....Kailipia Paragraph?....Obama on Tanzania:
".......The United States will focus our development efforts on countries like Tanzania that promote good governance and democracy; the rule of law and equal administration of justice; transparent institutions with strong civil societies; and respect for human rights. Because over the long run, democracy and economic growth go hand in hand......."
Hizo karata tu. Kikwete msanii.
Hiyo paragragh LAZIMA kailipia.
Watapataje Tanzanite nauranium bila kumwaga sifa hata kama ni za kinafiki??
mwananchi quotes"akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa marekani nchini, kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani
"nilikuwa nazungumza na balozi wa marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, barack obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa alitolea mfano kuwa tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema kikwete,
"maneno haya yanasemwa na wamarekani sio mimi... Watu wanasema tu marekani, marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".
Suala la Utegemezi usimlaumu JK, hilo limefanywa kuwa hivyo na the so called Super Powers!!!! kama hutaki utakiona cha Moto...!!!.
Soyry, kuna hotuba mbili: kuna hotuba aliyotoa tarehe 22 kwenye Millennium Development Summit na ile aliyotoa kwenye UN General Assembly tarehe 23. Hiyo ya tarahe 22 ni kweli aliitaja Tanzania isipokuwa hakusema kuwa tuna utawala mzuri kama Kikwete anavyodai ila alisema kuwa nchi zinazojitahidi kuwa na utawala mzuri kama Tanzania. Kujitahidi kuwa na utawala mzuri siyo kuwa una utawala mzuri.
Imaneiudhi zaidi kwa kiongozi kama Kikwete kutamba kuwa tutaenedela kupata misaada: ujinga gani huu jamani, yaani yeye anategemea kutawala nchi kwa kutegemea misaada?
Hivi alivyosema Balozi kampigia simu alikuwa ana maanisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania, au Balozi wa Tanzania nchini Marekani!! Nitamshangaa sana Balozi wa US Tanzania kumpigia simu JK kumueleza kuhusu paragraph moja ya hotuba ya Obama ambayo haina specifics!! I think kuna shida hapo
Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa JK alipokuwa kwenye ziara yake huko Ludewa, kabla ya kupanda kwenye jukwaa alipokea simu kutoka kwa balozi wa marekani nchini Bw. Alfonso E. Lenhardt. JK alidai kuwa balozi huyo alimwambia kuwa Rais Obama aliisifia Tanzania Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufuata utawala bora.
Ni vizuri pale Rais kama Obama kutambua uzuri wa taifa letu, lakini inatia shaka kama Obama aliongelea Tanzania kuhusu utawala bora. Nilisikia akiongelea South Africa (From Tyranny to democratic reforms), Congo Kinshasa (Human rights abuse), Kenya (New constitution).
Je wapi Obama aliongelea utawala bora wakati kuna fisadiz wengine bado wanadunda. Je Kikwete alidanganya ili aonekane kuwa ni kiongozi bora na kujiongezea kura? Je ni kweli balozi Alfonso E. Lenhardt alisema hayo wakati Rais wake hakuongelea hiyo mada kwa Tanzania? Nani hapa alidanganya? na kwa nini?
MWANANCHI quotes"Akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa Marekani nchini, Kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika Tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani
"Nilikuwa nazungumza na balozi wa Marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alitolea mfano kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema Kikwete,
"Maneno haya yanasemwa na Wamarekani sio mimi... watu wanasema tu Marekani, Marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".
Angalia video ujiridhishe. Karibu kwa maoni.
http://www.youtube.com/watch?v=1s7eHoRBqKI