuchumi, lakini aliacha misingi imara ya kiuchumi. Kwa mfano riba za bank ilikuwa alikuta zaidi ya 26% ameacha 14%,Akiba ya fedha za kigeni alikuta ya miezi miwili, akacha ya miezi7, JK akabakiza ya miezi4 na itaendelea kuwa ya miezi4 kwa hali ilivyo,alikabidhiwa nchi haikopesheki akaacha deni la 10trilion,

JK ameacha zaidi trilion 40 na linazidi kupaa, changamoto pekee ambayo awamu ya nne ilipaswa kushughulika nayo ilikuwa kufanya ukuaji wa uchumi na misingi yake aloacha Mkapa itafsiri maendeleo ya uchumi kwa maana ya kuboresha maisha ya watu.

Awamu ya nne ilishindwa jukumu hilo kwa kiasi kikubwa na awamu ya tano haioneshi mwelekeo wa kupunguza maskini kwa kiasi kikubwa.

Sababu ya uchumi kukua bila kupunguza maskini ni pamoja na sekta zinazokua kiuchumi kubeba watu wachache au kuwa na athari ndogo kwa watu wengi.sekta ambazo ukuaji wake upo juu kwa miaka mingi ni Utalii, Madini, Mawasiliano, huduma za fedha, nk . ambazo kwa hakika zinabeba watu wachache.

Cha kufanya bado ni kuhakikisha kilimo katika dhana pana kinainuka, tangu miaka ya 2000s, Tafiti zilifanywa na Taasisi ya REPOA na kuonesha kwamba kilimo kikikuzwa japo kwa asilimia nane kwa miaka3 mfululizo kinaweza kupunguza idadi ya maskini kwa asilimia50%

Ni bahati mbaya kwamba kwa miaka yote kilimo hakizidi ukuaji ni asilimia3 ikianda sana 4% kwa zaidi ya miaka 20.na mbaya zaidi haionekani kama awamu hii inamsukumo katika eneo hilo.

Tafiti za REPOA zimeonesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya mbolea na tija katika kilimo. Kwa mfano kijijini eka ya mahindi iliyolimwa bila mbolea wanavuna kati ya gunia 3 mpaka5. Wakati eka iliyolimwa kwa mbolea mavuno ni gunia 20 mpaka30.hivyo mbolea inaongeza kwa kiasi kikubwa tija ya kilimo

Nasema awamu hii inaelekea haina mpango na wakulima kwasababu miaka yote tangu mfumo wa kutoa ruzuku kwenye mbolea, tija iliongezeka ingawa mbolea ilikuwa kiduchu.

Ripoti ya Poverty&Human Development ya 2014, inaonesha umuhimu wa sekta ya kilimo na hasa matumizi ya mbolea na kutoa mifano ambayo ni aibu kwetu.kwamba kwa wastani Mkulima China inatumia zaidi ya 260kg za mbolea kwa eka1, Tanzania tunatumia wastani wa 9kg kwa eka1. Inawezekana tukawa na hoja kwamba China ni taifa kubwa kiuchumi, lakn ripoti hiyo inaonesha hata Malawi, nchi dhaifu kiuchumi, wastani mkulima anatumia 29kg za mbolea kwa eka1.

Sasa tujiulize, kama huo wastani wa 9kg kwa eka ni wakati ruzuku ya mbolea ilitengwa walau. je sasa? maana mwaka 2015/16 , ruzuku ya mbolea ilikuwa 78bn, wakati mwaka huu 2016/17 ruzuku ya mbolea imeshuka mpaka 10bn.

Nivema Mhe Rais akatazama upya eneo hili. kiasi hiki cha ruzuku ya mbolea hakifanani na serikali ya wanyonge. repoti ya USAID, 2014, inaonesha watanzania walio kwenye kilimo ni asilimia70% na kati yao asilimia75% ni akina mama.

Nikweli nikiwa bungeni tulisema sana kuhusu aibu ya Taifa kukosa ndege, binafsi nakubaliana na uamuzi wa serikali kununua ndege. lakini sikubaliani na uamuzi wa serikali kutekeleza mpango mkubwa wa kuwa na shirika kubwa la ndege sasa. Lazma watanzania wajue kuwa biashara ya ndege ni ngumu mno duniani.

Na nchi nyingi hapa Afrika zinaendesha biashara hii kwa hasara ikiwemo Afrika ya kusini, Rwanda yenyewe pamoja na kununua Airbus juzi, lakn wanakiri kuendelea kutengeneza hasara isipokuwa wana malengo ya muda mrefu, Kenya Shirika lao hoi kwa madeni, Walau shirika la ndege Ethiopia wana nafuu, Biashara ya ndege duniani kwasasa imezidi kuwa ngumu, tunaona fahari ya Emmirates,

Lakini nchi hizi za falme ya kiarabu zimeamua ku pump mabilioni ya kutosha kwenye ndege kuwa wababe wa dunia kwenye usafiri huo kama mbadala wa mafuta ambayo wanajua yatakwisha au bei itakwisha sana kadiri ya muda.Ndio mana unaona wana ubavu wa kutikisa mashirika kongwe ya Ulaya kama KLM au British Air,

Hivyo hili la ndoto ya shirika kubwa la ndege maana yake tuwe tayari ku pump mabilioni ya kutosha kwa hasara ya miaka kadhaa . binafsi nakubaliana na ule msemo wa kupanga ni kuchagua. Je tunadhani hii inapaswa kuwa kipaumbele kiasi hicho? Nikweli ndio njia rahisi ya kuinua umaskini wa wanyonge? nadhani sio!

