Julai mosi upinzani unafikisha miaka 24, wanaamini rais bora kutoka CCM

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
kufikia julai mosi 2016, mfumo wa vyama vingi na vyama vya upinzani nchini mwetu vitafikisha miaka 24 kamili tangu uanzishwe mfumo huu tulio nao leo wa vyama vingi mwaka 1992.

Lakini hadi leo hii vyama vya upinzani nchini vinakabiliwa na kasumba kama sio jipu la kutojiamini rais bora hawezi kutoka miongoni mwao zaidi ya kuamini rais bora lazima atoke ccm.

Vyama hivyo vipo tayari kuvurugana na kupoteza mashujaa wao waliovisaidia na kuvilea sababu tu ya kuchukua kapi au makapi kutoka ccm kama tulivyoona katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015.

Kwa akili ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani hawajiamini kana kwamba wanaweza kuwa viongozi mahiri wa nchi hii, ni kwa namna gani wananchi twaweza kuwaamini wasiojiamini?

Kwa miaka yote hii 24 bado hawajiamini kuwa wanaweza kuaminiwa na wananchi kwa kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii.

Ni aibu kwa miaka 24 wapinzani wamebaki wakivizia na kudaka makapi yanayotupwa nje na ccm wakati wa kinyang'anyiro cha uchaguzi kama tulivyoona mwaka wa jana wakati wa uchaguzi mkuu.

Nina uhakika kwa ombwe hili la vyam vya upinzani nchini la kutojïamini, inaonekana itawachukua miaka 24 mingine Viongozi wengine watakaokuwa uthubutu wa kubadili gia angani na kusema no makapi kutoka ccm na watajisimamia wenyewe bila makapi ambayo huwa mamluki ndani vyama hivyo.

Kwa wenye kumbukuku wanakumbuka kuwa kwa mara ya kwanza ccm ilitikiswa na kapi Agustino Mrema alifikia hatua ya kusukumwa ndani ya gari kutoka jangwani mpaka ktk ofisi za nccr mageuzi pale manzese agentina kwa wakati huo.

Tumeona pia katika uchaguzi mkuu wa 2016 jinsi kapi lingine lilivyoitikisa ccm hadi baadhi yatu kudeki barabara ili kapi lipite wakati leo wanapinga usafi wa kila jmos ya mwisho wa mwezi.

Tutarajie kapi lingine kutoka ccm kuaminiwa tena na vyama vyama upinza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2035 kuja kuitikisa tena ccm mtikisiko ambao huifanya ccm kuwa imara zaidi na kuviboboa vyama hivyo vya upinzani.

Ifikie hatua wapinzani watuonyeshe uwezo wao na thamani yao kwa wananchi kwa kuacha na makapi na kujiamini kwa kusimamisha wagombea wasio makapi na wajiamini ili nasi tuwaamini.
 
Back
Top Bottom