Jinsi ya kutengeneza barafu za kula (ice cream)

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
278,618
1,128,582
MAHITAJI
(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ X 10)
Maji lita 7
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote)
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza)
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)

HATUA:
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch au ubuyu na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu.

IMG_20180124_194628.jpg
 
Enzi hizo ice cream moja mnakula watu hata zaidi ya kumi...ile umenunua tu,watu wanakinga mikono kama omba omba.

Yaani km ulikuwa kichwani kwangu, nishaandika hicho kitu then nasoma hii comment yako.
Msingi jamani, alafu hata mikono hamnawi na matumbo hamuugui.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom