Kabla ya kuwa Rais, Msimamo wa Magufuli ulikuwaje kuhusu mchanga wa madini?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,533
Nianze kwaa kumpongeza sana mheshimiwa Rais kwa kuwa mkweli na kuishi ukweli... Hakika hatatokea Rais mwenye hulka isiyo na mawaa ya kisiasa.

Kabla ya kuwaza kuwa mwanasiasa mkuu wa nchi hii, yaani Rais, Mheshimiwa Magufuli alikerwa mno na utaratibu huu unaoendelea hapa nchini wa kuruhusu mchanga kama by-product inayotokana na uchimbaji wa madini kupelekwa nje ya nchi..

Jambo hili alilikemea waziwazi kiasi cha marafiki zake kumtaka achukue form na kugombeaa urais. Ni bahati mbaya sana hatukuwahi kumsikiliza Magufuli kwa umakini juu ya huu msimamo wake wa kizalendo. Na ni bahati mbaya sana kwa sisi watanzania kuwa wasahaulifu au kushindwa kuwahukumu wanasiasa kwa matendo yao kabla na baada ya kutwaa madaraka.

------

UPDATE: LEO HII TAREHE 24-5-2017 RAIS MAGUFULI AMEPOKEA TAARIFA YA KAMATI YA MRUMA KUHUSU MCHANGA WENYE MADINI NA AMECHUKUA HATUA ZA AWALI ....
 
Kuna clip anasema/aliapiza watasaga meno.

Nasikitika kama kuna mkataba wa kisheria nachelea kuona kodi nayokatwa kwenye mshahara imaenda kulipa fidia kama ile ya meli ya wachina.
 
Hii ni mara ya pili JPM kuweka zuio la mchanga wa madini kupelekwa nje ya nchi.

Mara ya kwanza ilikuwa 31 julai mwaka jana. Na kama tujuavyo kauli ya raisi ni sheria, nabaki najiuliza vipi utekelezaji wa zuio la kwanza uliishia wapi mpaka aje atoe zuio la pili!!??
 
Miongoni mwa wabunge walio kuwa hawaongei mbungeni kujenga hoja magufuli ni mmoja wao zaidi ya wizara yake hajawahi kuzungumzia issue yoyote ya maendeleao zaidi ya samaki na mabarabara kuhusu kupinga ufisadi hajawahi ongelea hata suala la michanga hajawahi zungumzia acha kumpamba ni mnafiki
 
Tunaomba ushahidi wa hizo porojo zako .
Hio video hata mimi niliiona humu JF alikuwa site na wafanyakazi ,kama nakumbuka vizuri alikuwa anakataa kurekodiwa na simu lkn akakubali

Alisema anashangaa kwanini matajiri wasitengeneze viwanda ya kuchengenua mchanga ,kwanza faida wanapata wao pili taifa pia

Wale wafanyakazi wakawa wanacheka kwanini usigombe urais sasa

Tukiacha unafki hio video ipo. Humu jf niliiona

Magu kwahili kaonyesha msimamo wake
 
Tatizo lenu hamuelewi...na mnaonhozwa zaidi na mihemko badala ya akili....wapinzani walipokataa mchanga usipelekwe nje walimaanisha hiyo mitambo ya kusafisha iwepo ndani...sasa mfalme anakurupuka bila kuandaa mazingira...
 
Tatizo lenu hamuelewi...na mnaonhozwa zaidi na mihemko badala ya akili....wapinzani walipokataa mchanga usipelekwe nje walimaanisha hiyo mitambo ya kusafisha iwepo ndani...sasa mfalme anakurupuka bila kuandaa wamazingira...
wabunge wawezeshe hayo mazingira sasa
 
Hio video hata mimi niliiona humu JF alikuwa site na wafanyakazi ,kama nakumbuka vizuri alikuwa anakataa kurekodiwa na simu lkn akakubali

Alisema anashangaa kwanini matajiri wasitengeneze viwanda ya kuchengenua mchanga ,kwanza faida wanapata wao pili taifa pia

Wale wafanyakazi wakawa wanacheka kwanini usigombe urais sasa

Tukiacha unafki hio video ipo. Humu jf niliiona

Magu kwahili kaonyesha msimamo wake
Haya mambo hayafanywi kwa kukurupuka, sasa mnaiingiza nchi kwenye migogoro na wawekezaji bila sababu yoyote!
 
Bunge lilitunga sheria na kanuni zimekalika...ni kazi ya serikali sasa...na si kwa kukurupuka na kuzuia mchanga

Haya mambo hayafanywi kwa kukurupuka, sasa mnaiingiza nchi kwenye migogoro na wawekezaji bila sababu yoyote!
mwalimu nyerere hakutaka haya madini yachimbwe mpaka tujiridhishe na kuelimka katika sekta hii sijui ni setani gani katuingiza hapa?
 
Huu mtonyo wa mchanga alipewa zamani huko kwao na kina Kitwanga na wenzake, wakamshauri chukua form bwana magu akachekaaaaa, akapotezea kwa hiyo alikuwa amejua ukweli wote alikuwa anasubiri tu siku ya kuuweka hadharani..
 
Ikumbukwe pia kuwa.rais anaweza vunja any mkataba kama anaona aufai.na yupo na haki hiyo
 
Ikumbukwe pia kuwa.rais anaweza vunja any mkataba kama anaona aufai.na yupo na haki hiyo
Unachosema ni kweli kabisa. Lakini waliotengeneza mikataba walijua mapema pia kwamba anaweza kutokea mtu unreasonable akataka kuvunja mkataba kwa nguvu. Hivyo, wameweka vipengele katika Mikataba hiyo inayozuia jambo hilo, la sivyo anayevunja kwa nguvu ajutie maamuzi yake. Nakukumbusha tena, makampuni ya uchimbaji madini karibu yote ni ya nje ya nchi. Jaribu kuvunja mikataba hiyo uone kama bajeti yetu itatosha kulipa fidia.
 
Raisi as long as mkataba umesahiniwa Tanzania Kisheria anayo power kuvunja,ipo ktk katiba pia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom