Don Draper
Senior Member
- May 30, 2012
- 176
- 87
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?
Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?
Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?
iran hospitali zao ni kama za kwetu so wakija hapa wataweza kufanya kazi muhimbili...huwezi mtoa daktari kwenye hospitali za ulaya ukamleta hapa mazingira ya kazi yatawashinda
wewe unaishi dunia ipi? Iran na kwa kifupi nchi za jamii yake si zakujilinganisha nazo kabisa kwani wako mbali nasa katika kila sekta. achana na propaganda za magharibi. open your eyes and mind.Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?
Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?
Haya mambo ya kuambiwa huwa yanatufanya tudumae kwa kiasi fulani na kukosa kujua mengi sana.Nilianga Press TV ambayo ni ya wairani lakini lugha ya kingereza,na wanacho kipindi chao kinaitwa Iran today.Kwakweli nimepata kujua mengi kuhusu hawa jamaa jinsi walivo hodari kielimu na maendeleo.Mahospitali yao ni ya hali ya juu na ukija ktk usafiri kwa mfano Tehran wanazo treni za Under ground ambazo ni nzuri na safi na za kileo kuliko hata za London.Na ni mahodari wa kutunza historia zao.Kwakifupi sina wasiwasi nao hasa ktk utendaji wa kazi na labda itatusaidia na sisi kuboresha mengi ktk hospitali zetu.
Lakini kwa ushauri tu serikali iliangalie hili suala la mgomo wa madaktari wetu kwani hawa ni wananchi wenzetu na lazima wasikilizwe.Kama watachukua madactari wageni ina maana watanzania watakuwa hawana kazi tena kwasababu ya madai yao na ni ya msingi tu.Na je inamaana madaktari wa kigeni watafanya kazi milele hapa kwetu?Hapana lazima kunakitu ambacho kitaweza kurahisisha matatizo haya.
Press TV ni kama TBC yetu, wanaonesha yale wakubwa wanataka. Ndio Iran wamepiga hatua lakini sio kama ambavyo wengi wanataka tuamini. Wana watu kibao wanaochunga mbuzi kama sisi huku bongo, na meno machafu kuliko ya mnywa wanzuki.
Haya mambo ya kuambiwa huwa yanatufanya tudumae kwa kiasi fulani na kukosa kujua mengi sana.......Kwakifupi sina wasiwasi nao hasa ktk utendaji wa kazi...... na labda itatusaidia na sisi kuboresha mengi ktk hospitali zetu.
.
Nakubaliana na maelezo yako kiasi fulani; lakini hata hao madaktari "tumeambiwa ni madaktari kutoka nje" Je ni jinsi gani mwananchi wa kawaida ataweza kudhibitisha kweli ni madaktari na wala sio kundi la watu tu? Inaweza pia kuwa wanafunzi wanaosomea udaktari wanakuja for exchange program. Ni ukweli usiofichika wananchi wengi hawana imani tena na kile serikali inachosema; inawezekana serikali ikaleta wanafunzi wa medicine ( tena bila cost yeyote) wakatudanganya wame-spend 200 billion on them alafu pesa inaingia mfukoni kwa fisadi.
On a separate note; hii mambo yakuonyesha hospitali za Iran kwenye picha tunaambiwa ndio hospitali zao zilivyo, tunaamini vipi. Je hizo ni hospitali ni za serikali au private? Je hospitali zote ziko hivyo? Je huko Iran kuna matabaka/class? Je hao madaktari wanaokuja ndio 1st class (wanaothaminiwa huko) au ndio yale yale tu? Nafahamu Iran wako way far ahead of us, lakini tunachoonyeshwa kwenye TV/picha kinaweza kuwa sio ukweli halisi, au sicho tutakachokipata. Je ni chombo gani cha serikali kinaaminika kinachoweza kupima ubora wa hawa madaktari?