John Mnyika: Mwana CHADEMA aliyekulia ndani ya chama anayefanana na Dr. Slaa!

Status
Not open for further replies.

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,593
36,012
Jina la John Mnyika leo usiku linatarajiwa kutamkwa zaidi na vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na vinywa vya watu.

Kimsingi mwana siasa huyu kindakindaki na kijana mahiri ana amini zaidi ndani ya Chadema na ameziishi siasa za Chadema katika maisha yake yote ya kisiasa hadi hii leo! Huyu ndiye mwanasiasa ambaye amemrithi baba yake kisiasa Dr. Willbrod Slaa kwa kila kitu ikiwemo msimamo mkali dhidi ya wazembe na wabadhirifu.

Kijana huyu leo anatarajiwa kusikika sana na kwa hakika anatarajiwa kubeba majukumu mazito ya chama na kuyasimamia!

Kila lakheri John Johnson Mnyika!!
 
mshaanza mambo ya kiccm kuvujisha siri za vikao!!!!!!kwa hiyo mnyika naye anakula mihogo for breakfast?ni msaliti wa chama?amelishwa limb.wata la kihaya!!!!toa ujinga hapa.
 
Katika hoja yako mimi sikubaliani na wewe jambo moja kwamba Mnyika hafanani na Slaa ana wasifu wake binafsi tena hajawahi kusimama kizimbani eti kisa mke wa mtu.
 
Jina la John Mnyika leo usiku linatarajiwa kutamkwa zaidi na vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na vinywa vya watu.

Kimsingi mwana siasa huyu kindakindaki na kijana mahiri ana amini zaidi ndani ya Chadema na ameziishi siasa za Chadema katika maisha yake yote ya kisiasa hadi hii leo! Huyu ndiye mwanasiasa ambaye amemrithi baba yake kisiasa Dr. Willbrod Slaa kwa kila kitu ikiwemo msimamo mkali dhidi ya wazembe na wabadhirifu.

Kijana huyu leo anatarajiwa kusikika sana na kwa hakika anatarajiwa kubeba majukumu mazito ya chama na kuyasimamia!

Kila lakheri John Johnson Mnyika!!
Muda utaongea
 
Mnyika hawezi kufanya kazi na Lowassa, Mbowe anajua hiyo kitu.

So, sahau hilo swala la Mnyika kupewa hiko cheo cha KM.
 
Inasikitisha sana kwa kuwa mbea,..wanaukawa hawana umbea kama wale jamaa wa lumumba....
 
Sina mashaka na hii I'd naamini itakuwa km ulivyosema masaa machache yajayo. Kila la kheri John J Mnyika.
 
Kiukweli Mnyika angefaa......lakini Mnyika hamkubali Luwassa na hapo ndipo anapopishana na Sultan Mbowe

Akiteuliwa mnyika, chadema asili itanyanyuka
 
Wakati Mh. Magufuli akivuta pumzi kuwasaka wasaidizi wake (mawaziri na manaibu), zilisikika kelele kwanini jamaa anachukuwa muda mrefu kuwatangaza. Lakini tulishasahau kuwa kuna nafasi moja nyeti kwenye Chama ambayo imechukua karibu mwaka bila ya uteuzi nasi hatukupiga kelele!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom