shabanijuma
Member
- Aug 3, 2015
- 6
- 6
HOT MIX
Na Kilawa the Iron
Akihojiwa kwenye kipindi cha Hot mix ndani ya EA TV kuhusu uamuzi wa Warioba na baadhi ya viongozi wanaojipambanua kama wazalendo kuzunguka nchi nzima kumpinga Lowasa kuhusu ufisadi husan wa richmond , mbunge huyo alijibu;
"Kwanza watanzania waelewe kwamba kabla Lowasa hajapokewa alihojiwa kuhusu hili, na kwa mara ya kwanza aliweza kumhusisha JK na sakata hili kwa kiwango cha kutosha".
Kwa mfano, wakati nchi ikiwa kwenye msukosuko wa kusubiri mitambo ya richmond, JK alitua nchini kutoka marekani na kuzungumza na wanahabari na kuwapoza watanzania kwamba ametoka marekani na amekutana na wamiliki wa richmond na wamemuhakikishia kwamba siku chache mitambo ingetua nchini.
Swali la kujiuliza , Kamati ya Mwakyembe ilisema ilichunguza mpaka marekani hakuna mahala kampuni hiyo ilisajiliwa marekani, je Mhe Rais alikutana na nani marekani? Tumwamini Rais au Kamati ua Mwakyembe?. Alihoji Kafulila
Akisisitiza hoja yake, Kafulila alieleza kwamba maelezo ya Lowasa kwa umma kuwa alitaka kuvunja mkataba wa richmond mapema lakini Katibu Mkuu wizara ya fedha Mgonja wakati huo na Mwanasheria mkuu wa serikali Mwanyika wakati huo walisisitiza kuwa mamlaka za juu zilikataa bado haijakanushwa popote na Mgonja, Mwanyika, Rais mwenyewe na hata wasaidizi wake wa chama na serikali mpaka sasa. Hii inathibitisha kwamba aliebeba kampuni hii feki ni Mhe Rais Mwenyewe bila kupepesa maneno.
Aidha ukifuatilia maneno ya Mhe Mwakyembe bungeni kwamba yapo mambo walificha kulinda heshima ya serikali, unaweza kujiongeza tu, kama yaliyosemwa yalitosha Waziri mkuu kama mkuu wa serikali bungeni kuanguka, yaliofichwa yangemwangusha nani kama sio Rais?
Pamoja na hayo, Kafulila alisisitiza kwamba watanzania wakumbuke kwamba hasara pekee iliyopatikana katika sakata la richmond ni serikali kuipa zabuni kampuni feki na hivyo nchi kuchelewa kupata umeme kwasababu ilishindwa kuzalisha. Lakini serikali kama serikali haikulipa senti moja kwa kampuni hiyo kwakuwa haikutekeleza mkataba. Hii ni tofauti na masakata mengine kama ya mabehewa feki ambapo zabuni ilipewa bila kufanyiwa uchunguzi kama ilivokuwa richmond na bado na ikalipwa zaidi ya 230bn..na bado hatuoni uwajibikaji. Alisema Kafulila.
Kuhusu warioba na wengine wanaojiita wazalendo kumpinga Lowasa kwenye kampeni, Kafulila alisema Warioba anaweza kumpinga Lowasa kama mwana ccm lakini sio kama mzalendo kwani hana uhalali wa kuvaa viatu vya uadilifu wakati anahusishwa kwenye tuhuma za ufisadi wa 6bn kupitia scandal ya Mwananchi Gold zilizothibitishwa na PCCB na kupelekwa kwa DPP kwajili ya mashtaka kufikishwa mahakamani ingawa mpaka sasa zimekuwepo taarifa za Mhe Rais kuzuia DPP kufikisha mashtaka hayo mahakamani. Hivyo Warioba akienda kwenye kampeni ajiandae na hayo pia. Maana tunaambiwa ufisadi wa Lowasa lakini hakuna mahala uchunguzi wa chombo chochote kilichothibitisha baada ya kufanyia kazi kama ilivyo kwa warioba ambapo pccb imefanyia kazi na kubaini ukweli.
Kafulila alisema hata Sumaye alipokewa UKAWA ni mtu safi kwani hakuna mahala katika orodha ya matukio ya ufisadi wa awamu ya Mkapa utakuta jina la Sumaye. Na hapa ikumbukwe awamu hii ilikuwa na orodha ndefu ya matukio ya ufisadi kuliko awamu zote katika utawala wa nchi hii ikifuatiwa na awamu ya Kikwete. Alisema kuwa katika matukio mengi mawaziri wa mkapa na hata mkapa mwenyewe alihusishwa katika wizi akitolea mfano wa ufisadi wa mgodi wa KIWIRA. lakini hakuna tukio lolote utamkuta Sumaye wakati yeye ndio alikuwa msimamizi mkuu wa serikali.
Pamoja na kueleza kuhusu mafanikio ya jimbo kama mbunge na nafasi ya UKAWA katika uchaguzi huu ambao vyombo vya kimataifa kama ICC vinafuatilia kwa karibu. Kafulila alisisitiza uchaguzi wa amani, na kutaka makamanda wa jeshi la polisi kupuuza maelekezo ya kisiasa yanayotolewa na wanasiasa kuanzia ngazi ya taifa mpaka mikoa na wilaya ambapo kuna wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni wanasiasa lakini wanamlaka juu ya ma RPC na OCD Kwa maelezo kwamba maangamizi ya raia yatakapotokea watakaowajibishwa ni waliofanya mamuzi na sio hao walioelekeza kwa simu