GE2025 John Mnyika: Zuio la kufanya siasa linawahusu bodi ya wadhamini na Katibu mkuu, Wanachadema wengine endeleeni bila kutumia mali za chama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama Agosti 18, 2025 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amewataka Wanachadema wengine kuendelea kufanya siasa ilimradi tu wasitumia mali za chama kwani zuio la kutokufanya siasa ni kwa katibu Mkuu na bodi ya wadhamini.
===

"Kitu kingine ambacho kimejitokeza bayana ni kwamba zuio la kufanya shughuli za siasa linahusu bodi ya wadhamini na katibu mkuu peke yake.

Kwa maneno mengine Wanachadema mna haki ya kuendelea kufanya shughuli za siasa maeneo mbalimbali, ilimradi katika kufanya shughuli hizoza siasa msitumie mali za chama kwahiyo mkifanya wenyewe huko kwa kujichangisha huko, kushirikiana huko endeleeni kufanya shughuli za kisiasa mpaka kieleweke" -John Mnyika
Your browser is not able to display this video.
 
Sawa

Ni kama Waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima Ibada zinaendelea siyo kwenye mali za kanisa
 
Polisi sasa inategemeana watapewa maelekezo gani na viongozi wa chama kinachotawala.
 
Imekaa vizuri sana

Iundwe team mbili (1) John heche (makamu mwenyekiti)

(2) Katibu mstaafu Dr wilbroad slaa

(3) waitishe harambee

No reform no election wailete Kwa wananchi mzunguko wa pili .......tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…