Julius Mtatiro, ni ya kweli haya?

Julius Mtatiro, ni ya kweli haya?

ndupa

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Posts
4,403
Reaction score
151
willium lukuvi ametoboa siri,eti wewe ukiwakilisha chama chenu cha CUF mlitaka tume iishe ukomo wake kabla ya bunge la katiba kukaa na ukaweka signature mara mbili je hizi allegations ni za kweli??na kama ni kweli leo hii nimeamini CUF ni hawara wa CCM..
 
willium lukuvi ametoboa siri,eti wewe ukiwakilisha chama chenu cha CUF mlitaka tume iishe ukomo wake kabla ya bunge la katiba kukaa na ukaweka signature mara mbili je hizi allegations ni za kweli??na kama ni kweli leo hii nimeamini CUF ni hawara wa CCM..

Kwani hujui kama walishafunga ndoa ya mkeka kule zanzibahari
 
Hakuna ubishi Mkuu katika hili kwani CUF ni HAWARA wa CCM, sii unaona hata maalim Seif alivyotulia kwa sasa?:frusty:
 
willium lukuvi ametoboa siri,eti wewe ukiwakilisha chama chenu cha CUF mlitaka tume iishe ukomo wake kabla ya bunge la katiba kukaa na ukaweka signature mara mbili je hizi allegations ni za kweli??na kama ni kweli leo hii nimeamini CUF ni hawara wa CCM..

Wewe una muuliza. Nabado hajajibu una hukumu?alaf matumizi ya maneno unayajua? Si kila neno ni la kuandika.
 
Unamuuliza afanye nini sasa kikubwa mswaada umepita sasa tutengeneze katiba mpya kwisha habari.
 
willium lukuvi ametoboa siri,eti wewe ukiwakilisha chama chenu cha CUF mlitaka tume iishe ukomo wake kabla ya bunge la katiba kukaa na ukaweka signature mara mbili je hizi allegations ni za kweli??na kama ni kweli leo hii nimeamini CUF ni hawara wa CCM..

Mtatiro ukimaliza kujibu hilo, Waambie wanachama wa CUF kwanini baada ya kipigo cha wafuasi wa CUF walichokipata Mtwara, mlisema mtaishitaki serikali kwa kitendo hicho, lakini siku mbili baadaye Mwenyekiti wa Chama chenu alienda Ikulu akaongea na Rais na sasa waliopigwa hawasikiki tena. Je mliisamehe serikali ya CCM kwa ukatili uliofanywa dhidi ya wafuasi wenu kwanini?.
 
Baba V; Hata mid ni mgeni mtaani hapa, ngoja niende zangu!
 
Last edited by a moderator:
mhuuuuuuuuuuuuuu... mashaka mkubwa haya !!!!!!!
 
mtatiro alishapewa pesa za kuibomoa cuf na cha kwanza kwa kudhihirishia wafadhili wake ccm ni kumuengeua hamad chaman kuonyesha kua yeye ana nguvu ndani ya cuf ili aweze pata ruzuku kubwa zaidi!!! kwa kifupi cuf hakuna chama tena.... kwa msiomjua mtatiro toka enzi za chaguz za daruso pale mlimani alikua ni double agent akiona flan ndo atashinda mwishon ndo anahamia kwake baada ya kuzunguka kwa wagombea wote...........

zitto ndo amechukua kozi ya usaliti kwa huyu bwana!!!
 
Nataka kujua kama Mnyaa , Lipumba na Seifu wanalifahamu hili ?
 
Mtatiro ukimaliza kujibu hilo, Waambie wanachama wa CUF kwanini baada ya kipigo cha wafuasi wa CUF walichokipata Mtwara, mlisema mtaishitaki serikali kwa kitendo hicho, lakini siku mbili baadaye Mwenyekiti wa Chama chenu alienda Ikulu akaongea na Rais na sasa waliopigwa hawasikiki tena. Je mliisamehe serikali ya CCM kwa ukatili uliofanywa dhidi ya wafuasi wenu kwanini?.

Wakati mwingine tunaweza kumuhukumu Mtatiro bure, kwani alikwenda kama Mtatiro au alikiwakilisha chama?
 
willium lukuvi ametoboa siri,eti wewe ukiwakilisha chama chenu cha CUF mlitaka tume iishe ukomo wake kabla ya bunge la katiba kukaa na ukaweka signature mara mbili je hizi allegations ni za kweli??na kama ni kweli leo hii nimeamini CUF ni hawara wa CCM..

