Jinsi ya kuongeza kasi ya kompyuta yako kwa dakika chache — hata kama wewe si mtaalamu wa tech

Jinsi ya kuongeza kasi ya kompyuta yako kwa dakika chache — hata kama wewe si mtaalamu wa tech

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
135
Reaction score
285
JINSI YA KUONGEZA KASI YA KOMPYUTA YAKO KWA DAKIKA CHACHE — HATA KAMA WEWE SI MTAALAMU WA TECH

Na

ITSMALEKOGJ

Kuna wakati kompyuta inakuwa nzito, haifungui programu kwa haraka, na kila kitu kinachukua muda mrefu — hata kufungua folder tu. Mara nyingi, watu hufikiri kompyuta imezeeka au imeharibika, lakini ukweli ni kwamba, kuna “uchafu wa ndani” unaozuia kompyuta kufanya kazi kwa ufanisi.

Habari njema? Hautakiwi kuwa fundi wa IT ili kurekebisha tatizo hili. Hizi hapa ni hatua rahisi, lakini za kitaalamu, ambazo unaweza kufanya mwenyewe
Anza kwa

1. Kuondoa Mafaili Yasiyo na Kazi (Temporary Files)
Kwenye kompyuta yako, kuna mafaili ya muda hujikusanya kila siku unapofungua programu au mtandao.Ni Kama Short Memory ya kompyuta yako
Mafaili haya hayaonekani kirahisi lakini yanachukua nafasi kubwa katika kompyuta yako .
Sasa Fuata Hatua Hizi

Hatua:
Fungua Command Prompt kama Administrator, kisha andika:

del /q /f /s %TEMP%\*

Hii itaondoa mafaili yote ya muda ambayo yamekuwa mzigo kwa mfumo wako.

2. Kagua Mfumo wa Kompyuta Yako na Urekebishe Mafaili Yaliyoharibika

Wakati mwingine kuna mafaili ya mfumo yamevunjika kwa ndani, na hii ndiyo sababu kompyuta yako huwa na matatizo ya ghafla au kuchelewa kufanya kazi.

Hatua:
Andika:

sfc /scannow

Hii itaiambia kompyuta yako ijipime na kujirekebisha kama kuna hitilafu.

3. Tibu Mfumo kwa Kina (Deep System Repair)

Hata baada ya kujirekebisha, bado kunaweza kuwa na matatizo madogo ya ndani. Hapa tunatumia dawa ya mwisho kabisa kusafisha mfumo kwa undani.

Hatua:

dism /online /cleanup-image /restorehealth

Hii ni kama “detox” ya kompyuta yako. Inafuta mabaki ya matatizo yaliyojificha.

4. Zima Programu Zinazokula Rasilimali Bila Kufahamika

Wakati mwingine kompyuta inakuwa nzito kwa sababu kuna programu zinaendelea kufanya kazi kwa siri nyuma ya pazia hata kama hujazifungua.

Hatua:
Andika:

tasklist

Itaonesha kila kitu kinachofanya kazi. Ukiona programu isiyo muhimu, zima kwa kuandika:

taskkill /f /im JINA.exe

Badilisha “JINA.exe” na jina la programu unayotaka kuizima.


5. Safisha Diski na Ondoa Takataka Zilizojificha

Hatimaye, tumia Disk Cleanup ya Windows kusafisha mafaili ya zamani, Recycle Bin, na vitu visivyo muhimu.

Hatua:
Andika:

cleanmgr

Chagua diski yako (mara nyingi ni C🙂, kisha chagua vitu visivyohitajika na ubofye OK.

Kwa Nini Hii Inafanya Kazi?

Kompyuta yako inaepuka mzigo wa mafaili yasiyo ya lazima

Mfumo wako unajirekebisha na kuwa mpya

Rasilimali kama RAM na CPU zinatumika vizuri

Unapata kasi na utulivu bila kutumia pesa yoyote

Unataka Kompyuta Mpya au ata Refurbished Yenye Kasi Tayari?

Basi Tunauza laptop zenye uwezo mkubwa tayari kwa kazi nzito au matumizi ya kawaida ya kila siku. Tunapendekeza na Kutoa Ushauri Kuhusiana Na Vifaa hivii

HP Spectre, Dell Latitude, Lenovo ThinkPad na zingine nyingi

Zina kasi kubwa

Zina betri za kud


Tuma neno “LAPTOP” kwa what's App
0675 031 229 0 upate ushauri wa bure na ofa ya wiki!
Kumbuka Tunauza Kasi, Si Tu Laptop!
Follow me on X as

@GoodluckMalekoJ
#MalekoLaptops #KompyutaYako #SpeedUpYourPC #TechTipsTanzania #LaptopDeal
 
Back
Top Bottom