Kabla hawajatuletea madaktari, je hali ya maisha Iran ikoje?

TANESCO YAO IKIWA KAZINI

5686712998_08eb97deec_b.jpg
 
  • Thanks
Reactions: F2S
Katika madaktari wazuri duniani sijapata kuona ni wairan, wacuba, wasyria wako makini na ndio madoctor wanaokubalika hata marekani na ulaya. Wakati naishi marekani niliwahi kutibiwa na muiran nilifurahia sana huduma yake. Vile vile uingereza kuna rafiki yangu amewahi kutibiwa na muiran walifurahia huduma yake wako makini mno and highly intelligent!!!!

Watakapokuja mie nitakuwa wa kwenda kutibiwa naye wako makini mno
 
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?

Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?

Kwa ufupi tu hakuna hata nchi moja ya Ulaya Mashariki inaweza kuifikia Iran kiuchumi na kimaendeleo...kila kitu wanatengeza wao.
 
Nakubaliana na maelezo yako kiasi fulani; lakini hata hao madaktari "tumeambiwa ni madaktari kutoka nje" Je ni jinsi gani mwananchi wa kawaida ataweza kudhibitisha kweli ni madaktari na wala sio kundi la watu tu? Inaweza pia kuwa wanafunzi wanaosomea udaktari wanakuja for exchange program. Ni ukweli usiofichika wananchi wengi hawana imani tena na kile serikali inachosema; inawezekana serikali ikaleta wanafunzi wa medicine ( tena bila cost yeyote) wakatudanganya wame-spend 200 billion on them alafu pesa inaingia mfukoni kwa fisadi.

On a separate note; hii mambo yakuonyesha hospitali za Iran kwenye picha tunaambiwa ndio hospitali zao zilivyo, tunaamini vipi. Je hizo ni hospitali ni za serikali au private? Je hospitali zote ziko hivyo? Je huko Iran kuna matabaka/class? Je hao madaktari wanaokuja ndio 1st class (wanaothaminiwa huko) au ndio yale yale tu? Nafahamu Iran wako way far ahead of us, lakini tunachoonyeshwa kwenye TV/picha kinaweza kuwa sio ukweli halisi, au sicho tutakachokipata. Je ni chombo gani cha serikali kinaaminika kinachoweza kupima ubora wa hawa madaktari?

Sawa kama wasiwasi wako watakaoletwa ni madaktari feki hili ni suala la serikali yetu na ya Iran kwasababu kutakua na mikataba ambayo itakayosainiwa kisheria.Lakini usemi hapo juu unaashiria kwamba hiyo nchi ya Iran bado haina maendeleo na watu wanaishi maisha kama ya kwetu,sio kweli kwasababu tukumbuke hawa jamaa wanaishi zaidi ya miaka 30 wakiwa wamewekewa vikwazo vya kiuchumi tokea walivofanya mapinduzi.Wameishi kwa shida sana lakini kilichowasaidia wamekuwa wamoja na wamepata viongozi walio na uchu wa maendeleo na nchi yao.Hivo ikawafanya kuekeza ktk elimu zaidi amabayo ndio leo tunashuhudia maendeleo yao ndani ya nchi yao.Hawajabaguana pamoja na kwamba nchi yao wapo wakristo na mayahudi lakini kila mmoja amepewa haki zote zinazostahiki hasa ktk elimu mpaka elimu ya juu na bure.Pamoja na kuzidi kuwekewa vikwazo lakini leo hii wanaunda vitu wenyewe na kuziuza product zao nje ya nchi na kufanya ni moja ya nchi za kutegemewa.Angalia uchumi wao ulivo yaani nchi yao inajitegemea kwa asilimia 90 yani asilimia 10 tu ndio wanahitaji kutoka nje.

