CDM walisema hana number, na kw aujinga kanyea kambi.Kama bado ni mamluki wa CDM basi atakuwa proof nzuri kuwa CCM ni very Vulnerable.Kama hadi Speaker wa Bunge 6 alikuwa na kadi ya CCM ,ni mbunge na speaker wa CCM, ni candidate wa urais wa CCM yet alitumikishwa na CDM .Siwezi ishangaa CCM ,kama jimama lenye kila aina ya hela jeuri, nguvu mbele ya wanaume.Halafu linachapwa makofi na kimwana mdogo kadiri apendavyo, huku linabaki lia kuwa haliachiki ng`o.Nape nadhani atahamia CDM punde lowassa akitawazwa kuanza kampeni!!
mkuu huoni hata aibu swala hili nape kaliongelea sana mpaka kwenye vyombo vya habari kweli wewe upo nyuma katika kutafuta habari.Kwa mujibu wa kada wa CCM ambaye ni mjumbe wa NEC ambaye amavujisha siri hii, inasemekana kuwa Mh Mangula alipotoa kauli ya kukataza wanaccm kujinadi kabla ya kipindi cha uchaguzi alisababisha Mh.Lowasa na wengine wengi wenye uchu na madaraka 2015 kuchukizwa na kauli hiyo na kuamua kufanya kila namna kahakikisha Mangula anadhibitiwa vema ama anafanyiwa kila namna hadi ajiunge na kambi ya Lowassa ili apunguze msuli dhidi ya harakati za mbunge huyu wa monduli.
Kwa mujibu wa kikao cha JK na wabunge kilichofanyika dodoma hivi majuzi, JK amedhihirisha kwenda kinyume na msimamo wa Mangula kwa kutoa amri kuwa wanaccm wanaotaka kuwania nafasi za urais na ubunge kupitia ccm ni ruksa kuanza kujipitisha kwa wapiga kura.
Kauli hii tata ya Mwenyekiti wa ccm mrisho jakaya kikwete imeshangaza wengi hasa baada ya kudhihirisha kuwa ni kauli inayopingana na maazimio ya awali yaliyopitishwa na kikao cha Nec yaliyotangazwa na Mangula ambaye ni m-nec wa ccm.
Viunga vya ccm vya ndani kabisa vinapasha kuwa baada ya JK kuonyesha wazi kuwa anasupport harakati za kujinadi zinazofanywa na Lowasa pamoja na wanasiasa wengi wa ccm kumesababisha mpasuko wa hatari ndani ya ccm ambapo mwisho wa siku tutajionea jinsi Mh. Mangula pia anajisalimisha kwa Lowassa mithili ya mbwa koko aliyekutana na chatu na wengine watasambaratika kila mmoja kivake bila kujitambua.
Huu unaitwa ni mpasuko ndani ya ccm kwasababu makada maarufu wameshaanza kutupiana maneno makali hasa baada ya wengine kugundua kuwa wanatumiwa vibaya na JK mithili ya mbuzi wa kafara.
Nape Nnauye ni Kada mashuhuri wa ccm ambaye ameonekana dhahiri kutetereka na mwenye hofu kubwa hasa baada ya kumuona JK akimsifia Lowasa hadharani na akimpa ruhusa ya kujinadi kwa wapiga kura kwa ajili ya urais 2015.
Wachambuzi wa maswala ya siasa wanakiri kuwa JK ameanza kudhihirisha kuwa anamsanifu Membe na na nia yake kuu ni kumrithisha Lowasa kiti cha kugombea urais 2015 kupitia CCM.
Makambi yote ya ccm yaliyokua yakiwania nafasi ya uwakilishi wa rais yameanza kuyumba gafla baada ya kutatanishwa na msimamo wa nwenyekiti wa CCM Mh.Mrisho Jakaya Kikwete juu ya nafasi ya urais 2015,
' wengi walidhani kuwa JK amemsaliti Lowasa na kuunga mkono kambi ya Membe kumbe la hasha bado JK anamuandalia makao Lowassa'. Hayo ni maneno ya kiongozi wa Nec aliyekuwa akichekelea mtafaruku huu mkubwa unaodhihirisha kuwa JK kama mwenyekiti wa ccm amepanic kutokana na speed ya CHADEMA hadi amejikuta akitoa maagizo yanayopishana wazi kabisa na maazimio ya NEC ya ccm yaliwekwa hadharani hapo awali na Mangula.
