Jumuiya ya vijana CUF (JUVICUF) yawaomba waandishi wa habari kumsusia Lipumba kama Makonda

Nabihu

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
293
109
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

*JUMUIYA YA VIJANA YA CUF ( JUVICUF )*

*LIPUMBA asusiwe kama alivyosusiwa makonda*

Kwanza nianze kwa kuwapongeza wanahabari hususani chama cha wamiliki wa vyombo vya habari kwa hatua nzuri na madhubuti mliyoichukua ya kuzuia habari zinazomhusu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Poul Makonda kutorushwa wala kutangazwa katika vyombo vyenu .

Hatua hiyo ni sahihi na imeichukua katika wakati muafaka ili kulinda uhuru wa tasnia hii muhimu kwa maendeleo na Ustawi wa taifa lolote lile duniani.
Ni wazi kwamba Kitendo kilichofanywa na mkuu huyo wa mkoa kimelitia doa taifa letu kwani Si cha kiungwana na wala hakijazoeleka katika mataifa yote yanayoendeshwa na serikali za kidemokrasia zilizo na katiba zinazolinda misingi ya utawala bora na utawala wa sheria. Ni ukweli usiofichika kua makonda ameitia doa kubwa nchi yetu na Laiti kama mamlaka iliyomteua ingekuwa inapenda kushauriwa basi makonda alipaswa hivi sasa Si kiongozi tena wa mkoa huo.

Kuhusu lipumba.
Ndugu wana habari, ni mda mrefu sasa chama chetu cha cuf kimekuwa katika mgogoro wa ndani kuhusu uhalali wa lipumba kuiongoza cuf. Mgogoro huu nyinyi mnaufahamu asili yake na chanzo chake . Ni mgogoro ambao kimantiki umepandikizwa na dola ili kuivuruga nguvu na kasi ambayo cuf inayo na imeipata mwaka 2015 baada ya uchaguzi mkuu. Yanayoendelea kufanywa hivi sasa na mtu anaeitwa lipumba ni kielelezo to sha kuwa lipumba yupo kazini kuhakikisha kuwa anaharibu nguvu ya upinzani nchini.

Ni mambo mangapi anayafanya yanaishangaza jamii yetu hapa nchini na hata jumuiya za kimataifa! !. Cuf inaongozwa na katiba na kanuni zake lkn lipumba anaivuruga cuf bila kutumia katiba wala kanuni ili mradi bosi wake afurahi. JUVICUF inahoji kwanini wanahabari msifanye juhudi za makusudi za kuisoma katiba ya cuf ipasavyo na kuielewa ili baada ya hapo mkaamua kuchukua hatua madhubuti dhidi ya upande ule unaovuruga chama na demokrasia kwa ujumla? .

Kwanini jukwaa la wahariri wasichukue juhudi za makusudi za kupata ufafanuzi wa kikatiba kutoka pande zote mbili ili jukwaa likaamua kumpuuza yule anae haribu chama? .Au jukwaa nalo lina subiri kesi iamuliwe mahakani ndipo iamue kuandika taarifa za upande mmoja? .

JUVICUF tunaona jukwaa linaweza kutafuta ukweli wa jambo hili kabla ya mahakama ili kusaidia kupunguza vurugu zinazo fanywa na lipumba na kundi lake katika kuuwa demokrasia ya vyama vingi nchini. Ni wazi kuwa JUVICUF tunajua kuwa nyinyi wanahari mnafahamu kuwa mapambano haya yaliopo cuf yana athari kubwa katika jamii na taifa kwa ujumla. Mnajua namna watu walivyohangaika miaka yote kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na demokrasia ya vyama vingi vilivyo na nguvu na hoja ili kuifanya serikali iliyo madarakani kuwa macho na kuwajibika kisawa sawa mda wote. Haya yanayoendelea kufanywa na lipumba ni usaliti wa wazi kwa watanzania ambao juhudi zao za kipindi kirefu zinafifiwa na maslahi binafsi ya mtu mmoja.

Ndugu wanahabari JUVICUF tunatoa wito kwa jukwaa la wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kumpuuza lipumba kama ambavyo mmemsusia Makonda kwa kutotoa habari zake kwani hao wote wawili wanafanya kazi moja ambayo ni usaliti dhidi ya raia na usaliti kwa taifa. Wakati mmoja anaharibu uhuru wa vyombo vya habari mwingine anaharibu Uhuru wa raia katika demokrasia ya vyama vingi.

Ninawashukuru sana

*Hamidu Bobali*( MB)
*Mwenyekiti wa Taifa JUVICUF*
 
Back
Top Bottom