Watanganyika si wakweli inawezekana Mtatiro amerubuniwa kweli kuisaliti CUF kwani Mapalala si alikuja na design kama kama hizi kumbe anaishabikia CCM., Tanganyika bado CUF haijapata mshirika wowote ni wanafiki tu
 
majibu ya julius mtatiro aliyoyaandika kwenye mtandao wa kijamii facebook.....
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;
09 Novemba 2013.
SHUTUMA ZA WAZIRI LUKUVI KWA CUF NI
ZA KIPUUZI NA HAZINA MSHIKO;
Nikiwa hapa Johannesburg nikihudhuria
mafunzo maalum ya usimamizi wa
uchaguzi, nimejulishwa kwamba huko
nyumbani Tanzania(bungeni), waziri wa
sera, bunge na uratibu mhe. Lukuvi
ameishutumu CUF kuwa ndiyo ilipendekeza
tume ya warioba ivunjwe mara baada ya
kukabidhi andiko la katiba kwa bunge la
katiba. Kulingana na umuhimu wangu
katika mchakato huu nikikiwakilisha chama
changu mara kadhaa, nimeona nijitokeze
kueleza ukweli uliopo katika jambo husika,
hivyo Naomba kutoa ufafanuzi kama
ifuatavyo;
1. Awali, maoni ya namna hiyo yalitolewa
na chama chetu mbele ya rais mwaka 2011
ambapo viongozi wa chama chetu
wakiongozwa na makamu mwenyekiti taifa
na mie mwenyewe nikiwepo, walikutana
na rais Ikulu jijini DSM mwishoni mwa
mwaka 2011.
Mantiki ya maoni ya chama chetu wakati
huo ilikuwa kwamba, nini itakuwa kazi ya
tume ikishawasilisha andiko lake kwa
bunge la katiba ? Serikali haikuwa na
majibu, maoni yetu yakawa kwamba tume
imalize muda wake kuliko kuendelea
kulipwa mabilioni ikiwa serikali inajua
hakutakuwa na kazi.
Maoni haya yalikuwa na lengo hasa la
kuhakikisha tunapata katiba mpya lakini pia
matumizi ya fedha yasiyo ya msingi
tunaachana nayo.
2. Tokea tulitoa maoni ya namna hiyo,
hatukuwahi kukosolewa na chama
chochote, taasisi yoyote au vyombo vya
habari. Ikumbukwe maoni tuliyoa ikulu
hayakuwa siri, tuliyasema wazi ba tuligawa
nakala kwa vyombo vya habari.
Baadaye mwaka 2012 mwezi wa Septemba,
serikali ilipokuwa inahitaji maoni juu ya
sheria ya mabadiliko ya katiba, wanasheria
wa chama chetu walihakiki maoni
tuliyoyatoa ikulu mwaka 2011 na bado
wakaona maoni ya ukomo wa tume ya
katiba yalikuwa na mashiko. Waraka huu
wa maoni uliopelekwa mara ya pili
ulipokamilishwa na hatua zote za chama
niliusaini mimi mwezi Septemba 2013.
Na mwezi wa tatu mwaka 2013 serikali
ilipoomba maoni(mimi sikuwepo ofisini
wakati huo), mwanasheria wa chama chetu
Twaha taslima aliwasiliana na mwanasheria
wetu wa Zanzibar na wakapitia maoni ya
Desemba 2011 na yale ya Septemba 2012
na kufanya mabadiliko kadhaa, suala ukomo
wa tume likabakia kuwa maoni yetu na
mhe. Taslima alisaini waraka kwenda
serikalini kuhusu jambo hili.
Wakati tumetoa maoni haya mara zote
hatukuwahi kupingwa na mtu hata
yalipoandikwa na vyombo vya habari.
3. Mjadala wa tume ikome au iendelee,
tutakubaliana ulianza kwa nguvu katikati ya
mwaka huu 2013 kabla ya bunge lililoenda
kupitisha muswada mbovu. Katikati ya
mwaka huu ndipo chama chetu kilijiridhisha
kuw mchakato wa katiba unatekwa na
vigogowa CCM na kwamba tume ikivunjwa
patakuwa na madhara makubwa sana.
Mwisho wa Mwezi mei 2013, chama chetu
kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari
kikiwashutumu watu wanaoiponda tume ya
katiba na kutaka iachwe ifanye kazi zake
kwa uhuru, ni wakati huo pia ndipo chama
kilieleza waziwazi kuwa tume ina umuhimu
wa kubaki ili kusimamia na kuwa sehemu
ya mchakato uliobakia ili kuondoa kabisa
uwezekano wa vigogo wachache kuuhodhi
mchakato huu.
4. Baadaye katika bunge la lilipotisha
marekebisho miezi michache iliyopita,
vyama vya CUF,CHADEMA na NCCR
vilishirikiana na kupinga masuala kadhaa
likiwemo hili la tume kuvunjwa.kama
chama chetu kibgetaka ivunjwe hata sasa
kingesema, lakini hivi sasa tumeona
umuhimu wa tume kuwepo na tumesema
hivyo na kupigania hivyo, siyo dhambi hata
kidogo.
Nani anataka chama chetu kiwe na mawazo
yaleyale kila wakati na kujifunga na ukake
katika jambo ambalo tumlipima na kuona
madhara yake?
Msimamo wetu wa kutaka tume ibakie
