Juni 01,2020: Maadhimisho ya Siku ya Maziwa Duniani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Juni 01 kila mwaka ni Siku ya Maziwa Duniani ambapo lengo kubwa huwa ni kuelimisha jamii kuhusu maziwa na umuhimu wake kama chakula ulimwenguni

Siku hii ilianzishwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) ili kutambua umuhimu wa maziwa na imekuwa ikisherehekewa kila Juni 01 tangu mwaka 2001

Kwa miaka michache iliyopita, India imetajwa kama mzalishaji mkubwa zaidi wa maziwa duniani ikizalisha zaidi ya tani Milioni 150. Maziwa na bidhaa za maziwa ni sehemu kubwa ya maisha nchini humo

Mwaka huu, kaulimbiu inasema "Miaka 20 ya Siku ya Maziwa", na kutokana na janga la CoronaVirus hakuna hafla kubwa zilizoandaliwa lakini washiriki wametakiwa kuzungumzia umuhimu wa maziwa pamoja na matatizo ya upatikanaji wake katika maeneo mbalimbali duniani

Hapa nchini, Naibu Waziri wa Kilimo na Ufugaji, Abdalah Ulega amesema kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ni wastani wa lita 47, kiwango ambacho ni kidogo kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO)

Naye Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Sophia Mlote amesema sekta ya maziwa Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kodi ambazo huongeza gharama za uzalishaji

====

1590990467459.png


June 1 is observed as World Milk Day with the aim to raise awareness about milk and its importance as a global food.

In the last few years, India has become the largest producer of milk in the world with over 150 million tonnes of production and per capita availability of over 300 grams per day.

Established by the Food and Agriculture Organization (FAO) of the United Nations to recognize the importance of milk as global food, World Milk Day is been observed on June 1 each year since 2001.

World Milk Day 2020 Theme

This year, the initiative has completed 20 long years, the theme is simply called 'the 20th Anniversary of World Milk Day'. Due to the COVID-19 pandemic, no major events have been organised by the committee but the Global Dairy Platform has been asking the participants to talk about the benefits of dairy and along with highlighting the problems in accessing milk and dairy products in several parts of the world.

Significance of World Milk Day

World Milk Day in India especially is celebrated with a lot of enthusiasm. Mik and dairy is a major part of lives in India and this day gives them the opportunity to discuss various aspects of milk & dairy products in India.

The day encourages the benefits of dairy products related to health and nutrition, effectiveness and attainability, and the passion of the sectors and commitment to feeding our communities.

Vice President of India, M. Venkaiah took to twitter to wish people on the occasion of World Milk Day. "Greetings on World Milk Day.The day recognizes the importance of milk as a global food, and celebrates the dairy sector.India being the largest milk producer in the world, dairying holds a special place in our rural economy. #WorldMilkDay", he wrote

Greetings on World Milk Day.

The day recognizes the importance of milk as a global food, and celebrates the dairy sector.

India being the largest milk producer in the world, dairying holds a special place in our rural economy. #WorldMilkDay pic.twitter.com/yGI7IqudQv
— Vice President of India (@VPSecretariat) June 1, 2020

To make this day even more special, donate milk packets to people who are in need due to the outbreak of coronavirus.
 
Hapa Tanzania nasikia kuna bodi ya maziwa, sijui inahusika na kitu gani?

Mara bodi ya nyama, sijawahi kusikia bodi ya dagaa au bodi ya mboga mboga kama mlemda, spinachi, sukuma wiki, kabeji, matembele, mchicha, na mambo kama hayo.
 
Ulega amesema kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ni wastani wa lita 47, kiwango ambacho ni kidogo kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO

Je kiwango sahihi ni kipi?
 
Maziwa ni anasa kwa Watanzania tulio wengi. Huwa nakunywa mtindi lakini maziwa fresh sijanywa siku nyingi na Wala sioni kupungukiwa kitu
 
Sikuwahi kuijua siku hii.
Sipendelei kunywa maziwa lakini usiku wa kuamkia leo nimekunywa karibu lita 1 ya maziwa. Kumbe nilikuwa nasherehekea sikukuu ya kunywa maziwa duniani bila kujua.
 
Maziwa ni anasa kwa Watanzania tulio wengi. Huwa nakunywa mtindi lakini maziwa fresh sijanywa siku nyingi na Wala sioni kupungukiwa kitu





KWANI UFIPA SI WANA FUGA NGOBE WA MAZIWA KWA WINGI HUWA HAMKUMBUKANI HATA KIDOGO:):):):):):):)
 
Back
Top Bottom