Hebu tuangalie hapa kwetu tulivo,kwasababu awamu ya kwanza haikufikiria kwamba elimu ni muhimu kwa wananchi hivo wangewekeza ktk elimu ili maendeleo yaje.Na hii nchi imebarikiwa na rasilimali chungu mzima lakini matokeo yake wanao faidika ni wa nje.Na hii inasababisha kunyimwa wananchi elimu na matokeo yake wenye elimu ni hao kwa hao na kupeana madaraka na kuendeleza uongozi uleule wa karne 100 iliyopita yaani kama vile yasiwepo mabadiliko yoyote na nchi iwe na wauza karanga wengi.

Kiufupi tu ukichunguza utaweza kuona madaktari wa kiirani wengi tu wanafanya kazi USA na EU na kwengine.Na hii ishu hatuna uhakika nayo kama kweli wataletwa madaktari wa nje na kama ni wa nje hatuna uhakika kama ni wa Iran.Lakini watu wamekuwa na jazba kwa kusikia wairan wanakuja na sioni kwanini sisi watanzania tunakuwa na kasumba ambazo hazitusaidii bali zinazidi kutushushia utaifa wetu,kwasababu kama maendeleo yenyewe ni 0 halafu tunajifanya kujua sana bila ya kipimo.Tuachane na hizi kasumba ili tuangalie matatizo tuliyo nayo kwa faida yetu wenyewe.
 
Press TV ni kama TBC yetu, wanaonesha yale wakubwa wanataka. Ndio Iran wamepiga hatua lakini sio kama ambavyo wengi wanataka tuamini. Wana watu kibao wanaochunga mbuzi kama sisi huku bongo, na meno machafu kuliko ya mnywa wanzuki.

Mkuu kumbe una karoho kawivu...Endelea kujidanganya eti kama sisi, hao wazungu wenyewe hawaifikii Iran...wanatengeza Silaha, Ndege, Magari, Sub Marine, wana rusha vyombo angani, utajiringanisha na Iran.
 
Ritz Unachekesha Ati Wanatengeneza Kila Kitu???naona Unahitaji Kujambishwa kthe Comedy Hita Cop and Paste... Hata wenyewe hawawezi kusema Wanatengeneza wao Unajua Irani ina waisrael waishio huko na wanapata huduma zote na kulindwa... ujuha wako peleka Nyumba nyeupe... Hakuna muirani mwenye Akili za hivyo hata Huyo Ahmedinajad Asili ake ni Israel na si Persian Nakuomba japo U google tu upate Darsa
 
Haya mambo ya kuambiwa huwa yanatufanya tudumae kwa kiasi fulani na kukosa kujua mengi sana.Nilianga Press TV ambayo ni ya wairani lakini lugha ya kingereza,na wanacho kipindi chao kinaitwa Iran today.Kwakweli nimepata kujua mengi kuhusu hawa jamaa jinsi walivo hodari kielimu na maendeleo.Mahospitali yao ni ya hali ya juu na ukija ktk usafiri kwa mfano Tehran wanazo treni za Under ground ambazo ni nzuri na safi na za kileo kuliko hata za London.Na ni mahodari wa kutunza historia zao.Kwakifupi sina wasiwasi nao hasa ktk utendaji wa kazi na labda itatusaidia na sisi kuboresha mengi ktk hospitali zetu.

Lakini kwa ushauri tu serikali iliangalie hili suala la mgomo wa madaktari wetu kwani hawa ni wananchi wenzetu na lazima wasikilizwe.Kama watachukua madactari wageni ina maana watanzania watakuwa hawana kazi tena kwasababu ya madai yao na ni ya msingi tu.Na je inamaana madaktari wa kigeni watafanya kazi milele hapa kwetu?Hapana lazima kunakitu ambacho kitaweza kurahisisha matatizo haya.
Iran ina maneeo inafanya vizuri ila bado si nchi ya kuweza tushawishi tuache mrafiki wengine wenye maana na maendeleo.Irani wasitufanye chambo wakati wamezidia,huku hawaheshimu ustawi wetu.Ni vipi watake support kwa kutulazimisha kuchukiwa na mtaifa yote muhimu duniani, halafu bado watudhalilishe kwa kutuvuga ndani ya nchi kwa kuwafadhili UAMSHO na kufadhili waandishi duni wanaoeneza propaganda za kubadili historia yetu na kuandika historia isiyo.Leo tuna watanzania wapuuzi wanatafuta watu wa dini yao katika kila chema cha nchi:Sijui uhuru wa nchi, sijui mwanzilishi wa hospital ya muhimbili, etc.
 