Uamuzi wa kutopandisha bei ya umeme kweli ni tija kwa wananchi na wenye viwanda, lakini naomba ieleweke tu kwamba Tanzania ndio nchi yenye bei ya chini ya umeme kuliko Rwanda, Kenya na Uganda. na ieleweke pia kwamba tatizo la viwanda Tanzania sio bei ya umeme bali umeme wa uhakika.

Sio affordability, but reliability. Pamoja na umeme wetu kuwa bei chini kiliko washindani wetu lakn kwasababu sio wa uhakika ni tatizo kwa viwanda kuliko hata nchi ambazo bei ipo zaidi yetu.

Pia ifahamike kwamba serikali inatumia fedha nyingi sana ya hazina ambayo ni kodi yetu kuliendesha shirika hili. zaidi ya bilioni 400 kila mwaka ni ruzuku inakwenda TANESCO. Hivyo tujue kwamba hata uamuzi wa juzi kuzuia bei kupanda, haina maana hauna madhara kwa wananchi kwani wanazuia bei kupanda na watapunguza bajeti ya elimu au dawa au kilimo au maji huko hazina ili kuibeba Tanesco.

Kwa hiyo ni sawa na kusema tumekubaliana gharama za umeme tubebe wote wenye umeme na wasio na umeme badala ya kuachiwa mwenye umeme peke yake. ndio ruzuku za zaidi ya 400bn huku mbolea kwa wakulima inaenda 10bn..afu tunasisitiza kuinua wanyonge

Mhe Rais amefanikiwa kuutikisa mfumo kwa kuutisha, anatisha, mfumo ambao kwa miaka yote ulikuwa very rigid. hilo nampongeza. ushauri wangu ni aende mbele sasa kutengeneza Katiba itakayotengeneza mfumo unaotisha dhidi ya ufisadi na uzembe.

Kama nchi tunahitaji mfumo unaotisha zaidi kuliko mtu anaetisha kwasababu mfumo upo leo na kesho lakini mtu yupo leo kesho hayupo. kama alikuja Nyerere akaondoka, Mwinyi, Mkapa na JK, wote wameondoka kama yeye atakavyondoka, lakin mfumo hata akiondoka atauacha.

Atekeleze agenda ya Katiba Mpya kutengeneza mfumo madhubuti na sheria, kwa mfano saivi ilipaswa apeleke mabadiliko ya sheria ya utumishi wa umma ili mengi anayoyafanya kwenye utumishi yawe kwa mujibu wa sheria, asipofanya anaweza kuingiza hasara kwani watumishi wengi watakwenda Mahakamani na kushinda kesi na kulipwa mabilioni.

Mambo mawili niliyasema sana nikiwa bungeni. mpaka mkutano wa bajeti wa mwisho June7,2015 nilisisitiza ilikuwa ni suala la kampuni za simu na migodi kuorodhesshwa kwenye soko la mitaji.Napongeza uamuzi wa serikali sasa kwamba kampuni za simu zimelazimishwa kuorodhesha hisa zoa kwenye soko la mitaji la Dar es saalam(DSE).

Kwa Kampuni za simu kuorodhesha hisa zao ni fursa kwa umma kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hizi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. lakini zaidi ni inatoa fursa kwa hesabu za kampuni hizi kufanyiwa uchunguzi na uchambuzi wa kutosha(sereous scruitiny).

Na hivyo kupunguza uwezekano wa kampuni hizi kuficha usahihi wa mapato na matumizi yao, kwani kampuni nyingi duniani zina tabia za kukuza gharama za uzalishaji na kupunguza mapato yake kwenye vitabu ili zionekane zinapata faida kiduchu ili kupunguza kodi ya faida.

Jambo la ziada kwa kampuni hizj za simu ni TCRA ihakikishe inanunua mtambo kurekodi matumizi ya simu ya simu zote ili serikali iwe na hakika zaidi ya mapato ya kampuni hizi. tangu mwaka 2007, sijawa Mbunge hoja hii imezungumzwa bungeni, lakn serikali ilikuwa na uzito saana.

