John Pombe Magufuli hajawahi kuwa na uchungu na wanyonge wa nchi hii

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,485
18,048
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli hajawahi wala siyo mtetezi wa wanyonge na masikini wa nchi hii katika historia ya utumishi wake wa Ubunge na Uwaziri katika Wizara mbalimbali alizowahi kuhudumu kwa miaka ishirini (20) na hatimaye Urais wa Tanzania alionao sasa.

Wakati CHADEMA na Upinzani kwa ujumla wakipinga kwa nguvu zote ndani na nje ya Bunge kuhusu mikataba mibovu ya rasilimali za nchi hii Wabunge wa ccm akiwemo Rais John Pombe Magufuli walikuwa watetezi wakubwa wa mikataba mibovu na ya wizi dhidi ya rasilimali za Taifa hili, Upinzani umepinga sana mikataba hii ya kinyonyaji huku hawa ccm vibaraka wa haya makampuni makubwa ya uwekezaji wakiipitisha ndani ya bunge kwa mbwembwe nyingi na kebehe nyingi kwa wale wapinzani waliojaribu kuhoji wakati wa kupitisha mikataba hiyo, na wengine waliojaribu kuhoji wizi na ufisadi unaofanyika katika makampuni hayo walikiona cha mtema kuni kwa kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kutumia kanuni kandamizi za bunge, huku John Pombe Magufuli (Rais sasa) akiwa sehemu ya ubazazi huo.

Hakuna rekodi katika Hansard za bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania inayomuonesha Rais Magufuli akipinga maovu ya serikali waziwazi kuanzia Serikali ya awamu ya (3) hadi ya (4). Leo hii Rais Magufuli anatoa wapi nguvu ya kukemea na kupambana na mikataba mibovu na ya kinyonyaji aliyoshiriki kikamilifu kuitengeneza mwenyewe na wanaccm wenzake akiwa mbunge na Waziri?!!!! Leo hii badala ya kuwajibika kwa umma kwa makosa makubwa ya kuisababishia nchi hasara kubwa ya mabilioni ya fefha kupitia mikataba hiyo eti analalamika tunaibiwa na haya makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini!!!!! Huu ni unafiki wa mwendo kasi hata shetani hushangaa! Haya yooote hakuwahi kuyakemea ndani ya bunge na nje ya bunge kwa miaka yote ishirini (20) lakini kuna wafia maslahi ya ccm na matumbo ya familia zao wanakuja na uongo uongo kuwa Rais Magufuli ni rais wa wanyonge, huo unyonge umeanza lini kama amekaa ndani ya bunge kwa miaka 20 kutetea maovu yote ya serikali?!!!!

Ushahidi mwingine mdogo ni kuhusu safari za nchi za nje za Rais wa awamu iliyopita Rais Jakaya Kikwete kuwa zilikuwa ni nyingi mno zisizo na tija kwa maslahi mapana ya Watanzania alizitetea sana Rais Magufuli ndani na nje ya bunge kwenye mikutano yake ya hadhara kwa wananchi wakati akitimiza majukumu yake kama Waziri wa Ujenzi, huku akiwananga Wapinzani kuwa wanachuki na Kikwete sababu zile ziara zilileta tija kubwa sana kwa taifa kwa kuhemea pesa huko nje pamoja na kuleta wawekezaji wa miradi mbalimbali nchini. Lakini wakati anafungua bunge lake la kwanza baada ya kuingia madarakani kama rais wa nchi alimnanga sana Mh Kikwete japo alitumia maneno ya mafumbo kuwa kuna watu wamesafiri sana nje ya nchi kuliko kwenda kusalimia wazazi wao huko kijijini, huku akisema ziara hizo za nje zililitia hasara kubwa sana serikali, na kwa muktadha huu Rais Magufuli na wanaccm wenzake hawajawahi kuwa watetezi wa wanyonge wa taifa hili na haitakaa itokee maana kwao UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI ndio nguzo kuu inayowaweka madarakani, hivyo hawawezi kupambana kulikata tawi walilolikalia. Wanaccm na viongozi wao hawana nia njema na taifa hili wala hawajahi kuwa nayo zaidi ya kuwa wanafiki dhidi ya maendeleo ya nchi hii.
 
Umemfumua za uso, vimulimuli tu.
Duniani kuna vituko na watu wa ajabu, pamoja na kuweka sawa mambo yote hivi wapo misukule itapondea uzi huu.
Natamani tupeleke huu uzi uwe makala kwenye gazeti la UHURU
 
HAkuna mwanasiasa mwenye uchungu na nchi, woote wanaangalia masalahi yao
 
Kwa hiyo tukusaidiaje sasa, labda?
 
Duh hapo narudisha buku 7. Hakuna sehemu katika kumbukumbu za bunge au media Magufuli alipinga usafirishaji mchanga au kuongeza mrahaba kutoka 4% hadi 50%, akiwa bungeni au nje ya bunge....
 
Mimi nafikiri unafiki ni hulka ya mtu...anazaliwa nayo hio
..
Hahahaaa ebwana hili likimfikia mwenyewe anaweza hata kujiuzulu.....lakini Mungu ni mwema ona nchi inavyowayawaya kutokana na yale aliyopigia chapuo?? Ona anavyotapatapa huku na kule?? Reap what you saw!
 
