Juma la wasiwasi kuhusu Marekani na Korea Kaskazini

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Ukafuatilia matukio, mijadala na ujumbe katika mitandao ya kijamii, unaweza kudhani Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia vinakaribia.

Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wamekuwa wakijibizana vikali kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kuendelea kustawisha silaha za nyuklia na pia kufanyia majaribio makombora, jambo ambalo taifa hilo haliruhusiwi na Umoja wa Mataifa.

Marekani ilituma kundi la meli zake za kivita karibu na Korea Kaskazini, jambo ambalo liliikera Korea Kaskazini.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili haujakuwa mzuri tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Hata hivyo wiki iliyopita uhasama ulizidi na kufikia kiwango cha juu kuliko awali.

Rais Trump aliagiza kundi la meli za kivita za Marekani pamoja na meli moja yenye uwezo wa kubeba ndege na pia kutumiwa na ndege hizo kupaa na kutua, zielekee upande wa Korea Kaskazini.

Taifa hilo limetekeleza majaribio kadha ya silaha za nyuklia na hilo halijaifurahisha Marekani.

Rais Trump alisema Marekani imejiandaa kuchukua hatua kivyake, bila usaidizi wa China, kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

Wizara yake ya mambo ya nje ilinukuliwa ikisema hatua hiyo ya Marekani ni ya "kipumbavu" na ikaahidi kujilinda "kwa nguvu zote za kivita."

China, ambao ni mshirika wa karibu zaidi wa Korea Kaskazini, walionya kwamba wataingilia kati na kutoa adhabu kali zaidi za kifedha kwa Korea Kaskazini iwapo taifa hilo lingefanya majaribio zaidi ya makombora.
Vyombo vya habari vya China vilisema rais wa taifa hilo alimpigia Rais Trump kutuliza hali.

Korea Kaskazini ilizindua mpango wake mpya wa ujenzi wa nyumba za makazi na biashara mjini Pyongyang.

Ulionekana kuwa mpango wa kawaida tu, lakini ilikuwa pia fursa ya taifa hilo kuonyesha nguvu zake.
Waandishi wa habari wa mashirika ya kigeni walialikwa kushuhudia wanajeshi wakifanya gwaride na kutembea kwenye barabara za mji huo.

Donald Trump hakufurahishwa na hilo.

Aliandika tena kwente Twitter kwamba Marekani iko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini.
China ilitahadharisha kwamba mzozo mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini "unaweza kutokea wakati wowote".

Ilizionya nchi zote mbili kukoma kurushiana vitisho, na kusema hakuwezi kuwa na mshindi katika vita.

Hayo yakijiri, Korea Kaskazini ilikuwa inakamilisha maandalizi ya gwaride kubwa na maonyesho ya kijeshi Jumamosi.
Korea Kaskazini iliadhimisha miaka 105 tangu kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung.

Vifaru zilitolewa barabara za Pyongyang. Serikali ya Korea Kaskazini pia ilionyesha hadharani kwa mara ya kwanza makombora yanayoweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine, na pia makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka kwenye nyambizi.

Maafisa wa serikali ya Korea Kaskazini waliionya Marekani dhidi ya kuchukua hatua zozote, wakisema nchi hiyo iko tayari kwa vita.

Walisema watajibu kwa "mashambulio ya nyuklia".

Marekani ilidai kwamba Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora, lakini likalipuka sekunde chache baada ya kupaa angani.

Inasadikika kwamba lilikuwa kombora la masafa marefu, ambalo hupaa juu anagani kwanza na ambalo huelekezwa, lakini baadaye huanguka hadi pahali ambapo panalengwa kutokana na mvuto wa dunia.

Umoja wa Mataifa umeipiga marufuku Korea Kaskazini kufanya majaribio kama hayo.

Rais Trump atachukua hatua gani?

Ni yeye mwenyewe pekee ajuaye jibu - au labda mwenyewe binafsi amekanganyikiwa!
 
Wacha wafanye wajuavyo, naamini mmarekani akidhubutu kushambulia korea kaskazini yatampata yaleyale ya mwaka 1950/53 na ya kule vietnam miaka ya 60 na 70
 
Marekani bwana ni sawa na wale nishike nitamuuwa nishikeni nitamuuwa kaambiwa kabisa kama yuko tayari arushe hata kokoto tu Kim yuko tayari kwa yote matokeo yake Donald amekalia kumlilia mchina amkanye dogo la sivyo yeye atamshughulikia bila msaada
 
Marekani bwana ni sawa na wale nishike nitamuuwa nishikeni nitamuuwa kaambiwa kabisa kama yuko tayari arushe hata kokoto tu Kim yuko tayari kwa yote matokeo yake Donald amekalia kumlilia mchina amkanye dogo la sivyo yeye atamshughulikia bila msaada

Marekani kaogopa. kaamua kuludisha vimeli vyake,
 
Kwa huo mkwala wa marekani kugonga mwamba, vyombo vyote vya habari vya magharibi kimyaa!

Tehtehtehteh kumbe na wewe umeliona mkuu!!!

Ingelikua ndyo mkorea au murusi wameludi nyuma. Vyombo vya habar vya magharibi vingeongeza na chumvi ikolee zaidi/Wazee wa propaganda hao.pumbaf zao
 
hivi marekani mnaijua au mnaisikia tu, hapana chezea marekani wandugu, Korea watakula kichapo kibaya sana na hili hata madenge wao analijua. marekani ni wazoefu wa vita tangu karne nyingi zilizo pita kuliko Korea, anauchumi imara kuliko Korea, na anauwezo mkubwa wa kijeshi na kitechnolojia kuliko Korea. tuongee sana lakini tuweke akiba ya maneno ili siku Korea akianza kudundwa km Iraq tusijekusema marekani mkorofi. sishabikii vita...lakini tusilinganishe marekani na Korea kijeshi jamani
 
Back
Top Bottom