Kitu pekee ambacho TCRA walifanya ni kununua mtambo wa kurekodi simu za nje tu. ambayo ni asilimia ndogo sana ya matumizi. Hii ni tatizo kubwa ambalo nadhani linahitaji msukumo wa Rais kwasababu watu wake wanavuta miguu kutekeleza kwa karibu miaka kumi sasa

Ni kweli hali ya mzunguko wa fedha kwenye uchumi ni mdogo sana. Nikweli kiasi fulani inatokana na serikali kuziba mianya ya dili. lakn tuseme kweli kwamba sio msingi wa ukubwa wa tatizo. kuna sababu nyingi, ikiwemo stracture ya deni letu na ulazma wa kulipa deni hilo. deni letu ni uwiano wa 80:20.

Kwamba asilimia 80% ni la nje. na limeiva kwa kasi. kiasi kwamba kila mwezi serikali inalazimika kulipa wastani wa 700bn. wastani makusanyo ya ndani ni 1100bn. lakini pia kwa kipindi cha mwaka mmoja huu serikali imekopa sana ndani kiasi cha kuvunja rekodi ya miaka yote. serikali imekopa karibu trilion2. kuanzia Novemba2015 mpaka Disemba 2016.

Miaka ya nyuma mikopo wa ndani kwa mwaka haikuwa inazidi 1trilion.na inakopa zaidi ndani kwasababu imekwama mikopo ya Ulaya. ndio mana umemsikia Waziri wa Fedha juzi akikiri kukosa mikopo nafuu na misaada toka Ulaya na kwamba wameamua kujielekeza nchi za Japan, China, Korea ya kusini, India,nk.

Sababu kubwa ya kukwama mikopo nafuu na misaada ni masharti ya siku zote kuwa Ulaya wanataka kuona demokrasia na utawala bora. ndio maana unamsikia waziri anasema mikopo mikwama kwasababu riba za ulaya zimepanda toka 6% mpaka 9% bila kusema huko upande wa pili riba ni kiasi gani?. tumevuruga uchaguzi zanzibar, sheria mbovu ya mitandao, vyama vya upinzani kuminywa na bunge gizani ndio siri ya ushirika wetu na ulaya kuchechemea.

Hali ni mbaya. tunajua sehemu kubwa ya miradi ya maendeleo inategemea misaada na mikopo nafuu toka nje. Baada ya kabanwa misaada na mikopo nafuu toka nje sasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka mzima ni chini ya 30% ya makisio ya bajeti. Hii ni kwa mujibu wa Monthly Economic Review Reports zinazotolewa na BOT kila mwezi. Makusanyo yetu ya mwezi yanaishia kulipa deni na mishahara tu

Kama tunalipa 700bn, na mishahara 560bn, wakati makusanyo ni wastani ni 1100bn, unategemea nini? ndio maana kwa mujibu wa repots hizo MER za BOT, inaonekana deni la ndani wakati awamu ya kwanza inamaliza muda wake ilikuwa 1.7trilion, na kwa miaka10 ya JK deni la ndani likafikia 7.5trilion na mwaka mmoja huu deni la ndani limefikia 10trilion kwa maana ya nyongeza ya zaidi ya 2trilion

Kasi zaidi ya serikali kukopa ndani inapunguza kiasi cha pesa kwenye mzunguko. lakini kwakuwa haina namna inabidi iwe hivyo, na hii inachochea kuzidi kushuka kwa shughuli za biashara(austerity economy).

Binafsi naamini Rais ana dhamira lakin inakosekana focus , hajawa strategic kufikia lengo lake analojipambanua kama Rais wa wanyonge. asipoangalia miaka 5 itamalizika bila kupunguza makali ya maisha na kubaki na orodha ya waliotumbuliwa. Huyo mvuvi ameuliza kwanini uvuvi baharini bado haupewi msukumo. Ndio msingi wa hoja yangu awali kwamba sekta ya kilimo katika dhana pana ambayo ni mazao, ufugaji na uvuvi, haijawa na msukumo

Tazama Nambia ukanda wa bahari kwajili ya uvuvi kwao una urefu wa 1500km na sisi 1400km, ni karibu sawa, lakn Namibia ndio wanaongoza kwa kuuza nje samaki ukanda wa kusini mwa afrika, na kwao baada ya madini,uvuvi ndio sekta ya pili ktk uchumi wao. Tunahitaji sera ya viwanda iwe ktk viwanda vya processing na mafacturing ya mali ghafi za kilimo. hivi ndio viwanda vinavyoajiri watu wengi dunian
 
tatizo la tanzania sio kilimo pekee watu wanalima lakini mazao yao hayawalipi , kwa kuwa hakuna sehem ya uhakika wa kuyapeleka mazao yao , tukishaakuwa na viwanda japo vichache vya kuwachakata mzai yetu kila mtu atavutiwa na kilimo
 
hela ya rambirambi tu anaiba na kudhulumu hivyo viwanda vitatoka wapi?
 
Nilicho jifunza.
1. Rais Mkapa alikuwa ni rais bora kabisa kwa masuala ya ku manage uchumi.

