Mfalme Ahmad
Member
- Nov 30, 2014
- 12
- 0
Umaskini ni suala ambalo linaumiza vichwa vya watu wengi sana. kila mtu hataki kuwa maskini. matajiri wanahakikisha kwamba hawafilisiki na kufanana na maskini na maskini nao wanahaha usiku na mchana kuhakikisha kwamba wanakuwa matajiri. Umaskini haupendi, umaskini unachukiwa, umaskini ni kero ya jamii nzima.
Kila mtu anawaza kwamba angekuwa na mtaji mkubwa basi umaskini alionao ungeisha mara moja na angeishi maisha ya hali ya juu ambayo yatakuwa na ahueni ukilinganisha na maisha yake ya sasa. hii imepelekea kila mtu kutaka kuwa mfanyabiashara mkubwa.
sio raia wa kawaida hata watu walioajiriwa serikalini wanatamani watumie mishahara yao kama mitaji ya kuendeshea angalau kajibiashara ili waweze kuyarahisisha maisha.
kila mtu anataka awe na mtaji mkubwa ili fedha ifanye kazi na yeye ale tu. kwa lugha nyingine kazi ambayo kila mtu anataka kuifanya ni kazi ya kusimamia miradi yake na kujua kwamba kwa siku hiyo ameingiza kiasi gani.
hivi ushaawahi kufikiri, Je endapo zitachapishwa noti nyingi na tukagawana mamilioni ya shilingi maisha yatabadilika? Jibu la uhakika ni hapana, tatizo sio fedha. sasa swali litakalofuatia je tatizo ni nini?
Tatizo sio lolote isipokuwa ni mfumo uliopo. Chanzo kikibwa cha kuwepo umaskini ni BIASHARA. Usishangae kuona kwamba nitakuwa tofauti na watu wengi ambao huamini kwamba biashara ndio mkombozi.
Waliogundua biashara walikuwa na nia nzuri tu ya kurahisisha kupatikana kwa bidhaa kwa sababu hakuna watu ambao wanazalisha kila aina ya bidhaa ambayo wanaihitaji. Biashara hurahisisha kubadilishana bidhaa ( Hii ndio faida ya biashara). Wafanya biashara wa karne hii wamekuwa ni madalali wa bidhaa wakiwaunganisha wazalishaji na watumiaji na wao wakiwa ni watu wa kati.
Faida anayoipata huyu dalali ni kubwa kushinda faida ya mzalishaji. Katika biashara kuna kodi za kila aina ambazo zote hubebeshwa mtumiaji wa mwisho yaani mlaji. Hiki ndicho chanzo cha umasikini. Utafanya kazi kwa bidii lakini kipato chako kitaishi kwenye kununua vitu vichache ili huyu dalali (mfanyabiashara) na serikali (inayokusanya kodi) ipate faida.
kwa hiyo mtumiaji wa bidhaa anakuwa kwenye mazingira ambayo hayampi nafasi ya kufaidi sawa na kazi yake.
Ninalo suluhisho la kudumu nalo ni kubadilisha mfumo mzima ya kuwafikishia bidhaa walaji. Mfumo huo hufanana kwa kiasi kidogo na mfumo wa ujamaa kwamba nyanja zote za uzalisha ni mali ya jamii tofauti ni kwamba mfumo huu ambao nimeuita usawa hufuta biashara na matumizi ya fedha.
Mfumo huo husimamia namna bora za kila mwana jamii katika kitengo alichopo kupata mahitaji yake ya msingi bila unyonyaji na kusukumiana kwenye umaskini.
Maisha ya mwanadamu kama ilivyo kwa viumbe wengine (ambao hawajui neno umaskini) hayategemei biashara wala fedha. Maisha ya mwanadamu hutegemea kazi anazozifanya yeye mwenyewe na kazi zinazofanywa na watu wengine. Wanadamu hutegemeana katika kazi.
Walimu huhitaji madaktari ili wawatibu wao na familia zao na daktari humhitaji mwalimu ili amfundishe yeye na kufundisha familia yake. mkulima humtegemea dereva ili amsafirishie mazao yake na dereva humtegemea mkulima kwa chakula. Katika maisha ya sasa watu wanaotegemea huunganishwa na biashara na fedha, mwalimu akitaka huduma ya daktari inabidi atoe hela.
Daktari akitaka huduma ya dereva inabidi atoe hela. mkulima akitaka huduma ya mhandisi inabidi atoe hela. Kumbe tunategemea na hela ndio inatuunganisha. sasa nimegundua njia bora ya kutuunganisha bila kutumia fedha ambayo ni chombo kizuri sana cha unyonyaji. Njia hiyo ni mfumo wa usawa ambao hufuta biashara na matumizi ya fedha.
MFUMO WA USAWA
Ni mfumo wa uzalishaji ambao huleta usawa kwa wanajamii wote katika suala la kupata mahitaji ya msingi (kama ilivyo kwa viumbe wengine).
KANUNI ZA MFUMO WA USAWA
1. Bidhaa zote ni bure. katika mfumo wa usawa kila kitu ni bure na kinagawanywa kulingana na kinavyopatikana
2. Kufanya kazi ni Wajibu. Kila mwanajamii anapewa ujuzi na kazi ya kufanya na anasimamiwa kuhakikisha kwamba amefanya kazi vizuri
3. Bidhaa za bure hutolewa kwa wale ambao wamefanya kazi vizuri tu na wale ambao kwa sababu ambao zimedhibitishwa hawawezi kufanya kazi.
Mfumo wa usawa huhitaji kuwepo na super market kila mtaa ambazo zitakuwa zimesheheni mahitaji ya msingi ya mwanadamu ya kila siku Mfumo wa usawa huhitaji kwamba kila mtu awe na kadi ya ki electonic au line ya simu yenye taarifa zake zote ambayo itatumika kumtambua wakati anakwenda kuchukua bidhaa dukani.
line au kadi hizo huingizwa taarifa kwamba amefanya kazi na msimamizi wa kazi kama afanyavyo wakala wa M pesa na akifika dukani ataonesha kadi yake au kutaja namba yake na baada ya kupitishwa na kuhakikiwa kwamba ameshafanya kazi basi anapewa mahitaji yake ya msingi. By by Umaskini.
Ninaposema kila kitu bure na maanisha kwamba, makazi, usafiri, mawasiliano, maji, umeme, elimu, matibabu na kila aina ya huduma ni bure ilimradi tu kila siku watu wanajifunza na kufanya kazi kisasa.
Mfano kila daladala inakuwa na dereva tu. ukifika unachukua siti, gari ikijaa dereva anaendesha kwa mujibu wa route yake kisha ukifika unashuka. Najua utahoji kuhusu mafuta.
Watu wote watakapo kuwa wanazalisha nchi itakuwa tajiri sana na itafanya biashara kimataifa juu ya bidhaa zilizo zalishwa (hii ni endapo mfumo huu usipofuatwa na dunia nzima) kwa hiyo itakuwa na uwezo wa kubadilishana mazao, gesi, madini na bidhaa na nchi nyingine na kuleta petrol ya kutosha kujaza madaladala.