Jinsi ya kulinda haki za wasanii wa filamu

Feb 28, 2017
54
23
Wasanii wa bongo movie mnachotakiwa kufanya ni kubadilisha mfumo wa soko lenu ulingane na wasanii wa filamu wenye mafanikio dukani.

Chukulia movie mpya imetoka bila ya kuwekwa kwenye CD wala mitandao. Moja kwa moja ichezwe kwenye majumba ya sinema miezi mitatu.

Ikiwa mtu mmoja atalipa 12000. Ukipata watu mia kwa siku ni milioni moja na laki mbili. Kwa miezi mitatu ni milioni mia na laki nane. Mwenye jumba la sinema achukue milioni 20 msanii atabaki na milioni 80 na laki nane. Hapo kama mzee Majuto alitengeneza vituko vyake kwa milioni mbili atakuwa anacheka meno yote nje.

Ikitoka hapo inaingia kwenye TV. Kwa wenzetu kuna TV kama HBO na Show Times ambazo zinaonyesha movies tu. Siku hizi kuna Netflix, Hulu na kokolo nyingine ambazo zinaonyesha movies kwa malipo ya mwezi. Hapo kutokana na mkataba movie inaweza kuingiza pesa mpaka siku ya kiama kutokana na ubora wake.

Na baada ya hapo ndio inaweza kuingizwa kwenye Youtube nk. Kuna siku kwenye audio ya kwenye ndege nilikuta kuna choice ya nyimbo za Bongo fleva. Ila zilikuwa ni zile za zamani sana.

Hivi ni vitu vinavyowezekana kabisa kufanyika Tanzania. Na ndio maana wasanii wa Marekani ni matajiri.

Ili kufanikisha hili zoezi hatua ya kwanza ni kuwa na maduka ya kuuza movies. Na wamachinga wasiruhusiwe kuuza movie barabarani kabisa. Ndio wanaosababisha watu wasiende sinema. Wakiachiwa haitajulikana movie mpya ni ipi na ya zamani ni ipi. Halafu hawalipi kodi na wanaleta misongamano na kusababisha wizi wa mifukoni mijini.

Vilevile kuungezeka kwa majumba ya sinema kunaendana sambamba na biashara nyingine nyingi ni pamoja na burudani na kuchangamsha maisha katika miji.
 
Kumbuka tv inayorusha filamu zao mbona ipo lakini imekosa mvuto kwa watazamaji
 
Back
Top Bottom