2. Rais Kikwete alishindwa ku manage vitu kama madeni ya nje, ufisadi na akiba ya taifa lakini mwana nchi wa chini bado uchumi ulimgusa, na pia pesa nyingi zilielekea kwenye miradi, bado kikwete ndio rais pekee aliye ongeza kwa kuzalisha ajira, kukiza sekta binafsi na kubuni projects mpya kubwa za nchi hii.

3.Rais Magufuli ameshindwa kufanya chochote yupo yupo tuu. Wakati ana sema ameziba mianya ya ufisadi, matumizi ya serikali yanaongezeka, serikali inakosa mikopo na pia uchumi wa mwananchi wa kawaida una hali mbaya, serikali imebaki tu kiendeleza miradi alo acha kikwete na haiwezi kubuni jipya kwa sasa huki ikishindwa pia kutoa ajira.

*kama asipo badilisha utaratibu wa sasa ki uchumi, Rais Magufuli atamaliza miaka 5 huku akiendelea kutumbua bila kuwa na jipya lolote. Na atakuwa the worst president kat ya awamu zote tano
 
JPM taasisi zake zingekuwa huru, for sure NBS ingekuwa ishatoa takwimu za ukuaji wa 4% kwa sasa. Lakini kwa kuwa wanaogopa kutumbuliwa ukitoa takwimu za namna hiyo, awamu hii itarekodi hadi ukuaji wa 15%. Duniani kote, takwimu zimeendelea kuwa manipulated kwa interests za wanasiasa.
 
ili nchi yetu isonge idadi ya wakulima lazima ipungue tuwe na wakulima wachache waliowezeshwa ,hakuna nchi duniani imeendelea ambayo 80 percnt ya watu wake ni wakulima
 
Kuna umuhimu kwa Rais Magufuli kuwarudisha Wizara ya fedha, waliokuwa wachumi wa serikali ya tatu haswa aliyekuwa Katibu mkuu Mr Mgonja ambaye alifanya kazi nzuri sana kukuza uchumi wa serikali ya awamu hiyo.
Mheshimiwa Rais Magufuli huyu ndugu Mgonja anafaa sana kuwa Waziri wafedha. Umefanya kazi nzuri sana katika muda wa utawala wako ila hili suala la uchumi ndio itakukwamisha.
 
Mgonja again. Tafadhali ndugu. Hawa walikuwa wapiga dili maarufu, Kikwete pamoja na huruma zake aliamua kushughulika nao. Hata kama mtu alipona kwenye lile sakata lao, ukweli Upo wazi walitukomesha. Labda Mgonja mwingine.
 
SOMA UCHAMBUZI WA KAFULILA KUHUSU UCHUMI MADA MOTO C.TEN JANA.IJUMAA 06,JAN,2017

Nikweli Serikali imejisifu kwa ukuaji wa uchumi wa asilimia7% , na nikweli kiasi hicho ni miongoni mwa rekodi ya juu ya ukuaji Afrika na dunia kwa ujumla kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kimataifa.

Hata hivyo ifahamike kwamba rekodi hii imekuwepo na imendelea kuwepo tangu awamu ya Mkapa. kwani hotuba ya mwisho ya Awamu ya tatu, Bajeti ya 2005/06,ukuaji wa uchumi ulikuwa asilimia 6.9%. na imendelea kuwa hivyo miaka yote kwamba uchumi wetu unakua kwa asilimia 6%-7%.

Tatizo kubwa la ukuaji huu umeshindwa kupunguza idadi ya maskini.kwani maskani wanaongezeka kila mwaka.ndio sababu wasiojua nadharia za uchumi wanakataa kuamini kuwa uchumi unakua.

Ukuaji wa uchumi sio lazma upunguze umaskini. inategemea sana usimamizi wa uchumi huo.Kwenye uchumi kuna dhana mbili, UKUAJI WA UCHUMI na MAENDELEO YA UCHUMI. ukuaji wa Uchumi unapimwa kwa vigezo vya ongezeko la uzalishaji ndani ya mwaka katika nchi husika, bila kujali uzalishaji huo unahusisha watu wangapi, bila kujali ni wenyeji kiasi gani wanahusika.unapimwa kwa vigezo kama Kiasi cha uwekezaji, Mfumko wa bei, Mauzo nje, Manunuzi nje, Kiasi cha akiba(saving), Matumizi ya serikali, nk.

Maendeleo ya Uchumi yanapima ubora wa maisha ya watu. vigezo vyake ni kiasi gani mazingira ya uchumi yameboresha maisha ya watu, kama afya, elimu, maji, umeme, uwezo wa kumudu mahitaji, nk

Mkapa alikabidhiwa nchi ikiwa na mazingira magumu sana ya kiuchumi, lakini aliacha misingi imara ya kiuchumi. Kwamfano riba za bank ilikuwa alikuta zaidi ya 26% ameacha 14%,Akiba ya fedha za kigeni alikuta ya miezi miwili, akacha ya miezi7, JK akabakiza ya miezi4 na itaendelea kuwa ya miezi4 kwa hali ilivyo,alikabidhiwa nchi haikopesheki akaacha deni la 10trilion, JK ameacha zaidi40trilion na linazidi kupaa, changamoto pekee ambayo awamu ya nne ilipaswa kushughulika nayo ilikuwa kufanya ukuaji wa uchumi na misingi yake aloacha Mkapa itafsiri maendeleo ya uchumi kwa maana ya kuboresha maisha ya watu.