Hii ni data za Iran kutoka kwenye tovuti ya CIA, does it look like zama za mawe to you?

GDP (purchasing power parity):


$928.9 billion (2011 est.)
country comparison to the world: 18
$906.2 billion (2010 est.)
$877.6 billion (2009 est.)
note:data in US dollars


GDP (official exchange rate):
$480.3 billion (2011 est.)


GDP - real growth rate:
2.5% (2011 est.)
country comparison to the world: 142
3.2% (2010 est.)
3.5% (2009 est.)


GDP - per capita (PPP):
$12,200 (2011 est.)
country comparison to the world: 99
$12,100 (2010 est.)
$11,900 (2009 est.)
note:data are in 2011 US dollars

GDP (purchasing power parity):
$928.9 billion (2011 est.)
country comparison to the world: 18
$906.2 billion (2010 est.)
$877.6 billion (2009 est.)
note:data in US dollars


GDP (official exchange rate):
$480.3 billion (2011 est.)


GDP - real growth rate:
2.5% (2011 est.)
country comparison to the world: 142
3.2% (2010 est.)
3.5% (2009 est.)


GDP - per capita (PPP):
$12,200 (2011 est.)
country comparison to the world: 99
$12,100 (2010 est.)
$11,900 (2009 est.)
note:data are in 2011 US dollars
 
Mkuu picha ulizoweka zinatosha... Ni kichekesho mbongo analinganisha bongo na Iran.. hahaha..
 
Iran iko Masafa. Huwezi kulinganisha Iran na Tanzania huo ni ukweli wa wazi.

Suala hapa si Madakatari kama ambavyo rais kikwete Waziri mkuu Mizengo na Spika wa Bunge Bi Makinda wanavyolazimisha kila mtu aelewe hivyo.

Tatizo la Hospitali zetu ni Ukosefu wa kutisha wa vifaa katika Hospitali zetu. Madaktari tunao siyo wengi sana Takwimu zinasema Hapa Tanzania kuna dakari 1 kwa kila watu 50,000 na nchi yetu ni moja katika nchi 10 ambazo close to 95% ya watu wake income yao iko chini ya $2.00 a day Tshs 3200.00. Kuna watu kati ya 2.5Millini - 3.0Million wenye income za kueleweka Tanzania.

Wairan hawawezi kuja na majengo yao na zana zao hapa Tanzania, watakuja na vichwa vyao kutoa huduma.
Sasa wakifika wakute hata maji hakuna, vyoo vimeziba X ray hazifanyi kazi CT Scan MRA Ultra sound zote mbovu na hazitoshelezi sijui wao ndo watakubali kufanya kazi kwenye mazingira hayo??

Serikali ya Kikwete ina linda UDHAIFU wake kwa kuhakikisha kwamba haisalimu Amri juu ya suala la Mazingira duni na yasiyo faa ya hosipitali zetu.
UDHAIFU wa serikai ya Kikwete unalindwa kwa gharama zote kwa sababu ndiyo asili hasa ya UTUKUFU wao. Udhaifu wa serikali ya Kikwete ndiyo unao zaa Mawaziri Mabilionea, Majaji Mabilionea Makamishna wa Polisi mabilionea Wafanya Biashara Mabilionea, na Makampuni yenye mikataba dhaifu.
UDHAIFU wa serikali ya CCM ndiyo umempa Edward Lowassa Mabillioni ya Tshs ambazo sasa anahonga Wachungaji, Mashemazi Maaskofu Masheikh na waumini wa dini mbali mbali kila pembe ya Tanzania katika harakati zake za kuwani U Rais mwaka 2015.
UDHAIFU ni Muhimili wa katikati wa serikali ya CCM Ikulu ya Kikwete na Ofisi ya Waziri mkuu Pinda.

The strongest system is as strong as the weakest point.

