Joho la Mwendawazimu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
JOHO LA MWENDA WAZIMU.











1)ukiona hakunacho,usinyooshe kidole.
Vidole kile ambacho,vipo kwako siyo mbele.
ukisifu kwa kijicho,utalogwa kwa tembele.
Joho la mwenda wazimu usivae harusini.



2)sitiri ulichonacho, kisiteleze kambale.
Yataja pofuka macho,akusibu msukule.
Konokono wa kichocho,katu haishi milele.
Joho mwenda harusini.
3)ukidhani kikulacho,atakula yule yule.
Ila ukweli kijacho,kipo nyuma hata mbele.
Fungua moyo na macho,kwa mbali tazama kule.
Joho la mwenda wazimu,usivae shereheni.
Shairi:JOHO LA MWENDA WAZIMU.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382486.
 
Back
Top Bottom