Awamu ya nne ilishindwa jukumu hilo kwa kiasi kikubwa na awamu ya tano haioneshi mwelekeo wa kupunguza maskini kwa kiasi kikubwa.

Sababu ya uchumi kukua bila kupunguza maskini ni pamoja na sekta zinazokua kiuchumi kubeba watu wachache au kuwa na athari ndogo kwa watu wengi.sekta ambazo ukuaji wake upo juu kwa miaka mingi ni Utalii, Madini, Mawasiliano, huduma za fedha, nk . ambazo kwa hakika zinabeba watu wachache.

Cha kufanya bado ni kuhakikisha kilimo katika dhana pana kinainuka, tangu miaka ya 2000s, Tafiti zilifanywa na Taasisi ya REPOA na kuonesha kwamba kilimo kikikuzwa japo kwa asilimia nane kwa miaka3 mfululizo kinaweza kupunguza idadi ya maskini kwa asilimia50%

Ni bahati mbaya kwamba kwa miaka yote kilimo hakizidi ukuaji ni asilimia3 ikianda sana 4% kwa zaidi ya miaka 20.na mbaya zaidi haionekani kama awamu hii inamsukumo katika eneo hilo.

Tafiti za REPOA zimeonesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya mbolea na tija katika kilimo.kwa mfano kijijini eka ya mahindi iliyolimwa bila mbolea wanavuna kati ya gunia 3 mpaka5.wakati eka iliyolimwa kwa mbolea mavuno ni gunia 20 mpaka30.hivyo mbolea inaongeza kwa kiasi kikubwa tija ya kilimo

Nasema awamu hii inaelekea haina mpango na wakulima kwasababu miaka yote tangu mfumo wa kutoa ruzuku kwenye mbolea, tija iliongezeka ingawa mbolea ilikuwa kiduchu.

Ripoti ya Poverty&Human Development ya 2014, inaonesha umuhimu wa sekta ya kilimo na hasa matumizi ya mbolea na kutoa mifano ambayo ni aibu kwetu.kwamba kwa wastani Mkulima China inatumia zaidi ya 260kg za mbolea kwa eka1, Tanzania tunatumia wastani wa 9kg kwa eka1.inawezekana tukawa na hoja kwamba China ni taifa kubwa kiuchumi, lakn ripoti hiyo inaonesha hata Malawi, nchi dhaifu kiuchumi, wastani mkulima anatumia 29kg za mbolea kwa eka1.
Sasa tujiulize, kama huo wastani wa 9kg kwa eka ni wakati ruzuku ya mbolea ilitengwa walau. je sasa? maana mwaka 2015/16 , ruzuku ya mbolea ilikuwa 78bn, wakati mwaka huu 2016/17 ruzuku ya mbolea imeshuka mpaka 10bn.

Nivema Mhe Rais akatazama upya eneo hili. kiasi hiki cha ruzuku ya mbolea hakifanani na serikali ya wanyonge. repoti ya USAID, 2014, inaonesha watanzania walio kwenye kilimo ni asilimia70% na kati yao asilimia75% ni akina mama.

Nikweli nikiwa bungeni tulisema sana kuhusu aibu ya Taifa kukosa ndege, binafsi nakubaliana na uamuzi wa serikali kununua ndege. lakini sikubaliani na uamuzi wa serikali kutekeleza mpango mkubwa wa kuwa na shirika kubwa la ndege sasa. Lazma watanzania wajue kuwa biashara ya ndege ni ngumu mno duniani.na nchi nyingi hapa Afrika zinaendesha biashara hii kwa hasara ikiwemo Afrika ya kusini, Rwanda yenyewe pamoja na kununua Airbus juzi, lakn wanakiri kuendelea kutengeneza hasara isipokuwa wana malengo ya muda mrefu, Kenya Shirika lao hoi kwa madeni, Walau shirika la ndege Ethiopia wana nafuu, Biashara ya ndege duniani kwasasa imezidi kuwa ngumu, tunaona fahari ya Emmirates, lakini nchi hizi za falme ya kiarabu zimeamua ku pump mabilioni ya kutosha kwenye ndege kuwa wababe wa dunia kwenye usafiri huo kama mbadala wa mafuta ambayo wanajua yatakwisha au bei itakwisha sana kadiri ya muda.Ndio mana unaona wana ubavu wa kutikisa mashirika kongwe ya Ulaya kama KLM au British Air, Hivyo hili la ndoto ya shirika kubwa la ndege maana yake tuwe tayari ku pump mabilioni ya kutosha kwa hasara ya miaka kadhaa . binafsi nakubaliana na ule msemo wa kupanga ni kuchagua. Je tunadhani hii inapaswa kuwa kipaumbele kiasi hicho? Nikweli ndio njia rahisi ya kuinua umaskini wa wanyonge? nadhani sio!

