Jinsi ya kutengeneza tangazo zuri la Biashara Instagram

Jinsi ya kutengeneza tangazo zuri la Biashara Instagram

Joined
Mar 25, 2026
Posts
15
Reaction score
6
Kabla ya kujisumbua kutumia hela kulipia tangazo Insta au kuboost post. Zingatia haya.

Miaka miwili iliyopita nilipata bahati ya kuajiriwa na kampuni moja ya logistics hapa Tanzania.

Kazi kubwa ilikuwa ni kutafuta wateja.

Siku moja mwenye kampuni alinialika kwenye kikao cha wateja potential (leads).

Walituma email wakitaka kikao kujua zaidi kuhusu huduma zetu.

Siku ya kikao nakumbuka mteja mmoja akaanza kulalamika.

Kampuni ya logistics aliyokuwa anafanya nayo kazi ilikuwa inazingua sana kwenye "'confirmation" ya oda za wateja.

Mwamba ni ecommerce seller kutoka Morocco.

Na oda zao nyingi ni cash on delivery (unalipa baada ya kupokea mzigo)

Kwahiyo anafanya tangazo online.

Anapata "leads" kupitia website yake.

Anakusanya namba za simu za hao leads.

Anawapa logistics company. Wawapigie simu hao wateja ku "confirm" oda zao.

Alikuwa anaamini changamoto kubwa ilikuwa kwenye call center ya hizo logistic company.

Anatumia hela nyingi. Na "delivery rate" ni ndogo. Kwasababu wateja hawapigiwi simu vizuri.

Nakumbuka tukafanya kikao na wateja wengine wawili.

Wakawa wanalalamika sana kuhusu changamoto hizo hizo.

"Their call center team is not very good"

"Im losing alot of money"

"The delivery rates are very low"

"They also dont pay me on time"

Tukaambiwa pia nchini kwao kila mtu yupo kwenye ecommerce.

Mpaka wanafunzi wa chuo.

Kuona hivyo nikamshauri mwenye kampuni tutengeneze tangazo la video.

Linalo onyesha "ufanisi" wa call center yetu.

Na tulenge hilo tangazo Morocco.

Tukarusha tangazo. Na siku ya kwanza tukapata "inquiries" kama 100 hivi.

Ndani ya ksiku 92. Mapato ya kampuni yakaongezeka kwa asilimia 102%.

Mchawi alikuwa kwenye video na maneno ya kwenye caption:

"Looking to expand your ecommerce operations in the Tanzanian market?

Or maybe...

You already have operations in Tanzania and aren't satisfied with the services of the company you're working with?" ...

Tulitumia maneno waliokuwa wanatumia kulalamika.

Na tukacheza na hisia zao kwa kuwaambia kwamba wanaweza kuwa the next "Amazon" in Tanzania.

Wateja 6 wenye operations nchi 17 Africa...

Walituletea oda 100+ kwa siku...

Tukawa tunafunga mizigo usiku mpaka kipara kikanitoka.a

Ukipitia mitandao ya kijamii utakutana na ushauri wa kila aina.

Watu wengi watakufanya uamini kutengeneza tangazo ni kazi fulani hivi ngumu.

Video tuliyotengeza tulishoot na iphone.

Na editing tuliyofanya ilikuwa ni kuandika "leading ecommerce delivery company in Tanzania" kwenye video.

Baada ya hapo tukaandika caption yenye maneno wanayotumia "kulalamika"

Ndani ya siku 92 = 10+ million TZS

Kabla ya kutumia muda wako kutengeneza tangazo.
  • Pitia online comments
  • Soma online reviews
  • Piga simu wateja wako kuwauliza kwanini wanatumia huduma za kampuni
  • Sikiliza maneno wanayosema
  • Nakiri hiyo lugha wanayotumia wakiwa wanalalamika
Alafu igeze hiyo lugha kama ilivyo.

Kama mteja analalamika:

"Low delivery rates"
"Payment delays"

Na wewe unasema:

"We know from experience customers who typically struggle with these problems:
  • Payment delays
  • Low delivery rates as a result of poor confirmation from the call center team"
Na sio unasema:

"We are a logistics entity with longstanding operations. We focus on strategic points to fullfill your logistics needs. Our strong network of strong pickup and drop centers is spread across Tanzania"

Unam-boa mteja hata kabla hajamaliza kusoma sentensi.

Unaanza kusema matangazo hayafanyi kazi.

Bila kujua unamlenga nani.

Unakua sawa na kipofu anayetembea na fimbo barabarani.

Ungekua "unaona" usingehitaji msaada wa fimbo.

Ungekua unatembea kwa uhakika bila wasiwasi.

Unaamka asubuhi ukijua unaelekea wapi bila shida.

Ni ngumu kufanikiwa kwenye matangazo bila kujua LUGHA anayotumia mteja akiwa analalamika.

Na siri kubwa ndio iko hapo.

Kutengeneza "content" au "creative" ni rahisi.

Video inaweza kuwa local tu. Ya Kawaida. Na utapata wateja.

Watu wakiwa na shida hawajali video yako inafanana vipi.

Au muonekano wake.

Una suluhisho ya changamoto waliyo nayo.

Na wanahisi unawaelewa kwasababu unatumia UGHA wanayotumia wakiwa wanalalamika.

Kuwa na siku njema.

NB. Kuna tangazo nimetengeneza wiki iliyopita linalolenga wateja wenye "hofu" ya kununua simu used. Nilipata wateja ndani ya siku 3. Na sina duka la simu. Nilifanya utafiti kwanza hapa Jamii kujua lugha watu wanayotumia kuongelea hiyo "hofu" . Ndio nikatengeneza hilo tangazo. Simu za million+
 
Back
Top Bottom