Kabisa ni mawazo mazuri mnokuhusu kuzuia bidhaa za nje ni lzm uwe na uhakika kuwa hizo bidhaa unazozuia lzm ziwe zimeanza kuzalishwa nchini kwako na kwa ubora stahiki,alasivyo yatakuwa ya sukari 5000 kilotunakuza uchumi wa nchi
Kwenye swala la uongozi ni lzm kuangalia weledi,hekima,utimamu na uzalendo si uniambie ati waliopata 150-120 ndo wanatakiwa wawe viongozi hapana,watu tunatofautiana vipaji,kuna watu hawakusoma sana lkn wameibadili dunia kiasi kikubwa sana.
Kwenye suala la vyuo nipo nawe 100%..
Nafikiri kwa nchi yetu hata tukiegemea kilimo kiudhatiti hatuitwi maskini tena,sera mipango na utekelezaji ndio nyezo ukijitambua.
SIASA ISICHANGANYWE NA UHALISIA WA MAISHA
kwanza elimu kipindi cha nyuma hasa kwa kikwete alifanya elimu kama ngazi ya kudanganya wananchi kuwa tumeongeza vyuo vikuu, kumbe havikukidhi malengo au sifa, ila anataka tu idadi ionekane yeye ameacha vyuo vikuu vingi zaid, suala ambalo limeua elimu yetu,
Jingine viongozi wakubwa kulazimisha ndugu na jamaa zao kudahiliwa katika vyuo mbali mbali bila sita stahiki, nayo ilileta shida mnoo,
Suala au Jambo kingine ni kuogopa kuwa sema wazembe kwa kuogopa kuchukiwa kisiasa au kukosa Kura kwa awamu ya pili,
Hapa watu wengi wameharibu nchi sana,
Njia zipo Nyingi tuungane
Hapo kwenye siasa kwa nchi zetu Africa inakua tabu kidogo, kwa kuwa sisi wenyewe tumewakabidhi uaminifu mkubwa wanasiasa na wao kutufanya wanavyotaka.
Vile vile wanasiasa ni watu ambao siku zote mtaji wao ktk mafanikio ni watu ambao Lazima wahakikishe wanafanywa kuwa Wateja wao ktk sanduku la kura. Kwa hiyo ndo hao ambao husema maisha bila siasa haiwezekani.
Lakini maisha ukichanganya na siasa ni sawa na kuchanganya "sukari na chumvi".
Ni hakika Nyerere alituachia viwanda vingi nadhani vimekufa 1995Siasa iwe siasa. Ila mwanasiasa asiwe ndie mchumi wa kupanga mipango, asiwe mwanasheria wa kujivunjia mikataba hovyo, asiwe igp wa kutaka nani awekwe ndani na kunyanyaswa. Abaki na siasa yake ila akae na wote wenye taaluma zao na kuangalia masualaa ya nchi yanaenda aje na kushauriana nao juu ya kuyaboresha.
Msisitizo wa elimu ya ufundi iwe ni kipaumbele. Kuliko kuwaleta wachina wengi, tungepeleka WaTz wengi nje kupata ujuzi, wataalamu wachache kutoka nje waletwe pale kwenye mambo mkubwa kama kufunga mitambo na washirikiane/ kuwaelekeza wa kwetu jinsi ya utunzaji na kufanyia matengenezo.
Mambo yanayosikitisha ni kwamba nchi haina dira ya muda mrefu, leo viwanda vinashadidiwa majukwaani, lakini ukweli ni kuwa 1985 kulikuwa na viwanda vya kumwaga si vya vibiriti, batteries, magurudumu, makaratasi/daftari, kalamu, radio, majiko, taa za chemli, baiskeli, nguo/vitambaa, viatu/ngozi, plastic(ndoo/vyombo vya ndani n.k) mbao, vyuma, chokaa na cement, uzalishaji, sabuni zote, mafuta ya kujipaka, ya kupikia, vya maziwa, pembejeo za kilimo, mbolea, yaani karibu kila idara ilikuwa na kiwanda kinachozalisha vifaa husika. Vimeachwa na kufia mbali so wananchi wala viongozi walioona kuwa tunaelekea siko , leo tunakurupuka ili tuanze upya. Ipitiwe historia na kuangalia viwanda vile vilianzishwa kwa muda gani na nini kilipelekea hadi kupotea kwake. Ili makosa yasirudiwe tena kama kuna nia ya dhati. La sivyo siasa ikiendekezwa, kama ilivyo kwa umasikini na ujinga kuwa mtaji wa wasiasa wa nchi hii, basi na suala la viwanda litaongezwa katika hiyo orodha, mwanasiasa wakipata uhakika wake wa kuwa madarakani kwa kutumia kauli mbiu hiyo, anaondoka, hakuna lolote lililotekelezwa, akija mwingine, anakuja na uzushi wake, itabakia Tz ya kuchezewa na wanasiasa na wananchi hawajitambui.
Najaribu kuku pm cm yng inagoma ni pm tujadili jambo tuweza fanya jamboKabisa hapa inabidi tuwe na mitaala yetu