JPM upo sahihi,ila angalia haya ili twende vizuri

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,815
Uamuzi wa kuwakataza vijana kucheza pool table asuuhi na kuacha kuzurura ovyo badala yake wakafanye kazi ni uamuzi sahihi ila kuna mambo mkuu wa kaya anatakiwa kuyaangalia. Nitayataja kwa ufupi;
1.Somo la ujasiriamali lifundishwe kuanzia shule ya msingi,liwe na walimu wanaotambulika na waajiriwe na serikali kama walimu wengine.

2.Bei za mazao zipandishwe na masoko yapanuliwe yawe ya uhakika muda wote wa mwaka na yawe haadi vijijni ili kuepusha mrundikano wa watu mijini.

3.Kuwa na utaratibu wa kuwakopesha vijana hasa wale wasio na kazi wala mali kwa ajili ya dhamana

4.Kwa wakulima wapelekewe vifaa vya kisasa na pembejeo za uhakika,kuwa makini na wapigaji ili mahitaji hayo yaweze kufiika kwa wahusika.

5.Punguza tozo za ajabu ajabu kwa wazawa ili wale vijana wenye nia ya kuchukua biashara nje ya nchi wafanye hivyo

6.Tengeneza miundombinu rafiki utakaowawezesha vijana hawa kuasafirisha mazao yao popote na kwa wakati muafaka.

7.Vijana wanaofanya kazi kwenye kampuni za usafirishaji kama mabasi,malori n.k wasaidie waajiriwe rasmi na usisahau kuchukua kodi

8.Kuza hadhi ya kilimo,zalisha wataalam wengi na hakikisha utaalam wao unatumika,mabwana shamba wakae mashambani sio mijini kama ilivyo sasa

9.Boresha huduma za kijamii kama afya,elimu n.k ili kuhakikisha vijana hawa wanakuwa na afya njema ili waweze kufanya kazi vyema.

10.Kumbuka kuwashirikisha wadau katika mikakati yako bila kujali uwanachama wao,maendeleo ya Taifa hili yanahitaji muunganiko wa pamoja na sio ya kichama .

Nilikuwa na hayo mzee,nakutakia kila la heri katika kutekeleza majukum yako.

Mungu akubariki sana.
 
Hiyo namba
8 umenikumbusha 2008 nikiwa Halmashauri ya wilaya ya kilindi kulikuwa Na bwana samaki ili hali hakukuwa hata bwawa!
 
Back
Top Bottom