Ili kuhakikisha system yeyote ile haingiliwi kirahisi ni lazima system ile iutambue udhaifu wake mkuu na kuulunda at all costs.

Rais Kikwete na serikali yake wanajua fika udhaifu wao. Pia wanajua fika kwamba udhaifu huu ni sehemu muhimu sana ya system yao kwa hiyo wakikubali udhaifu wao uende na maji maana yake system nzima inakwenda na maji.Udhaifu huu ni lazima ulindwe kwa gharama yeyote hata kama ni damu ya 30% ya Watanzania wote. Kwa sababu kanuni kwamba hakuna mfumo ulio imara zaidi ya udhaifu uliopo katikati yake, maana yake ni haki mfumo wowote wenye udhaifu kugharamia kwa hali na mali kuulinda UDHAIFU ulio sehemu muhimu ya mfumo wake. Ili kundi hili la Watawala wetu waendelee kuwepo kama Chama, kama serikali na Kikwete binafsi aendelee kuwa rais ni lazima waulinde UDHAIFU wao kwa nguvu zao zote na kwa akili zao zote. Hili jambo la UDHAIFU ni jambo very sensitive kwanza kwake yeye Kikwete mkewe na familia nzima Pili kwa serikai yake na lumbesa ya watu aliowateua na Tatu kwa wabunge wote wa CCM. Kila anufaikaye na system hii ni wazi kwamba atatumia nafasi yake kuulinda UDHAIFU huu ili aendelee kuneemeka.


Ili kulinda heshima ya UDHAIFU wa serikali ya CCM ni muhimu kutumia fedha nyingi kuleta madaktari kutoka nje ya Tanzania. Lakini je wataendelea kuulinda udhaifu huu mpaka lini na kwa gharama kiasi gani??
 
May be it is because you dont like Iran.

If Iran is still in Stone age then by comparison Tanzania does exist amongst the apes.

Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?

Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?
 
Upo dunia gani wewe? eti umeambiwa kumbe hujui kitu....IRAN sio wenzetu ata kidogo fatilia documentary mbalimbali na utaona GREECE AND PERSIAN ndo elimu toka zama na zama imelala....IRAN wanaexport all medicines including medical equipments na mgogoro wao mkubwa ulikua ni shida ya ku import vifaa vya kutibu cancer kwani hii technology ilikua kwa nchi za magaribi km vile huduma za mionzi na ndo mwanzo kutrain watu wao kwenye nuclear issue kwani wagonjwa wa cancer matibabu yake ni miionzi ya nuclear....IRAN ana export vifaa mpaka kwa nchi ULAYA mfano GERMANY ameoda meli kubwa toka IRAN sasa hao utajilinganisha nao na walikua km sisi tu lakini wamewekeza ktk elimu...Tembelea websites zao kwenye ishu za technology na last year ndo ilikua leading nation kwa kuchapisha vijarida vingi vya sayansi...wenzako wanategemea by 2017 warushe asrtonomy ktk sayari, wanaexport ndege,magari,meli,silaha mbalimbali na optical obejct eg binocular,lenses na upuuzi mwingine....Hawa sio waarabu hawa ni wapersia bro

....sidhani kama iran wamewahi kuwa kama sisi( kama ulivyosema) hata mara moja...tanganyika kama nchi ilianzishwa mwaka 1884, na tanzania mwaka 1964...iran ni moja kati ya mataifa yenye historia ya miaka mingi, ikitajika kwenye biblia na ktk mafundisho ya kiislam.wakati wa vita baridi iran ilikuwa ndio rafiki wa pekee wa marekani na nato ambae alikuwa mpakani na ussr, na akiandaliwa kujihami dhidi ya hujuma yeyote ya ussr.makamanda wa kushindwa vita hitler na marekani na washirika wake ulisainiwa tehran...unazungumzia nchi ambyo raisi wake amepewa mamlaka na katiba yao kuamua matumizi ya takriban dola za marekani zisizozidi miliioni mia mbili kwa siku...!ni kujionea kufikiria kujilinganisha nao kihistoria au hata ktk kipindi hiki...
 
