Julius Mtatiro: Tunaku-miss ile mbaya kwa mapambano haya yanayoendelea

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Naibu Katibu Mkuu wa CUF -- Julius mtatitiro -- uko wapi katika show hii kababambe inayoendelea baina ya wapigania haki na wkandamizaji? Tunajuwa wazi wewe ni mpiganaji -- tangu Chuoni, lakini ulikwenda chama mfu kwa sababu tu ya ahadi ya cheo na pesa.

Ulifanya miscalculations kubwa sana -- Ungekwenda CDM na kugombea ubunge Kinondoni hakika ungemwonyesha mlango wa kutokea lile gamba lisilokuwa na tija kwa taifa hili -- Idi Azzan.

Bado unaweza kufanya uamuzi mgumu. I know moyo wako uko wapi maana ktk CUF inakubidi kukaa kimya, maana kamwe hulka yako na historia yako haiko katika kutetea uchafu.
 
kama alikuwa mpiganaji huko chuoni kwenu,inatuhusu nini?na alifanya nini cha maana?
 
Julius Mtatitiro anahitajika CHADEMA, akishafika huko apewe jimbo ambalo anaweza akashinda kiulaini. Kuna nafasi ambayo anaistahili pale juu. CUF haiwezi kumpeleka popote kisiasa. Itamdhalilisha tu
 
Kwa wasiomjua Mtatiro vizuri wanaweza kukubeza na kuona kama uko kwenye ndoto za mchana. Lakini kwa tunaomfahamu hakika tunaumia sana kuona jembe kama Mtatiro likipotezwa taratibu kwenye ramani ya siasa kwa kuwekwa kwenye nafasi butu na ambayo wanaharakati wenzie hawaiamini. Sishangai sana kwani najua hii ndio tabia ya kweli ya siasa, wanasiasa wengi wanapiga kelele na wakishapewa nafasi wanakua wapole kama makondoo. Ndio maana siamini sana hawa wengine wanaojiita wanaharakati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom