Kadiri unavyoukimbia mwangwi ndivyo unavyoukaribia

 
Aha ha ha nani huyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Tabia ya uvundo hauvundi mpaka unuke sana. Na kadiri unavyoufutika mchagoni ndio kadiri unavyotoa harufu kali"
 
Kwani mbunge wa Kongwa anasemaje juu ya suala hili?
 
Gharama za matibabu ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, nchini India kwa kipindi cha miezi mitano kufuru!

Kwa uchambuzi wa ripoti ya CAG, Bw. Job Ndugai alikaa India kwa miezi mitano, sawa na siku 150. Kwa siku moja alilipwa posho ya dola 500 sawa na Sh. 1,160,100.00, na hivyo kwa miezi mitano alilipwa dola 75,000 sawa na Sh. 174,015,000.00.

Akiwa India alikuwa na wasaidizi wawili – maana alihamishia ofisi yake huko huko hotelini. Kwa gharama ya dola 450 sawa na Sh. 1,044,090.00 kila moja kwa siku, walilipwa dola 900 sawa na Sh. 2,088,180.00 kwa siku. Kwa siku 150 walizokaa India, walilipwa dola 135,000 sawa na Sh. 292,950,000.

Kwa ujumla, matibabu ya Ndugai kwa miezi mitano huko India yalitumia posho za sh. 466,965,000. na hapo bado gharama za hospitali huko India, na tiketi za ndege kwa watu wote hao, na bado gharama alizokuwa anatumia mkewe.

Takwimu hizi zilikuwa ni kwa mujibu wa ukaguzi wa CAG katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hospitali za India.

Wakati huo huo tusisahau kuwa Bw. Job Ndugai aliendelea kupata mshahara wake na posho zake kama Spika wa Bunge ambazo idadi yake naomba kama kuna watu humu wanazijua watusaidie kuzitoa.

Hakuna anayejua kwa uhakika Bw. Job Ndugai alikuwa anaumwa ugonjwa gani uliosababisha hadi ofisi yake ihamishiwe 5-star hotel nchini India ambako alichukua VIP suite nzima. Mpaka sasa gharama za matibabu yake ni siri kama ulivyo ugonjwa wake.

Ana apartments 78 dodoma,ivi CAG huku hafiki??

Mungu tupe nguvu....

Veronica France
 
mmmh hii kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…