Wananchi washiriki vipi? Kwa kutoa pesa au kushika fagio na koleo? Na kodi tunayolipa inafanya kazi gani? Kwanza majumbani kwenu ni pasafi? Kabla ya kwenda nje ya nyumba zetu, tuanzie majumbani mwetu. Kagua leo nyumba yako kama hautakuta tandabui, majani mengi nje ya nyumba, rangi ya choo si ile wakati choo kipya!! Halafu wewe mwenyewe mfano umekata kucha zako au kucha zako ni fupi, unapiga mswaki mara ngapi kwa siku?