My take.
Wale makada waccm wanautumika kama big.G huu ndo muda wao maalum wa kutemwa rasmi na JK pamoja na viongozi wengine wa ccm wenye uchu wa madaraka.
Sakata hili pia linadhihirisha kuwa JK amewaingiza mkenge puppets wengi sana wa ccm.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
CDM (The badger) haoni hata haja ya kujali nani anachaguliwa ktk hii kambi dhaifu na tamu kutafuna.Kwani siku anataka lunch hahitaji kujua kama ni black mamba, green mamba, cobra, au nani, yeye atavuta kunzi apopote kama anayevuta spagheti vile..Si Lowassa huyu huyu alikwend ameru kwa mbwembwe kuwa yeye ni wa vitendo.Baada ya kuwagaragaza CCM ktk uteuzi wa Sioyi. Alichoambulia ni kuingia kimaficho ktk chumba cha kuhesabu kura ili akabadili matokeo, magari yalipasuliwa na mwisho sioi akakubali matokeo.SIjui kama hiyo habari hata kama iliwahi somwa tena.CCM hata revision hawataki sikia.
Ukiacha Mdhaliliko alioupata kwenye RICHIMOND , Kusema ule ukweli mahali pengine alipodhalilika Lowasa ni Arumeru , usifanye Mchezo na CDM aisee , hao jamaa hawajali Mvi za Mtu ! Ukiwakalia kwenye 18 lazima wakubutue !
Mgawanyiko bado, mgawanyiko utaonekana dhahiri kwenye bunge la bajeti la mwaka 2015. Mambo bado, na kutakuwa na kambi tatu tu. Na nawakumbusha tu kuwa hela zitamwagwa sana mwaka 2015, mfumuko wa bei utaongezeka, na wachache wataneemeka, lakini kumbukeni wahenga walisema, wapambanapo mafahali wawili, ziumiazo ni nyika
Mchezo JK anaoucheza hapa ni kutaka Lowassa ABWETEKE na kuachana na plan B. Sio mwepesi kama tunavyodhania mpaka kwamba "better the devil you know"
Mimi si mwana ccm, nionavyo ni kuwa angalau MEMBE anaheshima kidogo mbele ya jamii ya watanzania ukilinganisha na LOWASA miongoni mwa wana ccm wanaotajwa tajwa kuwa na nia ya kutaka kupanga magogoni. Mshambulizi dhidi ya lowaza ikiwa ataomba na kupewa ridhaa na wanachama wa ccm kuiwakilisha ccm kwenye mbio za kwenda mtaa wa luthuli aka magogoni yatakuwa mazito na ya silaha za maangamizi yatakayosababisha chama kupoteana na wanachama wake.
Lowasa atashindwa kwa aibu kubwa afadhali atakavyoshindwa membe.
chezea watanzania weye!
LUGHA HII WATAIELEWA WENYE MASIKIO
Ha! ha! ha! ha!ha1 ha! ha! ha! one sana, kama vipi mjipange na propagnga zenu. CCM ni chama dume haipasuki
Unjaua, you know, nyinyi watu mburula sana !
Kama vipi jipangeni mrudi na santuri nyingine
sauti ya Umeme NY
Mh.....hata huyu naye pia aende cdm,wakae meza moja na dr? nina mashaka.Nape nadhani atahamia CDM punde lowassa akitawazwa kuanza kampeni!!
Mchezo JK anaoucheza hapa ni kutaka Lowassa ABWETEKE na kuachana na plan B. Sio mwepesi kama tunavyodhania mpaka kwamba "better the devil you know"
Lowasa ni chaguo la Mungu Acheni kupingana naye
Yaaani tena ni mshambuliaji mwenye vyenga kuliko pele na anapiga krosi kali sanaaaa...yaaani hakabiki
Ivi ile miezi 6 ya Mangula inaisha lini?