JONAS SAVIMBI ATAKUMBUKWA KWA MENGI

JONAS SAVIMBI ATAKUMBUKWA KWA MENGI

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
Jonas Savimbi, mtoto wa ‘mtumishi’ aliyeingia msituni
Kwa ufupi
Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye alijiunga na chama cha FNLA.

Risasi 15 zilizoingia katika maeneo tofauti ya mwili wa Jonas Malheiro Savimbi ziliukatiza uhai wake, baada ya miaka 27 ya mapambano ya msituni dhidi ya Serikali ya Angola.

Katika mapambano hayo ya mwisho, Savimbi ambaye alipambana hadi pumzi yake ya mwisho, pale roho ilipouacha mwili, aliingia katika historia ya taifa hilo na ya dunia, kutokana na namna alivyoshiriki katika vita baridi, akichukuliwa kama ngome muhimu kwa nchi za dunia ya tatu, hasa za Afrika.

Risasi hizo zilimaliza mapambano ya Savimbi aliyezaliwa Agosti 3, 1934 huko Munhango akiwa mtoto wa Lotte, mfanyakazi, Mkuu wa Stesheni wa Shirika la Reli la Angola na mhubiri katika Kanisa la Kiprotestanti la Angola lililoanzishwa na wamisionari wa Marekani.

Jonas Savimbi alikuwa ni kiongozi wa vita vya msituni Angola. Savimbi alifariki Februari 22, 2002.

Alisoma katika shule za Kiprotestanti na Kikatoliki, lakini akiwa na miaka 24 alipata udhamini wa kwenda kusoma Ureno ambapo alimalizia masomo yake ya sekondari na somo la lazima la siasa huku akishindwa kuanza kwa wakati masomo ya udaktari wa binadamu aliyotakiwa kuyachukua.

Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la Unita kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.

Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye alijiunga na chama cha FNLA.

Mwaka huohuo alipata fursa ya kufanya ziara maalumu China na aliahidiwa kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi na misaada ya zana za kijeshi.

Hatua hiyo ilitokana na mgongano wa kimasilahi, baada ya FNLA na MPLA kuanza kupingana kuhusu nani anastahili kupewa nchi iwapo watapata uhuru, hivyo muda mfupi baadaye wakoloni hao walitoa taarifa kueleza kwamba Savimbi anapigana kwa ajili ya masilahi yao.

Hatua hiyo ilisababisha kuungwa mkono na Marekani iliyokuwa na masilahi tofauti na MPLA iliyoungwa mkono na Wasovieti tangu mwaka 1974 na kilijipambanua kufuata mrengo wa Marxist-Leninst kuanzia mwaka 1977, wakati Savimbi alijipambanua kufuata sera za Mao na kuungwa mkono na China.

Vita baina ya MPLA na Unita hata hivyo ilikuwa na sababu nyingi za ndani na kwa hiyo kuanza kutumiwa kama chanzo cha mvutano wakati wa vita baridi baina ya Marekani na USSR.

Baada ya kupata Uhuru mwaka 1975, mwaka 1985, kwa msaada wa Serikali ya Marekani chini ya Ronald Reagan, taasisi ya Jack Abramoff kwa kushirikiana na wabunge wa Conservative iliandaa kongamano kubwa la kimataifa la demokrasia katika mji wa Jamba, huko katika Jimbo la Cuando, kusini mwa Angola ilipokuwa ngome ya Savimbi na huo ukawa mwanzo mpya kwa Savimbi.

Kupitia Taasisi ya Heritage Foundation ya Marekani ambayo kiongozi wake, Michael Johns na wenzake walianza safari za kila mara katika ngome ya Savimbi, Marekani ilijikita kumpatia msaada wa kujijenga kisiasa na kijeshi dhidi ya Serikali ya Angola iliyokuwa chini ya MPLA.

Marekani ilianzisha mkakati maalumu kwa ajili ya kumpatia Savimbi silaha za kisasa na mafunzo kwa wapiganaji wa msituni ili kumpa nguvu katika vita yake dhidi ya Serikali ya Angola ambayo ilikuwa ikiunga mkono sera za Kikomunisti chini ya USSR mjini Moscow.

Baada ya kunusurika katika mashambulizi karibu 15 ya kujaribu kumuua, akiwa ameripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo, hatimaye aliuawa Februari 22, 2002 kwenye mapambano na majeshi ya Serikali.

Nnachokumbuka ni hilo jina la mji ilipokuwa ngome ya Savimbi basi
 
Maiti yake ilidhalilishwa mitaani. Baada ya kumuua walimfunga katika gari na kuanza kumburuza mitaani.
 
Mkuu, tunashukuru kwa bandiko lako ingawa taarifa kumhusu Jonas savimbi haijajitosheleza. kuna information nyingi sana kumhusu mbabe huyo (RIP) wa kivita na hazijawa included. Once again, thanks for sharing
 
Maiti yake ilidhalilishwa mitaani. Baada ya kumuua walimfunga katika gari na kuanza kumburuza mitaani.
siyo kweli. maiti yake iliachwa kama mzoga na huku inzi wakiizonga. aliyefungwa kwenye gari na kuburuzwa mtaani ni samwel doe ambaye alizungushwa katika mji wa monrovia kwa kuburutwa na gari...
 
watu wengi wa Angola wanamkumbuka kwamba alikuwa shujaa kuliko tulio nje ya Angola tulivyokuwa tunamchukulia kama katili na muuaji.
 
Back
Top Bottom