Uamuzi wa kutopandisha bei ya umeme kweli ni tija kwa wananchi na wenye viwanda, lakini naomba ieleweke tu kwamba Tanzania ndio nchi yenye bei ya chini ya umeme kuliko Rwanda, Kenya na Uganda. na ieleweke pia kwamba tatizo la viwanda Tanzania sio bei ya umeme bali umeme wa uhakika. sio affordability, but reliability. Pamoja na umeme wetu kuwa bei chini kiliko washindani wetu lakn kwasababu sio wa uhakika ni tatizo kwa viwanda kuliko hata nchi ambazo bei ipo zaidi yetu.

Pia ifahamike kwamba serikali inatumia fedha nyingi sana ya hazina ambayo ni kodi yetu kuliendesha shirika hili. zaidi ya 400bn kila mwaka ni ruzuku inakwenda Tanesco. hivyo tujue kwamba hata uamuzi wa juzi kuzuia bei kupanda, haina maana hauna madhara kwa wananchi kwani wanazuia bei kupanda na watapunguza bajeti ya elimu au dawa au kilimo au maji huko hazina ili kuibeba Tanesco. kwaiyo ni sawa na kusema tumekubaliana gharama za umeme tubebe wote wenye umeme na wasio na umeme badala ya kuachiwa mwenye umeme peke yake. ndio ruzuku za zaidi ya 400bn huku mbolea kwa wakulima inaenda 10bn..afu tunasisitiza kuinua wanyonge

Mhe Rais amefanikiwa kuutikisa mfumo kwa kuutisha, anatisha, mfumo ambao kwa miaka yote ulikuwa very rigid. hilo nampongeza. ushauri wangu ni aende mbele sasa kutengeneza Katiba itakayotengeneza mfumo unaotisha dhidi ya ufisadi na uzembe. kama nchi tunahitaji mfumo unaotisha zaidi kuliko mtu anaetisha kwasababu mfumo upo leo na kesho lakini mtu yupo leo kesho hayupo. kama alikuja Nyerere akaondoka, Mwinyi, Mkapa na JK, wote wameondoka kama yeye atakavyondoka, lakin mfumo hata akiondoka atauacha. atekeleze agenda ya Katiba Mpya kutengeneza mfumo madhubuti na sheria, kwa mfano saivi ilipaswa apeleke mabadiliko ya sheria ya utumishi wa umma ili mengi anayoyafanya kwenye utumishi yawe kwa mujibu wa sheria, asipofanya anaweza kuingiza hasara kwani watumishi wengi watakwenda Mahakamani na kushinda kesi na kulipwa mabilioni.

Mambo mawili niliyasema sana nikiwa bungeni. mpaka mkutano wa bajeti wa mwisho June7,2015 nilisisitiza ilikuwa ni suala la kampuni za simu na migodi kuorodhesshwa kwenye soko la mitaji.Napongeza uamuzi wa serikali sasa kwamba kampuni za simu zimelazimishwa kuorodhesha hisa zoa kwenye soko la mitaji la Dar es saalam(DSE).

Kwa Kampuni za simu kuorodhesha hisa zao ni fursa kwa umma kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hizi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. lakini zaidi ni inatoa fursa kwa hesabu za kampuni hizi kufanyiwa uchunguzi na uchambuzi wa kutosha(sereous scruitiny). na hivyo kupunguza uwezekano wa kampuni hizi kuficha usahihi wa mapato na matumizi yao, kwani kampuni nyingi duniani zina tabia za kukuza gharama za uzalishaji na kupunguza mapato yake kwenye vitabu ili zionekane zinapata faida kiduchu ili kupunguza kodi ya faida.

Jambo la ziada kwa kampuni hizj za simu ni TCRA ihakikishe inanunua mtambo kurekodi matumizi ya simu ya simu zote ili serikali iwe na hakika zaidi ya mapato ya kampuni hizi. tangu mwaka 2007, sijawa Mbunge hoja hii imezungumzwa bungeni, lakn serikali ilikuwa na uzito saana. kitu pekee ambacho TCRA walifanya ni kununua mtambo wa kurekodi simu za nje tu. ambayo ni asilimia ndogo sana ya matumizi. Hii ni tatizo kubwa ambalo nadhani linahitaji msukumo wa Rais kwasababu watu wake wanavuta miguu kutekeleza kwa karibu miaka kumi sasa

Nikweli hali ya mzunguko wa fedha kwenye uchumi ni mdogo sana. Nikweli kiasi fulani inatokana na serikali kuziba mianya ya dili. lakn tuseme kweli kwamba sio msingi wa ukubwa wa tatizo. kuna sababu nyingi, ikiwemo stracture ya deni letu na ulazma wa kulipa deni hilo. deni letu ni uwiano wa 80:20.

