Samahani
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 237
- 355
UMELIA KWA BIDII NA WELEDI MKUBWA?
Jikaze kiume!
Wanaume hawalii!!
Usilielie kama mwanamke!! Na kauli nyingine nyingi zinazoendana na hizo kimekuwa ni kitu cha kawaida sana katika mazingira tunayoishi.
Na halafu? Unalazimishwa kukinzana na mfumo wa maumbile! Unajikuta unakubali kujikaza hicho unachokiita “kiume” na kumbe unaumia zaidi, na kujiacha na jeraha baya. Jeraha la hisia lisilopona!!
Kisha? Magonjwa ya moyo, wasiwasi, msongo usiokuwa na afueni, na mwisho, magonjwa mengine mengi yasiyoambukiza. Na kifuatacho kinajulikana!!
Ni wendawazimu kukinzana na uumbaji. Ni ujinga usio na nafuu kuendelea kuikataa misingi halisi ya maisha.
Wataalamu wameainisha faida kadhaa za kulia. Tena sio tu kulia, bali kulia vizuri. Ndio, kila jambo lenye heri na faida unaopaswa sio tu kulifanya, bali KULIFANYA VIZURI. Kulifanya kwa weledi hasa!!
MOSI, unapolia vizuri unaondoa maumivu ya hisia. Unaziponya hisia zako zilizojeruhiwa. Hisia hasi mara nyingi huleta mkazo na maumivu kwenye ubongo pamoja na mfumo mzima wa fahamu. Hii unaweza kuithibitisha pale unapokuwa na hasira, uchungu au maumivu makubwa. Upesi hata namna yako ya kuamua mambo inaathirika. Ni kama kuna ukuta unajengwa mbele yako ambao unapaswa kuubomoa ili kuona mbele. Sasa ukuta huu unaweza kuubomoa kwa kulia!! Lia tu kwa weledi mkubwa, sauti ikiwa ya kiwango kizuri, huku mikono na miguu ukiirusha huku na kule, na kisha utayaona matokeo chanya kabisa ya weledi wako.
PILI, mfadhaiko katika mwili huzalisha kitu kiitwacho “cortisol”. Hii hasa ndiyo huongeza zaidi kufadhaika na kuathirika zaidi kimwili. Kulia kunaweza kukusaidia kupunguza sumu hii katika mwili wako. Sumu inaua, utake usitake!! Hakuna sumu yoyote iliyo na urafiki na uhai. Kila siku unashuhudia sumu ya panya inachowafanya panya wazembe, ila unashindwa kuiondoa sumu mwilini mwako huku ukisisitizwa kuendelea kuandaa bomu jipya kwa kupewa moyo kuwa”jikaze kiume!”. Shtuka upesi, uko hatarini
Hii ya TATU. Macho yako yanafanya kazi “kwa weledi” ukijiwekea utaratibu mzuri wa kulia lia mara kwa mara. Mwili unapokosa maji, afya ya macho inazorota pia. Maji yana faida tele mwilini. Machozi yanasaidia kusafisha macho yako na kukuongezea uoni wenye “weledi”. Hata vumbi linapoingia machoni, machozi yako yana msaada wa kutosha kuweka mambo sawa. Sasa unangoja nini kuanza kulia wewe?
Kumbuka pia kuwa, kuna siku uliwahi kufundishwa kuhusu kinga ya mwili, unakumbuka? Hao waliokufundisha kuhusu hizo kinga za mwili wanaitwa wanasayansi. Sasa ni haohao wanathibitisha kuwa, kwa kulia kwa bidi na maarifa, tunapata nafasi ya kuboresha kinga ya mwili. Hii ni njia ya asili kabisa ya kuufanya mwili wako kuwa bora zaidi. Yapo magonjwa lukuki ambayo yanapatiwa ahueni kwa kulia. Magonjwa kama mzio, kukakamaa kwa misuli, msongo mkubwa wa mawazo, sonona na aina fulani za magonjwa ya ngozi yanaweza kutibika kwa kilio tu. Yani unalia, na ukishamaliza, ni sawa kabisa na aliyemeza tembe kadhaa za panado!!
Kuna tabia zinaweza kuwa ni dalili ya moja kwa moja ya mtu ambaye hajalia kwa bidi. Ndoto za kutisha, kushtuka shtuka mara kwa mara, kukosa hamu ya kula, hasira iliyopitiliza, hofu, kiburi na hata ugomvi usio na chanzo vyote vinaweza kuwa dalili za moja kwa moja za mtu anayezuia kilio. Unapojizuia kulia, uchungu unaoukusanya katika mwili wako unaweza kukupa hali ya upweke na huzuni endelevu.
Juzi namuuliza mtu aliyevaa saa anijuze ni muda gani, akanitumbulia macho kwa hasira na kunionya nisirudie tena kumsumbua kwa kuwa naichakaza saa yake!!! Nilibaki kinywa wazi!! Hasira iliyopitiliza ni dalili za kuishi na uchungu usio na faraja ya kudumu. Faraja inayoweza kuletwa kirahisi sana na kilio chako, kilio cha bidi na maarifa!!!
Unapaswa kulia vizuri, kwa bidii na weledi mkubwa!! Acha kudanganywa!! Uwapo msibani, lia vizuri!!! Unapokosa hela, jitahidi kulia vizuri. Unapokuwa katika maombi na dua zako, hebu lia mbele ya muumba wako! Hata unapofeli mtihani, lia vizuri. Unapoumia kwa kujikwaa, kujikata na kitu kikali, au hata kudondoka bahati mbaya, kabla ya chochote, lia kwanza! Lia vizuri watu wasikie!!
Sasa endelea kuvumilia na kujikaza, ila ukifa, wenzako lazima TULIE KWA WELEDI!!