Sikuona kwa nn mikataba ya gesi ilisainiwa km emergency, na bado hatukujua tunapata nn au kiasi gani na mwekezaji anapata nn. Naomba Rais afumue hii mikataba yote tuchukue angalaau40% tunachakaa na kupigika wakati tuna Mali? Asiyetaka hiyo 40 aondoke. Na waliotuingiza hasara wapigwe risasi hadharani.
 
Rais alianza vizuri na bandari sawa. Sasa ingefatia mikataba ya madini na katiba, Sasa sijui na anapatwa na ugonjwa gani tena wakati tulimwani anaubavu? Anachelewa nn?
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli hajawahi wala siyo mtetezi wa wanyonge na masikini wa nchi hii katika historia ya utumishi wake wa Ubunge na Uwaziri katika Wizara mbalimbali alizowahi kuhudumu kwa miaka ishirini (20) na hatimaye Urais wa Tanzania alionao sasa.

Wakati CHADEMA na Upinzani kwa ujumla wakipinga kwa nguvu zote ndani na nje ya Bunge kuhusu mikataba mibovu ya rasilimali za nchi hii Wabunge wa ccm akiwemo Rais John Pombe Magufuli walikuwa watetezi wakubwa wa mikataba mibovu na ya wizi dhidi ya rasilimali za Taifa hili, Upinzani umepinga sana mikataba hii ya kinyonyaji huku hawa ccm vibaraka wa haya makampuni makubwa ya uwekezaji wakiipitisha ndani ya bunge kwa mbwembwe nyingi na kebehe nyingi kwa wale wapinzani waliojaribu kuhoji wakati wa kupitisha mikataba hiyo, na wengine waliojaribu kuhoji wizi na ufisadi unaofanyika katika makampuni hayo walikiona cha mtema kuni kwa kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kutumia kanuni kandamizi za bunge, huku John Pombe Magufuli (Rais sasa) akiwa sehemu ya ubazazi huo.

Hakuna rekodi katika Hansard za bunge la Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania inayomuonesha Rais Magufuli akipinga maovu ya serikali waziwazi kuanzia Serikali ya awamu ya (3) hadi ya (4). Leo hii Rais Magufuli anatoa wapi nguvu ya kukemea na kupambana na mikataba mibovu na ya kinyonyaji aliyoshiriki kikamilifu kuitengeneza mwenyewe na wanaccm wenzake akiwa mbunge na Waziri?!!!! Leo hii badala ya kuwajibika kwa umma kwa makosa makubwa ya kuisababishia nchi hasara kubwa ya mabilioni ya fefha kupitia mikataba hiyo eti analalamika tunaibiwa na haya makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini!!!!! Huu ni unafiki wa mwendo kasi hata shetani hushangaa! Haya yooote hakuwahi kuyakemea ndani ya bunge na nje ya bunge kwa miaka yote ishirini (20) lakini kuna wafia maslahi ya ccm na matumbo ya familia zao wanakuja na uongo uongo kuwa Rais Magufuli ni rais wa wanyonge, huo unyonge umeanza lini kama amekaa ndani ya bunge kwa miaka 20 kutetea maovu yote ya serikali?!!!!

Ushahidi mwingine mdogo ni kuhusu safari za nchi za nje za Rais wa awamu iliyopita Rais Jakaya Kikwete kuwa zilikuwa ni nyingi mno zisizo na tija kwa maslahi mapana ya Watanzania alizitetea sana Rais Magufuli ndani na nje ya bunge kwenye mikutano yake ya hadhara kwa wananchi wakati akitimiza majukumu yake kama Waziri wa Ujenzi, huku akiwananga Wapinzani kuwa wanachuki na Kikwete sababu zile ziara zilileta tija kubwa sana kwa taifa kwa kuhemea pesa huko nje pamoja na kuleta wawekezaji wa miradi mbalimbali nchini. Lakini wakati anafungua bunge lake la kwanza baada ya kuingia madarakani kama rais wa nchi alimnanga sana Mh Kikwete japo alitumia maneno ya mafumbo kuwa kuna watu wamesafiri sana nje ya nchi kuliko kwenda kusalimia wazazi wao huko kijijini, huku akisema ziara hizo za nje zililitia hasara kubwa sana serikali, na kwa muktadha huu Rais Magufuli na wanaccm wenzake hawajawahi kuwa watetezi wa wanyonge wa taifa hili na haitakaa itokee maana kwao UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI ndio nguzo kuu inayowaweka madarakani, hivyo hawawezi kupambana kulikata tawi walilolikalia. Wanaccm na viongozi wao hawana nia njema na taifa hili wala hawajahi kuwa nayo zaidi ya kuwa wanafiki dhidi ya maendeleo ya nchi hii.
Pengine alikuwa anaumia ndani kwa ndani? Kuna wakati inabidi tubaki na matumaini yetu aka ujinga. Tukipoteza matumaini tutakuwa watu wa aina gani? Nchi za uarabuni tulizoamini ni stable nazo zimesambaratika.
 
Back
Top Bottom