Iran ina maneeo inafanya vizuri ila bado si nchi ya kuweza tushawishi tuache mrafiki wengine wenye maana na maendeleo.Irani wasitufanye chambo wakati wamezidia,huku hawaheshimu ustawi wetu.Ni vipi watake support kwa kutulazimisha kuchukiwa na mtaifa yote muhimu duniani, halafu bado watudhalilishe kwa kutuvuga ndani ya nchi kwa kuwafadhili UAMSHO na kufadhili waandishi duni wanaoeneza propaganda za kubadili historia yetu na kuandika historia isiyo.Leo tuna watanzania wapuuzi wanatafuta watu wa dini yao katika kila chema cha nchi:Sijui uhuru wa nchi, sijui mwanzilishi wa hospital ya muhimbili, etc.

Kwakweli topic ipo tofauti na haya maoni yako lakini kwa kukujibu machache ni kwamba hakuna taifa moja au mawili muhimu ila mataifa yote hata sisi taifa letu ni muhimu tena muhimu sana kwasababu hata hao unaowaita muhimu wanatutegemea sisi japo kuwa unaona sisi ndio tunapeleka bakuli huko kwao.Na hakuna nchi itamlazimisha nchi nyingine kuunga urafiki ila kwa hiyari ya nchi.Uchumi wetu hivi sasa ni mbaya sana kama uulivo kwa mataifa mengine kwahiyo pengine sisi tunapata mafuta kwa muiran kwa bei rahisi na hao unaowaita mataifa muhimu watulazimishe sisi wapi tununue au wapi tusinunue kwasababu ya ugomvi wao kwakweli huo ni utoto mimi nauita.Nchi yetu haijafungamana na upande wowote kwahivo ni vizuri mataifa yakaheshimiana kwani mafuta yakiadimika au tukinunua kwa bei ya juu ni sisi ndio tunaathirika na kuanza kuomba omba.
 
Ritz Unachekesha Ati Wanatengeneza Kila Kitu???naona Unahitaji Kujambishwa kthe Comedy Hita Cop and Paste... Hata wenyewe hawawezi kusema Wanatengeneza wao Unajua Irani ina waisrael waishio huko na wanapata huduma zote na kulindwa... ujuha wako peleka Nyumba nyeupe... Hakuna muirani mwenye Akili za hivyo hata Huyo Ahmedinajad Asili ake ni Israel na si Persian Nakuomba japo U google tu upate Darsa

Wewe kweli Duduwasha hujui chochote kuhusu Jomhuri-ye Eslam-ye Iran...nimecheka eti Iran mafanikio yake kuna Waisrael wanawapa huduma zote ha haa haaa! JF sio sehemu ya porojo weke ushahidi hayo maneno yako!

Halafu Ahmedinajad ndani ya Iran hana sauti yoyote..unamjua Reza Shah, Kashafrud, Ganj Par, soma historia ya Iran au pita kule kwenye jukwaa la Great Thinkers Nguruv3 kawaelezea kidogo wa Iran.

Iran adui yake mkubwa ni Israel na hawalitambui taifa la Wasrael leo wewe unatuletea stori za kwenye vijiwe vya mbege eti mafanikio yao ni Wasrael, Nuclear program of Iran wameanza toka 1950, kazi kubwa wamefanya kina Ayatollah Khomein na wenzake.
 
Kwa jinsi nilivyoona hzo picha za hospital zao,, sidhani kama hao madoctor watakuwa na uwezo wa kufanya kazi katika hizi hospital zetu kwasababu kubwa mbili
(i)mazingira mabovu na
(ii)ukosaji wa vifaa
kwahiyo tusishabikie ujaji wao hapa kwetu bila kufikiria mazingira yao waliyoyazoea na mazingira ya kwetu ambayo ndio chachu kubwa a kufanya kazi kwa ufanisi mzuri


nawakilisha//
 
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?

Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?

Mtaje aliyekwambie. Tuna tatizo la kuzisema tetesi kama zilivo bila hata ku edit!
 
Back
Top Bottom