MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,296
Ni furaha kubwa sana na inatia matumaini kusikia Mhe JPM mara kwa mara akisisitiza "msemakweli ni mpenzi wa Mungu" na pia kuibainisha kama mtu anazingatia sheria katika utendaji badala ya kuedekeza siasa (anayaita mavyama, japokuwa ni mavyma hayo hayo ndio yalimwezesha kuukwaa urais). Hadi hapo ninamwelewa na kumuunga mkono.
Lakini mara kwa mara hawaambii wananchi ukweli na hapa ninaomba nijikite tu kwenye suala la wahisani husasan MCC ambayo inaelekea imemuumiza sana na anaitumia kuwaaminisha wananchi kuwa Marekani ni taifa baya kwa sababu linataka kutupa misaada kwa masharti na vitisho, na nchi kama Japani na China ni watu wanaotupenda sana kwa sababu wanatupa misaada/mikopo bila masharti! Angekuwa antenda anayoyahubiri (yaani kusema kweli ili uwe mpenzi wa Mungu), JPM angewaeleza wananchi kuwa Marekani imekuwa ikitoa misaada ya aina mbalimbali kuanzia enzi za Hayati JFK (kumbuka unga wa yanga). MCC ulikuwa ni mmojawapo ya aina za misaada ambao ulikuwa na masharti ambayo sisi Tanzania tuliweka sahihi kukubaliana nayo. Kama ilivyo kwa mkataba wo wote ule, usipotimiza masharti basi kile ulichokuwa unapata kinayeyeyuka. Kwa bahati mbaya - kwa kujua au kutojua - hatukutimiza masharti (na hiyo ndio sheria) na hivyo wahusika wamesimamisha huo msaada. Tutaangalia ni wapi tulijikwaa!
Angechukua mweleko huu badala ya kuwalisha wananchi sumu kuwa hawa ni watu wabaya vs. hawa ni wazuri, mara tuko tayari kula mihogo badala ya mkate wenye masimango, nk, nk, (vijembe vingi tu sijui Msukuma ameanza lini kuwa mtaalamu wa vijembe kama Mkwere), ningekubali kuwa ni 'msema kweli na hivyo ni mpenzi wa Mungu' na ni mtu asiyependa kupindisha sheria!