Kweli kabisa hakuna kushangilia wala kuchekelea historia inaonyesha Mawaziri wote walio wahi kushitakiwa walishinda kesi zao,
1 ) Fundikira alifikishwa mahakamani baada ya kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa miaka michache tangu Tanganyika ipate uhuru.
Hata hivyo, alishinda kesi.
2 ) Venance Ngulla, aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya pili katika miaka ya 1990. Ngulla alikamatwa na kufikishwa mahakamani katika miaka ya 1990,
naye alishinda kesi.
3 ) aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Nalaila Kiula, katika serikali iliyokuwa chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika miaka ya 1990. Kiula alikamatwa na kufikishwa mahakamani chini ya uongozi wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwa tuhuma za rushwa. Hata hivyo,
naye pia alishinda kesi.
4 ) Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya pili, Augustine Mrema naye alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatuhumu hadharani baadhi ya viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali kwamba, wamepokea rushwa yenye thamani ya Sh. milioni 900.
Hata hivyo, naye alishinda kesi.
Je na hawa hata hivyo watashinda kesi ? Ikiwa mmoja mmoja waliweza kushinda kesi je hili genge zima ? Tumesikia wakubwa wakisema kuwa watu wanaohusika ni hatari au kasheshe la safari hii ni hatari kudili nalo ,je kwa kuanza kufikishwa mahakamani ndio tuamini kuwa hatari ambayo wakiiogopa au wakiisema ndio imeshadhibitiwa. Tatizo tumepelekwa kwenye EPA wakati kuna majanga ya ubadhirifu ambayo inaonekana kutaka kufunikwa na hili la EPA ,ni lazima wananchi waamke ,mahakama kunaweza kuendeshwa kesi tofauti kwa wakati mmoja ,tunataka wadau wadai na kesi zingine za ubadhirifu zianze kunguruma , hakuna kulala mpaka kieleweke.Ndio utawala bora ulivyo ,ni madai tu.
Kwa kukumbusha tu kuna majina ambayo tulikuwa tukiwasikia wakubwa kuwa wanayo ,majina ya wale watu wa unga ,naona tatizo limezimika ghafla na hatuwasikii tena , wabunge mnayo kazi ya kuwakumbusha viongozi wamefikia wapi na listi ya majina ya vigogo wa unga.