Umefuatilia kwa nini hakikufanya kazi baada ya kufunguliwa na raisi? Walikosa mtaji wa kuendeshea, samaki au wafanyakazi?
Nimefuatilia sana, ni usanii tu uliofanywa, ili watanzania wadhani kuwa fedha zao kweli zimewekezwa. Nimefuatilia zaidi ya hapo na kugundua kuwa mwenyekiti wa NICOL na wenzake wachache walifisadi kiwanda toka wakati wa ujenzi. Haiingilii akilini kuwa mnawezaje kumuita Rais kufungua kiwanda hali mkijua kuwa hamna mtaji wa kuendeshea kiwanda. In fact baada ya Raisi kufungua tu ndipo wakaanza kuomba mkopo kwenye bank ya ABC. Kazi ya samaki inahitaji mtaji mkubwa sana, ABC wakawapa fedha kwa mafungu, na biashara ikawashinda.
Labda baya zaidi ni uamuzi wa mzee Mosha wa kumwajiri Meneja Mkuu, raia wa India, na sisi watu wa Mwanza tunafahamu fitina ambazo wahindi wenye viwanda vingine wana vifanya. Kwa kifupi huyo meneja alinunuliwa ili kuua kiwanda, na baada ya kufanikisha alikimbia nje ya nchi. Sasa sijui kama JK anaambiwa mambo haya. Kama mimi mkuu wa nchi nisingekubali jina langu liishie kwenye kiwanda kisichofanya kazi.
Habari nilizozipata hivi karibuni ni kuwa kumbe JK alidanganywa na maafisa wa NICOL na kwenda kufungua kiwanda cha samaki Mwanza na baada tu ya kufanyiwa usaini wa kuonyeshwa process ya kuakata samaki, kiwanda hicho hakikufanya kazi tena. DOH! jamaa yetu aliingizwa mjini.
Na taarifa za hivi karibuni ni kuwa kiwanda hicho kiko chini ya mufilisi na kimetangazwa kuuzwa kwa kuwa wameshindwa kulipa deni la Bank (ABC). Sasa huu ni utapeli wa kupitiliza. Kwanza wamewatapeli Watanzania masikini kabisa wamekusanya pesa nchi nzima, halafu wakawekeza kisanii, halafu kana kwamba hiyo haitoshi wakamualika Raisi wetu mpendwa kwenda kuweka muhuri usanii wao.
Haya jamani, wakifanya wahindi, ni mafisadi mapapa, je hawa waswahili wenzetu tutawaitaje?
Kazi kweli kweli.
Najuta sana sana kwani mie ni mmoja kati ya wanahisa wa NICOL, nilinunua hisa hizo toka 28 juni, 2008. Hadi leo hii sijapata mgao hata wa senti moja, nasasa eti NICOL ni mufilisi, duu tumeibiwa.
Hivi huyu Felix Mosha, duu kumbe nae ni bonge la fisadi, inatisha!!!
Tunaiomba menejimenti ya NICOL itupe feedback sisi wanahisa mmoja mmoja.
umefuatilia kwa nini hakikufanya kazi baada ya kufunguliwa na raisi? Walikosa mtaji wa kuendeshea, samaki au wafanyakazi?
walienda kununua kiwanda chenye deni kubwa mara baada ya kuingiza mtaji ,ukaenda kufidia benki, kumbe haikuwa hivyo matokeao yake wakawa bado wanadaiwa mojakwa moja wakaingia kwenye receivership, lakini naamini management walikuwa wanajua hilo, walifanya usanii ili wajinufaishe wao na familia zao
Kuna mtu ana NICOL financial yearly report ending 31st December 2009? natafuta jamani naona mwisho ni ya 2008!Huo uwekezaji wa NICOL nayo ilikuwa kama upatu. Kwa nini Wadanganyika hamuendi kwenye makampuni yaliyo katika soko la hisa mkawekeza huko? Mnadanganyika mno.
Huyu raisi naye kazidi na style yake kila kitu ni yeye tuuuuuuuu! Mawaziri anao lakini kila siku kafungua hoteli inayomega barabara, branch ya benki fulani, kiwanda fake kwa nini wasimpige changa la macho. Yeye size yake kabisa ila ndugu zangu wadanganyika poleni sana
Kama kiwanda tayari kilikuwa kinafanya kazi ufunguzi ulifanyika wa nini? Na walinunua "As a going concern entity" au "Assets i.e. outright sale" kwa maana kama ni Outright sale hawawajibiki kulipa madeni yaliyoachwa na mmiliki wa kwanza.
Habari nilizozipata hivi karibuni ni kuwa kumbe JK alidanganywa na maafisa wa NICOL na kwenda kufungua kiwanda cha samaki Mwanza na baada tu ya kufanyiwa usaini wa kuonyeshwa process ya kuakata samaki, kiwanda hicho hakikufanya kazi tena. DOH! jamaa yetu aliingizwa mjini.
Na taarifa za hivi karibuni ni kuwa kiwanda hicho kiko chini ya mufilisi na kimetangazwa kuuzwa kwa kuwa wameshindwa kulipa deni la Bank (ABC). Sasa huu ni utapeli wa kupitiliza. Kwanza wamewatapeli Watanzania masikini kabisa wamekusanya pesa nchi nzima, halafu wakawekeza kisanii, halafu kana kwamba hiyo haitoshi wakamualika Raisi wetu mpendwa kwenda kuweka muhuri usanii wao.
Haya jamani, wakifanya wahindi, ni mafisadi mapapa, je hawa waswahili wenzetu tutawaitaje?
Kazi kweli kweli.
NICOL ilinunua majengo toka kwa Mzee Paul Bomani baada ya yeye kushindwa kuendesha, haikuwa Outright sale, baada ya kununua hilo jengo moja ndipo walipoanza kujenga na kuagiza mashine toka nje. Utashangaa ukisikia kuwa ujenzi ulifanywa kiholela mno, hakuna mkandarasi maalum aliyewekwa kujenga, Mosha na Mkurugenzi wa fedha wa NICOL walihamia Mwanza kusimamia ujenzi, mimi nilishuhudia huo usanii, sheria ya manunuzi ya umma haikufuatwa, walikuwa wao wenyewe wanakwenda kwa wahindi kununua vifaa vya ujenzi, wenyewe wanawasimamia wajenzi, ajabu leo hii ukienda kwenye hicho kiwanda utashuhudia mipasuko mikubwa ya kutisha. Nilibahatika kusoma management letter ya auditors 2007, tshs 200m/= zilipwa bila viambatanisho vyovyote. Ningeweza kuandika mengi ninayoyajua lakini inaniuma sana kama mwana hisa kuona kiwanda kimekufa kwa utapeli mtupu. Nina ushahidi wa maandishi jinsi hawa jamaa walivyowatapeli wadanganyika.