Dar es Salaam. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaonya wale wote wanaojihusisha na utapeli wa ajira jeshini kwamba wataendelea kuchukulia hatua kali zaidi.
Pia, JWTZ imesema kesho April 6, 2018, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli atazindua ukuta wa machimbo ya madini wa Mirerani mkoani Manyara.
Hayo yamesemwa leo April 5, 2018 na Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali Ramadhan Dogoli wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi hilo, Upanga-Dar es Salaam.
Amesema kuna baadhi ya majangili hujifanya ni watumishi wa jeshi na kuweza kuwatapeli wananchi kuhusu ajira
Hatua kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya mapateli hawa kwani hatuwezi kuwafumbia macho," amesema.
"Kwa askari ambao tumekuwa tukiwabaini, adhabu ndogo kabisa ni kuwafukuza kazi na wengine wanafikishwa mahakamani. Kwa hiyo wananchi wanapaswa kuwa makini."
Kuhusu uzinduzi wa ukuta, Kanali Dogoli amesema shughuli itaanza saa moja na wananchi wanakaribishwa kushuhudia uzinduzi huo.