JPM geukia na huku Kigamboni New City Project

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
34,153
41,525
Wakuu,

Sisi Wananchi wa Kigamboni tuonaona hatma ya Kigamboni New City kwa sasa ipo mikononi kwa Rais mwenyewe, Sisi wakazi wa mji huu kwa kweli tumekuwa wavumilivu vya kutosha na sasa tunakaribia kufika tamati.

Mwaka 2008 tulipata zuio toka Serikali Kuu kuhusu kutoendeleza chochote ndani ya eneo hili kwa muda wa miaka 2, kwa sababu ya hii Project- tukavumia.

Mwaka 2010 tukapata zuio jingine tena la kutoendeleza chochote kile ndani ya eneo hili kwa miaka mingine 2, sababu ya hii Project - tukavumila.

Mwaka 2012 mazuio yaa kisheria yakawa yameisha na watu ikabidi tuanze kuendeleza makazi yatu ki mbinde mbide hivyo hivyo bila michoro wala chochote, kila mtu anafanya lake sababu hatukuruhusiwa kufanya chochote kile kilichoruhusiwa ndani ya eneo la Project. hatukuweza kupima, kupata kibali cha ujenzi nk hadi hivi leo. Familia zinapanuka, watoto wanakua hapa ndipo hatma yetu inavyozidi kuwa ngumu mno.

Baada ya purukushani nyingi sana kati ya wananchi na viongozi wa mradi huu ambazo zitaki kuzitaja maana hata ninyi mnazijua, hatimaye Bunge likapitisha KDA (Kigamboni Development Agency) kama ilivyo CDA kule Dodoma, lakini tangu KDA ianzishwe ndugu zangu karibu miaka 2 sasa hakuna lolote lililofanyika, narudia tena hakuna chochote kilichofanyika kwenye mji huu mpya kilichopo ni alama tu za vi-nguzo kando kando mwa barabara kuashiria itapita wapi na kwa upana gani, lakini cha ajabu si barabara zote walizoweka alama, sasa hatujui hawa jamaa wanafanya kazi gani wakifika ofisini kila siku kwa miaka hiyo zaidi ya 2.

Hatima yetu ni ipi?

Sisi wakazi tuna haki zetu kama wengine, tuna familia pia tunataka kuendeleza makazi yetu, tunataka pia tupate hati za makazi ili hata kupata mikopo nk

Juzi juzi nimemsikia mbunge wetu wa Kigambaoni akiomba Bunge litengue KDA na kurudisha Project hii kwa Halmashauri mpya ya Kigamboni, sisi wananchi tunaungana na Mbunge wetu maana Serikali kuu kupitia KDA imeshashindwa kuendesha mradi huu.

Sisi wakazi wa Kigamboni tunaona nafasi ya mwisho kabisa tuliyonayo ni kulifikisha suala hili kwa rais JPM ili lipate suruhisho la mwisho. tumeteseka sana, tunaishi kama digi digi ndani ya Tanzania kwa nini!! sasa hivi makazi karibia 95% hayana documents za kisheria za ujenzi hii ni hatari sana, kila mtu anajenga anavyoona inafaa kwake yeye ili akidhi mahitaji ya familia yake.

Rais JPM, tunaomba kama unavyozigeukia project nyingine, hebu itisha file la Kigambani New City ofisini kwako ulipitie, utaona maajabu ambayo hujawahi kuyaona. Project gani inachukua miaka 9 bila hata tofali kuwekwa? bila hata nondo moja kuwekwa?, wakati project inaanza hadi leo kijana aliyezaliwa sasa yupo darasa la Tatu, je kijana huyu atalala wapi wakati mmetuzuia kuendeleza makazi kisheria?

Tuliambiwa Phase 1, itakuwa ni ujenzi wa miundombinu, yaani Barabara, Maji, Gesi, Umeme nk, hii pia itakuwa ni kulipa fidia stahiki kwa wenye maeneo ambayo miundombinu hii itapita lakini tangu tathmini hiyo ifanyike sasa mwaka wa nne kama sikosei, sasa unamlipaje mwananchi huyu kwa tathmini ya miaka minne iliyopita.

Hitimisho.

JPM tunaomba uitishe file la project hii ofisini kwako maana tunaona ni wewe sasa mwenye hatma ya Project hii.

Tunakuomba saana tena saana, maana hatma ya mradi huu unayo wewe mikononi mwako!! Kama ni kuurudisha mradi huu mikononi kwa Halmashauri yetu mpya pia litakuwa jambo jema sana.

Tumebakia kuangalia video huku tukiishi kwa matumaini.

TAZAMA VIDEO YA MJI MPYA 'THE KIGAMBONI NEW CITY' [ OFFICIAL ] - TABIANCHI
 
Back
Top Bottom