Jinsi ya kujua kama wewe mume au mke unatumika kuvunja au kuvuruga ndoa yako

romaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
477
218
Habarini wana jamii,

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili yaani mke na mume. Ni vizuri unapozungumzia ndoa tukagusia na mwanzo wake. Mwanzo wa ndoa umenakiliwa katika Mwanzo 2:23-24: “Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama nyangu, basi ataitwa “mwanamke,” kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Ngoja nirudie hapa "nao watakuwa mwili mmoja".

Muunganiko ambao Mungu pekee ndie aliyeuunganisha (ndoa) hupata changamoto nyingi sana kutoka kwa shetani mwenyewe. Nia na madhumuni ya shetani kuwapa changamoto wanandoa hawa ni kwa sababu hataki kuona miunganiko kama hii hapa duniani kwani miunganiko hii humtukuza mwenyenzi Mungu na wakati huo huo Shetani anataka atukuzwe yeye. Shetani alianza kuvuruga ndoa zilizounganishwa na Mungu tangu enzi za adam na hawa.

Katika kila ndoa inayofanikiwa kuvurugwa na shetani matokeo yake huwa ni mabaya sana. Rejea ndoa ya kwanza ya adamu na Hawa, matokeo yake yalikuwa makubwa na mabaya yakiwepo kifo, njaa na taabu.

Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu. “Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Mathayo 19:6).

Sasa wewe kama mkristo, utajuaje kama unatumika kuvuruga ndoa yako?

Wakristo wengi hasa wa wakati huu ambao wanamtegemea Mungu wamekuwa wakiwindwa na shetani kila kukicha, hii hutokana na kwamba wanaishi maisha yenye kumpendeza Mungu kumcha Mungu. Lakini hii haizuii kuwa na changamoto kwenye ndoa zao. Mara nyingi kunatokea arguments na miss understandings kati ya mke na mume.

Jinsi ambavyo utakuwa unasuluhisha migogoro ambayo imetokea kwenye familia yako/ ndoa yako ndio njia pekee ya kujitambua kama unatumika kubomoa ndoa / uhusiano ambao unaingia kwenye ndoa.

Hii ni njia ambayo imejificha sana na shetani amekuwa akiifunika na watu wengi kutoitambua hata kama wameokoka. Najua una hamu kujua ni njia ipi hasa?

Ni hivi; ili kujua kama unatumika, inapotokea miss understanding au kutoelewana kwa kitu flani ikafika mahali mkaongea weee lakini hakuna muafaka na wawili nyie mkastop kuendelea kuongea, mkachuniana kila mmoja akimshutumu mwenzake, narudia tena hapa mkachuniana," kila mmoja akaa kimya, sasa jiulize baada ya hiyo hali kutokea huwa unapata mawazo gani?? Je unapata mawazo ya kwamba utafanya juu chini na kufanya hili changamoto liishe?? Au unapata mawazo ya kuumba changamoto zingine na hata kumdharau mwenza wako kwa mawazo yake? Je unasimamia ile misingi ya ndoa au ya mahusiano ya upendo??

Kama huwezi kusimamia misingi ya upendo kati yenu inapotokea suala la kutoelewana ujue shetani anakutumia kuvuruga amani ya ndoa yako, mfano endapo itatokea ukaongea vibaya juu ya mwenzako kwa kiashiria cha dharau basi naye utakuwa umemtupia roho ya dharau ambayo zitakuja kupigana kati ya hiyo yako na hiyo iliyomwingia. Sasa ni hivi waswahili wanasema tembo wawili wakiwa wanapigana anayeumia ni majani sasa kwenye mfano huu majani ni nyie wanandoa na tembo ni hizo roho chafu yaweza kuwa roho ya dharau, hasira, kiburi, jeuri. Rejea yohana 6:63 " roho ndio itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho tena ni uzima" andiko linatukumbusha kwamba kila neno unalotamka na mimi naongezea (unalowaza) nyuma yake kuna roho itiayo uzima au mauti.

Nimeongezea kuwaza kwa sababu wakristo wengi wa sasa hivi wamejisahau kwamba wana uhuru wa kuwaza chochote wakiamini hakuna mtu anaye waona au kuwasikiliza wanachowaza na hakuna madhara na kusahau shetani haingizii watu hizo roho chafu katika maneno tu bali hata mawazo. Na hili ndilo msingi wa makala hii.

Kama umejitambua kwamba umekuwa ukitumika kuvuruga ndoa yako ni wakati wako sasa kubadilika na kumgeukia Mungu na kuishika upya misingi yako ya ndoa na upendo. Ukifanya hivi kila inapotokea changamoto kwenye ndoa yenu utaishia kuongea mema na kuwaza mema kwani unaongozwa na misingi ya ndoa na upendo nanyi mtaishi kwenye ndoa miaka mingi kwa amani upendo na furaha.
 
asante mhubiri, somo zuri, na we uishi kwa vitendo na siO kwa nadharia tu
 
ni kweli katika ugomvi wa wanandoa wengi wao huwa hawakubali hata kidogo kujishusha au kukiri kosa ili kuepusha ugomvi,yaani mmoja anapokosea Huwa ana hakikisha kuwa hakubali kosa lake,Hali ya namna hii ikifikia ujue ndoa yenu imebakia mazoea tu yaani hamuishi ki upendo tena.
 
Back
Top Bottom