kwamba asilimia 80% ni la nje. na limeiva kwa kasi. kiasi kwamba kila mwezi serikali inalazimika kulipa wastani wa 700bn. wastani makusanyo ya ndani ni 1100bn. lakini pia kwa kipindi cha mwaka mmoja huu serikali imekopa sana ndani kiasi cha kuvunja rekodi ya miaka yote. serikali imekopa karibu trilion2. kuanzia Novemba2015 mpaka Disemba 2016.

miaka ya nyuma mikopo wa ndani kwa mwaka haikuwa inazidi 1trilion.na inakopa zaidi ndani kwasababu imekwama mikopo ya Ulaya. ndio mana umemsikia Waziri wa Fedha juzi akikiri kukosa mikopo nafuu na misaada toka Ulaya na kwamba wameamua kujielekeza nchi za Japan, China, Korea ya kusini, India,nk. sababu kubwa ya kukwama mikopo nafuu na misaada ni masharti ya siku zote kuwa Ulaya wanataka kuona demokrasia na utawala bora. ndio maana unamsikia waziri anasema mikopo mikwama kwasababu riba za ulaya zimepanda toka 6% mpaka 9% bila kusema huko upande wa pili riba ni kiasi gani?. tumevuruga uchaguzi zanzibar, sheria mbovu ya mitandao, vyama vya upinzani kuminywa na bunge gizani ndio siri ya ushirika wetu na ulaya kuchechemea.
Hali ni mbaya. tunajua sehemu kubwa ya miradi ya maendeleo inategemea misaada na mikopo nafuu toka nje. Baada ya kabanwa misaada na mikopo nafuu toka nje sasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka mzima ni chini ya 30% ya makisio ya bajeti. Hii ni kwa mujibu wa Monthly Economic Review Reports zinazotolewa na BOT kila mwezi. Makusanyo yetu ya mwezi yanaishia kulipa deni na mishahara tu

kama tunalipa 700bn, na mishahara 560bn, wakati makusanyo ni wastani ni 1100bn, unategemea nini? ndio maana kwa mujibu wa repots hizo MER za BOT, inaonekana deni la ndani wakati awamu ya kwanza inamaliza muda wake ilikuwa 1.7trilion, na kwa miaka10 ya JK deni la ndani likafikia 7.5trilion na mwaka mmoja huu deni la ndani limefikia 10trilion kwa maana ya nyongeza ya zaidi ya 2trilion

Kasi zaidi ya serikali kukopa ndani inapunguza kiasi cha pesa kwenye mzunguko. lakini kwakuwa haina namna inabidi iwe hivyo, na hii inachochea kuzidi kushuka kwa shughuli za biashara(austerity economy).

Binafsi naamini Rais ana dhamira lakin inakosekana focus , hajawa strategic kufikia lengo lake analojipambanua kama Rais wa wanyonge. asipoangalia miaka 5 itamalizika bila kupunguza makali ya maisha na kubaki na orodha ya waliotumbuliwa. Huyo mvuvi ameuliza kwanini uvuvi baharini bado haupewi msukumo. ndio msingi wa hoja yangu awali kwamba sekta ya kilimo katika dhana pana ambayo ni mazao, ufugaji na uvuvi, haijawa na msukumo

Tazama Nambia ukanda wa bahari kwajili ya uvuvi kwao una urefu wa 1500km na sisi 1400km, ni karibu sawa, lakn Namibia ndio wanaongoza kwa kuuza nje samaki ukanda wa kusini mwa afrika, na kwao baada ya madini,uvuvi ndio sekta ya pili ktk uchumi wao. Tunahitaji sera ya viwanda iwe ktk viwanda vya processing na mafacturing ya mali ghafi za kilimo. hivi ndio viwanda vinavyoajiri watu wengi dunian
Kuna point chache hapo zinashtua kidogo. Ukisema tunalipa wastani wa billion 700 kwa mwezi, kwa mwaka ni trillion 8.4 na miaka 5 ni trillion 40.2. Huo wastani unaishia lini? Si kweli tunalipa hivyo wakati wote. Kwa wastani huo na kama kweli ni wastani tungekuwa tumekwama.
Unasifia ndege kwamba na wewe ulishiriki kuzipigia debe, kisha una malizia kuponda. Unasema ATCL haitakiwi kuwa shirika kubwa kutokana na ugumu wa biashara na vipaumbele. Kama ulishiriki kupigia debe ununuzi wa ndege, na wewe una matatizo. Kifupi tunachoma pesa yetu. Wakati utasema ukweli.
Licha ya uhalisia na ugumu wa uchumi, baadhi ya maelezo yako hayapo sahihi. Uchumi umekuwa kipindi cha JK. Biashara licha ya kuwa za kifisadi zilishamiri. Waulize bodaboda au mama ntilie. Angalia miji ilivyokuwa kwa kasi na huduma ya usafiri.
 
