JUKATA: Mchakato wa Katiba Mpya uanze sasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Jukwaa la Katiba (Jukata) limeitaka Serikali kutangaza kwenye gazeti la Serikali tarehe ya kuanza upya kwa mchakato wa Katiba mpya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Jukata, Deus Kibamba amewaeleza waandishi wa habari leo kuwa Serikali pia inatakiwa ipeleke bungeni miswada miwili ili kuhuisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 pamoja na Sheria ya Kura za Maoni 2013.

Chanzo:Mwananchi online

Binafsi naongeza na harakati za kuondoa kinga ya Raisi zianze sasa.Kauli ya Jenerali Ulimwengu iwe ni chachu ya kuanzisha harakati hizi vinginevyo maraisi watakuwa wanaharibu na mwisho wa siku wataishia kuomba radhi na mambo yanakuwa yamekwisha na wengine hata radhi wanaweza wasiombe.

Kama Raisi ana kinga na halazimika kupokea ushauri wa mtu yeyote, mnatarajia makosa haya yataisha?Mtu akijuta au kutuomba radhi,sisi kama Taifa inatusaidia nini?Watanzania tubadilike tuige kutoka kwa wenzetu ambao hata Raisi wa nchi anashitakiwa.
 
Wacha raisi aweke akili kwenye masuala ya msingi zaidi ya katiba.
 
Tatizo wengi wetu hatuelewi ile dhana ya BINADAMU WOTE NI SAWA, wenzetu wa-Israel wanaiheshimu sana hiyo dhana. Hapa kwetu mtu akiwa Rais kila kitu anachofanya ni sawa na hakuna wa kuhoji!! Tumeweka mahakama kwa ajili ya nani sasa?? Tukiweka mfumo mzuri kila mmoja wetu atafaidika kwa namna moja au nyingine...ndo maana unaona wabunge wanalalamika kukatwakodi kwenye mafao...katiba iseme wazi kila mtu mwenye umri kuanzia miaka 18 mwenye kipato halali LAZIMA alipe kodi bila kujali cheo chake.
 
Labda wangeshauri kwanza mchakato ulioanza ukamilishwe kwa kura ya maoni. Wananchi wapige kura ya Hapana ndipo likaribishwe wazo la kuanza upya mchakato. Logically (ingawa sio lazima) huwezi kuanzisha mchakato mpya bila kuufikisha mwisho kwanza mchakato uliokwishaanzishwa hata kama kulikuwa na mapungufu mengi ambayo hata hivyo yana msingi wa kisheria.
 
Tatizo ni kushikiwa akili na viongozi. Zidumu fikra za mwenyekiti
 
Mpaka Tanzania ya viwanda aliyoiahidi ipatikane ndo aanze viporo vya JK maanake ataongezewa miaka mitano kwa kutimiza ahadi zake siyo za JK.
 
Labda wangeshauri kwanza mchakato ulioanza ukamilishwe kwa kura ya maoni. Wananchi wapige kura ya Hapana ndipo likaribishwe wazo la kuanza upya mchakato. Logically (ingawa sio lazima) huwezi kuanzisha mchakato mpya bila kuufikisha mwisho kwanza mchakato uliokwishaanzishwa hata kama kulikuwa na mapungufu mengi ambayo hata hivyo yana msingi wa kisheria.

Kama waliweza kuiba kura watashindwaje kuiba hizo za katiba?
 
Watanzania hatutapata katiba tunayoitaka kwasababu ya uzalendo finyu wa wabunge hasa wa ccm. Sehemu zote zinazowabana watazibadilisha kama ile katiba ya Sitta.
Kwahiyo tuendelee hivihivi hadi pale upinzani watakapopata akidi ya kuweza kuuteka huu mchakato.
 
Mchakato uanze mpya au ule wa zamani uendelezwe ulipoishia? Kurudia mchakato upya ni kupoteza pesa, we can't afford to loose such amount again. Bora hiyo pesa tuwekewe bunge live
 
Kikwete era priorities are over ndugu. JPM has a complete different policy priority. Not time for copycat again. its over. it didn't work sorry.
 
Labda wangeshauri kwanza mchakato ulioanza ukamilishwe kwa kura ya maoni. Wananchi wapige kura ya Hapana ndipo likaribishwe wazo la kuanza upya mchakato. Logically (ingawa sio lazima) huwezi kuanzisha mchakato mpya bila kuufikisha mwisho kwanza mchakato uliokwishaanzishwa hata kama kulikuwa na mapungufu mengi ambayo hata hivyo yana msingi wa kisheria.
hamna kukubali katiba ya chenge
 
Back
Top Bottom