R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,578
na Sitta Tumma, Tarime
ZAIDI ya nyumba 100 zimeteketezwa kwa moto na watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Serengeti katika vijiji vya Chegonga, Masanga na Kibasu wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.
Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, askari wa JWTZ walitembeza vipigo kwa baadhi ya wananchi, akiwemo Diwani wa kata ya Nyanungu, Mustafa Masiani (CHADEMA), ambaye anadaiwa hali yake ni mbaya na amelazwa katika Hospitali Teule ya wilaya mjini Bunda.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Oktoba 14, mwaka huu, ambapo wananchi hao wanadaiwa kujenga ndani ya Hifadhi ya Serengeti.
Wanajeshi hao walikuwa wamevalia sare za JWTZ wakiwa na magari sita ya serikali, walifika eneo hilo kisha kuanza kuchoma moto nyumba hizo kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa operesheni ya kupambana na majangili katika hifadhi za wanyamapori, iliyotangazwa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa waliochomewa nyumba zao walikuwa wakiishi nje ya mpaka wa hifadhi hiyo ambao ni Mto Mara.
Ni kweli nyumba zaidi ya 100 zimechomwa moto na watu waliokuwa wamevalia magwanda ya JWTZ. Inavyoonekana waliochomewa hawaishi ndani ya hifadhi. Ila tunaona ni kama unyanyasaji wa raia maana hata jana kuna mtu amepigwa hadi kuuawa na askari, kwa sababu ya operesheni hii.
Mpaka wa Tarime na Hifadhi ya Serengeti ni Mto Mara, na walikuwa wakiishi bonde la Nyanungu, ambalo serikali inadai ni eneo la hifadhi lakini wananchi tunavyoelewa si eneo la hifadhi, alisema Chacha Heche na kuungwa mkono na Ernest Bagige mkazi wa Muriba - Tarime.
Mmoja wa viongozi wa serikali katika maeneo yaliyoathirika na tukio hilo, ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alikiri kuchomwa kwa nyumba hizo na watu waliokuwa wamevalia sare za JWTZ, na kwamba tukio hilo limelalamikiwa na watu wengi sana.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Julai 22, mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa, alitembelea maeneo hayo kisha kuzungumza na wananchi hao akiwataka wahame kwa hiari yao, kwa madai kwamba eneo hilo ni Hifadhi ya Serengeti.
Julai 22, mkuu wa mkoa alikwenda kuzungumza na wananchi waliochomewa nyumba zao majuzi. Aliwataka waondoke kwa hiari yao, lakini wananchi nao walimkatalia wakisema wanaishi nje ya hifadhi, alisema.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, alisema yuko likizo mkoani Morogoro.
Alisema anachojua kuna watu walijenga ndani ya hifadhi, na kwamba kama wamekumbwa na tatizo hilo ni kwa sababu ya kuingia ndani ya hifadhi ya taifa.
Tanzania Daima