Kafulila ni ushahidi kuwa katika uongozi elimu kubwa ni bure na zaidi anatuthibitishia kuwa CCM wamefikia kikomo katika kuongozo hii nchi kwani wameishiwa mawazo na ubunifu.
 
Mgonja again. Tafadhali ndugu. Hawa walikuwa wapiga dili maarufu, Kikwete pamoja na huruma zake aliamua kushughulika nao. Hata kama mtu alipona kwenye lile sakata lao, ukweli Upo wazi walitukomesha. Labda Mgonja mwingine.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpe Mgonja alifanya kazi nzuri sana akiwa katibu mkuu. Yeye aliachiwa na baada ya mahakama kumuona hana hatia. Ndugu Mgonja ndio alisimamia kikamilifu kuanzishwa kwa TRA na alipoondoka kama katibu mkuu aliacha hazina ina hali nzuri sana.
Mbona Proff. Muhongo alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow na baada ya kubainika hakuhusika aliteuliwa kuwa Waziri tena.
 
David ktk maelezo yake inaonekana anakubali uchumi kukua kwa wastani wa 6% to 7% ila anasema watu wasiojua dhana ya ukuaji wa uchumi wanaweka kataa takwimu hzo za ukuaji wa uchumi ningeshangaa sana kama David angepinga ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango hicho lakini niulize tu anasema mkapa aliacha deni la nje ni trillion 10 mwaka 2005 lakni ujatuambia riba ya kipindi hicho ilikuwa ni sh ngpi huko wanapokopa na sasa riba ni sh ngapi pia unatakiwa kujua exchange rate ya mwaka 2005 kurudi nyuma mpaka 1995 ilikuwa sh ngapi ? mkapa anaondoka bajeti ilikuwa ni Trillion 7 deni trillion 10 exchange rate ilikuwa ni 1000 na riba ilikuwa 13.9 kwa ndani cjuh kwa nje naimani nayo ilikuwa ni ndogo kulinganisha na sasa so kwa hesabu za kawaida tu mkapa alikuwa anakopa si kwamba alikuwa hakopi makusanyo yalikuwa ni 121.6 Billion kwa mwezi sasa mfano kama mkapa alikopa 10 milion usd na anayekopa 10 million usd leo kwa hesabu za kawaida tu tena bila ya riba aliyekopa kipichi hcho atarudisha sh billion 10 na huyu aliyekopa sasa atarudsha zaid ya billion 20 je uoni tofauti hapo kwa kukopa kiwango kimoja cha fedha na kurudisha viwango tofauti? na bajeti ya sasa ni trillion 23 tunaelekea 29.5 mwaka huu so uwezi tena kulinganisha mikopo ambayo mngekopa kwa bajeti ya trillion 7 za mkapa na sasa trillion 23 kwenda 29 za JPM

Wanasema kila nabii na zama zake uwezi kusema Musa ni bora kuliko Yesu kwani kila mtu alikuja dhama zake na changamoto zilizokuwa kipindi cha Yesu ni tofauti na zilizokuwa kwa Musa kinachotumaliza sisi ni Riba dhidi ya mikopo tunayokopa na bahati mbaya watunishi wa umma wanapiga deal tena kwenye hyo mikopo na kuongeza riba

Kila siku nasema tatizo hapa ni kuwa uchumi wetu unakua kwenye sector ambazo si rafiki kwa watanganyika hasa kwenye swala la ajira thanx to David kusema tena utalii,mawasiliano,madini,usafirishaji,huduma mahotel uchumi wetu ndo umebend huko dunia nzima hakuna nchi yenye uchumi mzurii wasiegemee kwenye viwanda na kilimo huko ndo kwenye tija zadi

Nyinyi mtakuwa mashaidi sera ya serikali ya Tanganyika kwa sasa ni Viwanda tunakata kutoka kwenye uchumi wa sector White - collar jobs kwenda kwenye sector yenye tija kwa watu wote wenye elimu kubwa mpaka wenye kujua kusoma na kuandika huko ndio tunakwenda
 
Ingekuwa umesoma hilo andiko na kulielewa usingeandika ulichoandika. Kinyume chake ungeandika justification ya ulichokisema. Msiwe mnakuja kujisaidia huku hiki sio choo.
Noted.
Tumbili hana jipya amehama Ukawa amehamia Ukawa baada ya kuwa Compromised na Mkewe.
 
tatizo la tanzania sio kilimo pekee watu wanalima lakini mazao yao hayawalipi , kwa kuwa hakuna sehem ya uhakika wa kuyapeleka mazao yao , tukishaakuwa na viwanda japo vichache vya kuwachakata mzai yetu kila mtu atavutiwa na kilimo
Ndugu Tatizo la kwanza ktk sekta ya Kipimo ni Tija. Mkulima anapata kiasi gani kwa Ekari ? Kama ndio anaambulia gunia 3-5 kwa Ekari Tambua hata akipata soko halitomlipa maana atapata bei gani ili hizo gunia 5 zilipe gharama y'a kutunza eka moja n'a kubaki n'a Faida?
 
Back
Top Bottom