umekuwepo tokea mwezi Mei mwaka huu
na ni kabla ya ushirikiano wa bungeni na
tulipokaa na wabunge wetu kabla ya bunge
lile waliekezwa kwenda kupigania tume
iendelee kuwepo, na ndiyo maana ilikuwa
rahisi kushirikiana na CHADEMA na NCCR
kwa sababu tayari pana masuala mengi
tulijikuta tuna mtizamo unaofanana.
5. Maneno haya aliyosema Lukuvi jana
bungeni alianza kuyasema siku wakuu wa
vyama sita vyenye wabunge walipokuwa
Ikulu kuonana na rais. Wakati rais
anafafanua hoja ya uwepo au ukomo wa
tume ya katiba ambapo alianza kueleza
umuhimu wa tume kuendelea kuwepo,
Lukuvi aliingilia kutaka kumtoa rais kwenye
hoja yake, Lukuvi akajenga hoja kuwa CUF
ndo walipendekeza tume ivunjwe. Rais
alimkataza Lukuvi na akamwambia kuwa
hayo yalikuwa maoni ya chama na
yalishapita, kwa sasa tuangalie hoja zilizoko
mezani na hasa hoja ya vyama vyote kuwa
tume iendelee kuwepo.
Lukuvi aliendelea kujenga hoja kuwa hata
kipengele "hatari" cha kupitisha vipengele
vya katiba kwa kutumia wingi mdogo
(simple majority) ulipendekezwa na
CHADEMA kupitia kwa Halima Mdee
ambaye alipigania utaratibu huo na kamati
ya bunge ikaukubali na kuupitisha.
Lukuvi alipokaa kitako na nyaraka zake mie
nikapewa nafasi na nikaeleza kikao msingi
wa maoni yale na nikasisitiza kuwa
"yalishapitwa na wakati" na nikaeleza kwa
nini hivi sasa tunataka tume iendelee
kuwepo na nikatoa sababu tunazosimamia.
Mimi na Mnyika tuliongoza mazungumzo
ya kamati ya vyama na ile ya serikali
ambapo upande wa serikali waliongozwa na
Lukuvi na kuna masuala ambayo
tulikubaliana na kuna yale ambayo
hatukukubaliana. Kwa mfano hili la ukomo
wa tume sisi tumepigania tume iendelee
lakini kamati ya serikali ikakataa kata kata,
sasa kama wanasema wanataka ivunjwe
kwa sababu CUF ilishauri, je mbona CUF
inaposema isivunjwe wao wanakomalia
kuivunja? Huu ni uchuro.
5. Watu wanataka kuleta hoja hii iliyopitwa
na wakati leo hii. Ikiwa tunahukumiana
kwa maazo tuliyowahi kutoa, mbona
serikali kila kukicha inakuja na mawazo
mapya kupinga mawazo ya zamani? Mbona
kila mara wanakuja na sheria mpya
kuondoa na kupinga za zamani?
Na kama tunahukumiana, mbona
CHADEMA wameoigania mfumo wa serikali
za MAJIMBO tangu wamekuwa chama cha
siasa, lakini hivi sasa wameona mfumo huo
sio muhimu na wanasimamia mfumo wa
serikali tatu. Je ni nani anayetaka vyama
vya siasa na viongozi wake, wajifunge
kwenye ukale na wasifikiri kwa mujibu wa
wakati uliopo?
6. Hoja hii ya Lukuvi inaweza kuwa na
lengo la kuupotosha umma na kuwagawa
watanzania na hasa kugawa "spirit" ya
vyama vya upinzani na wananchi kwa
ujumla, kuwa CUF ilikuwa na lengo la
kuhujumu mchakato wa katiba, jambo
ambalo ni upuuzi usiopaswa kufikiriwa.
CUF imekuwa ni chama pekee
kilichopigania mabadiliko ya katiba ya nchi
hii kwa kuungana na vyama, taasisi na
wafau wote bila kusita, tangu chama
kilipoanzishwa, na tutasimama imara
kuendeleza mapambano hayo bila
kuangalia nyuma.
Suala la hoja fulani kuwahi kupendekezwa
namna fulani na chama fulani wakati fulani
na kwamba hivi sasa chama husika
kinashikilia hoja nyingine ni jambo
endelevu na si jipya(mawazo ya vyama
vyote duniani) hubadilika kulingana na
mahitaji ya wakati husika.
Kwa sasa mawazo na maoni ya CUF juu ya
uwepo wa tume ya katiba yako wazi sana.
TUNATA TUME IENDELEE KUWEPO na
tumependekeza juzi katika majadiliano na
serikali kuwa WAJUMBE WA TUME WOTE
AU BAADHI YAO KWA KADRI
ITAKAVYOONEKANA INAFAA wawe sehemu
ya wajumbe wa bunge la katiba.
Ikiwa LUKUVI ati anatuhukumu kwa maoni
ya kale atakuwa ni waziri na kiongozi wa
serikali mwenye maono, busara na uwezo
wa kufikiri mdogo sana. Asitumie mwanya
huu ambao uko wazi kujaribu
kuichonganisha CUF na watanzania ambao
wanategemea sana mchango wa CUF katika
ustawi wa demokrasia ya kweli na
maendeleo ya nchi yetu.
Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF Tanzania Bara,
(Safarini JOHANNESBURG-Afrika ya Kusini),
09 Novemba 2013.
 
Back
Top Bottom