peter tumaini
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 573
- 94
Hongera! Tunaomba isiwe kampuni kama zile za Nigeria!
mkuu ungeweka na ghalama kabisa ili tuangalie. mfano kusaidia kusajili kampuni ghalama zake na kazalika na hatua mnazo saidia
SALAAMS WANABODI!
Napenda kuwafahamisha kuwa tumeanzisha huduma ya kupata vitu mbali mbali bila kuathiri shughuli zako na muda wako.
Huduma unazoweza kupata ni zifuatazo kwa sasa;kusajili biashara yako,kampuni,kupata ofisi eneo lolote unalohitaji Tanzania,kupanga nyumba,kununua nyumba,kununua kiwanja na kuuza na hata vitu mbali mbali,kupata birth certificate,kumtafutia chuo au shule inayostahili.
Baadhi ya huduma gharama zake ziko fixed hivyo utachotoa ni commission kwetu tu kwa makubaliano maalum, hii itaokoa muda wako na kuepusha utapeli.
Kama una kiwanja unauza,nyumba unapangisha,una vifaa unauza leta taarifa kwetu na jukumu letu ni kukutanisha na mteja sisi tutachukua commission baada ya biashara kukamilika.
Hii ni mwanzo tunaanda Business yard kwa ajili ya watu kuleta bidhaa zao kuuza na watu kuja kununua.
Wasiliana nasi kwa e-mail hii;tanzanialifeclub@gmail.com.
Mkuu nawapongeza sana kwa hii innovative idea hasa katika changamoto hii ya ukosefu wa ajira. Advise yangu kwenu ni kuwa: business mnauoifanya inahitaji uaminifu na uadilifu wa hali ya juu hivyo basi mafanikio yenu yatategemea sana uaminifu wenu katika kufanikisha kazi mtakazopewa na wateja. Vilevile, utii wa sheria msije mkampa mteja document za kuchakachukua kama bith certificate
Usikatishwe tamaa na hawa ma "toy soldiers" songa mbele kaka, hii huduma yako wanatoa pia Majembe Auction Mart mimi napelekaga bidhaa zangu kuziuza wanachukua 10% ya bei ya kuuzia, wana yard yao mwenge njia ya kwenda cocacola.Haya ndo mambo tunayotaka kuyasikia humu ndani.
Hapo bold sujaelewa unapata birth certificate kutoka wapi?
Huu ni udalali tu na ufisadi tu! Mi nashauri acha watz watumie muda wao kuchacharika na kujifunza zaidi ya kuwaongezea gharama za maisha kwa kuwataka wawalipe Commission. Eti usajili wa kampuni? Jamani!!!!!!!!!!!!!
Mmefanya jambo la maana mtatusaidia kweli kuokoa muda kama mtakuwa serious na kazi zenu. Vp Kama nahitaji mchumba mnaweza kunitaftia jamani? Commission nitalipa baada ya ndoa ila naomba isiwe kubwa.
Nahitaji birth certificates za wanangu! Ni-pm au call 0754 75 45 93 nikuungishe. Big up mkuu.