agudev
Member
- Apr 5, 2016
- 83
- 131
Habari zenu wadau leo ningependa kushare jinsi ya kufanya advanced search google ili kuweza kuwa sahihi zaidi katika kupata matokeo ya kitu unachojaribu kusearch badala ya kutype stori nzima kwenye search bar, google ina option tofauti unazoweza kutumia kuchuja matokeo ya search zako ili upate kile unachokitaka kwa muda mfupi. Kwa sababu ya wingi wa vitu ntajaribu kuandika baadhi nnavyoona vina umuhimu na unavyoweza kutumia mara nyingi.
Kwa ufupi tu nje ya mada nieleze vitu unavyoweza kusearch kutumia google unaweza kusearch kwa kutumia picha mfano kama una soft copy ya picha kwenye computer au simu unaweza ukaiupload google bila kuandika maneno na ukapata matokeo yanayoihusu hiyo picha. Unaweza kuatafuta matokeo katika muda fulani (mwaka, mwezi au wiki au siku) na mengine kwa kutumia “Tools” iliyopo chini ya search bar.
Tuingie kwenye mada kamili ya advanced search, google inaruhusu kutumia maneno maalum yanayoitwa “search operators” ili kuongeza uhakika wa search unayofanya, hapa nitagusia za muhimu ili kufupisha post;
1. Quotation operators(“”)
Quotation inatumika kuilazimisha google irudishe matokeo kama ulivyoyaandika katika mpangilio huo huo uliouandika, hii unaweza ukatumia mfano hasa labda unatafuta kitu lakini unakumbuka baadhi ya maneno katika kitu hicho mfano lyrics za wimbo, habari, document n.k. Mfano ukasearch "mapenzi yao kweli yakadumu" (kujumuisha alama za “”) then google itakuletea matokeo yote yenye maneno hayo kama yalivyo na kwa vile ni maneno ya lyrics za “Maria Salome” wa Saida Karoli then itakuletea kurasa zinazohusiana na wimbo huo. Operator hii unaweza kuitumia zaidi ya mara moja kama unavipande kadhaa vya maneno unayokumbuka ili kuongeza usahihi zaidi.
2. - (Minus operator)
Hii inatumika kutoa maneno usiyoyahitaji kuoneshwa kwenye majibu ya search yako. Mfano “Matokeo necta csee -acsee”, hii itakuletea majibu yote yenye maneno uliyosearch na kuondoa majibu yote yenye neno “acsee” kwenye page. Unaweza kutumia zaidi ya moja kwenye search term kuondoa neno zaidi ya moja usilotaka litokee kwenye majibu ya search yako.
3. site:
Hii ni operator ambayo inatumika kupata matokeo kutokea katika website moja andika site:yourwebsite (neno “site” ikifuatiwa na colon[:] halafu website unayotaka bila kuacha nafasi katikati), kwa mfano tuseme unatafuta matokeo ya necta na lakini hutaki matokeo ya website au blog tofauti na ile ya necta hapo unaweza kuandika mf. “Matokeo form four site:necta.go.tz” search hii italeta kurasa zenye maneno “Matokeo form four” kutoka website ya “necta.go.tz”. “site” operator inaweza kutumika kwenye top level domain mf. ukisema site:co.tz au site:net itakuletea matokeo ya website zinazoishiwa na “.co.tz” au “.net”. Unaweza kutumia “site” zaidi ya mara moja kwenye search ili kuongeza idadi ya sites unazotaka matokeo yake.
4. OR
Operator “OR” inatumika katika kutafuta matokeo yanayofanana na neno la kwanza au la pili yaliyotenganishwa na “OR”. Mfano “Matokeo OR results necta form four”, search hii italeta majibu yote yenye neno “Matokeo” au “Results” pamoja na “Necta form four”. Unaweza kuitumia zaidi ya mara moja kadiri unavyokufaa.
5. cache:
Operator hii inatumika kusearch kurasa zilizohifadhiwa na google unaitumia kwa kuandika cache:your_link ( neno “cache” ikifuatiwa na colon “:” halafu link ya page unayotaka kutafuta bila kuacha nafasi), unaweza kutumia hii kuangalia page ilivyokuwa wakati google imecrawl kwenye hyo kurasa, hii inaweza kuonekana kama haina faida lakini unaweza kuitumia kucheki kurasa ya website ambayo ipo restricted na options kama kutumia proxy au vpn inaweza ikala muda mwingi pia unaweza kucheki content za document kama vile pdf, excel, word na ppt bila kuidownload na kuisoma direct kwenye browser, kwa njia hii unaweza kuepuka virus wanaofichwa kwenye document na pia inasave muda kama huhitaji document nzima. “cache” operator itarudisha page tu ambazo google imesave kwa hyo kuna mara chache kama page haipo then itafeli.
Zipo operators zingine nyingi unazoweza kutumia katika search zako google lakini kuepuka post ndefu tuishie hapa.
Kama unaona kutumia operators itakuwa shida unaweza kutumia advanced search kupata functionality zinazofanana ingawa utakuwa na haipo flexible kama search operators. Pia unaweza kupitia kurasa hizi kwa taarifa na operator zaidi
Link1
Link2
Link3
Link4