Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria, imeagiza kufanyika uchunguzi haraka katika jengo la ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ili kuweza kubaini ubadhirifu uliofanywa na wataalamu waliohusika katika mchakato wa ujenzi wa jengo hilo.
Kamati iligundua kwamba pamoja na jengo hilo kujengwa kwa gharama kubwa ya zaidi ya Tshs Billioni 8 katika ujenzi, wajanja wamepiga pesa na mpaka sasa jengo hilo limeanza kupasuka.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi katika jengo hilo na kubaini limejengwa chini ya kiwango.
“Tumetembelea jengo hilo na kujionea limetumia fedha nyingi lakini limejengwa chini ya kiwango kwani halina hata miaka tisa lakini lina ufa mkubwa ambao unahatarisha maisha ya wafanyakazi ndani ya jengo hilo,” alisema Mchengerwa.
Alisema jengo hilo limetumia zaidi ya Sh bilioni 8 katika ujenzi, lakini limejengwa chini ya kiwango.
Aliongeza kuwa kisheria fedha zilizopangwa kwa ajili ya mradi huo zilitakiwa zibaki bilioni 1.6 kwa ajili ya ukarabati lakini zimebaki Sh milioni 200 tu na hakuna maelezo billioni 1.4 zilikoelekea.
Mchengerwa alisema hali hiyo imesababisha kamati hiyo kuagiza uchunguzi ufanyike na wataalamu waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria kwa kufunguliwa kesi za jinai na madai.
Source: Mtanzania