Jinsi Ya Kufanya Maamuzi

Jinsi Ya Kufanya Maamuzi

Radium

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
490
Reaction score
871
Maisha mazuri ni matunda ya mfuatano wa maamuzi sahihi. Hasa katika nyanja za mahusiano na kazi. Ila huwa tunadogodesha shughuli ya ufanyaji maamuzi na huipa attention ndogo sana.

Pale ambapo maamuzi makubwa yanatuface, tunakosa hatua na utaalamu kwa ujumla. Sanasana tunafanya procrastination(mapuuza), au kuegemea kwa mtu wa karibu kwa ushauri au kuchagua chaguo ambalo liko unexamined .

Bahati nzuri ufanyaji maamuzi ni skill na kama skills zingine, inaweza kufudishwa. Adui mkuu wa maamuzi ni ukosefu mitazamo sahihi ya tatizo lililoko mbele yetu.

Systematically inabidi tufikirie kila jambo kutoka kwenye angle 5 tofauti. Na njia hizi zitatusaidia kupata maono sahihi ya nini ni cha kutuwajibisha na hivyo kufanya maamuzi ambayo matokeo yake yana chance kubwa ya matokeo chanya na kama matokeo yakiwa hasi basi majuto yanakuwa yenye kuvumilika.

#1 -OUR ENEMY.
Maadui zetu wana deep insight kwenye udhaifu wetu. Wao muda wote wanachotaka ni sisi tuteseke. Na wanatumia akili na nguvu zaidi kuhakikisha chochote tusichokitaka kinatutokea.

Katika zama za utandawazi ni vigumu zaidi kwako kuwa rafiki wa kweli kwako mwenyewe na hili tunalijua ni tokeo la nini. Akili yako inaweza kuwa empty yenye giza unapoambiwa uimagine ninini ambacho mtu wako wa karibu angekushauri ufanye kwa hali uliyo nayo sasa, ila ni rahisi kabisa kujua ni idea gani adui yako angekupa.

Wao wanatuangalia kwa madhaifu tu, sehemu ya motisha wanakuja kutuponda, wanasema "Huwezi wewe ni ngumu mno, achana nayo, au Wamefanya wangapi wenye uwezo mkubwa kabisa yamewashinda unajisumbua tu" Wanaoenda kutupa temptations muda wote.View attachment 2452335

Sasa kazi ni kwetu kuwatumia maadui zetu kwa faida, kwa kufanya kinyume na chochote kile wanachoweza kupropose au kusema.

"We Will Be Energised And Focused By The Haunting Voices Of Those Dispiriting But Very Telling Mesmerising Judges: THOSE WHO REFUSE TO BELIEVE IN US"

#2- GUT INSTINCT.
View attachment 2452341
Kwa namna fulani, jibu tunalijua tayari au walau upande mmoja wa suluhisho. Tunasema ni roho au moyo unatuambia lakini kiuhalisia hisia hizi tunazisikia kutoka tumboni na tunalijua hili.

Jibu hili huwa tunakuwa nalo palepale tu tunapokuwa na dilemma. Kwa mfano Mwanamke yeyote anapofuatwa na mwanaume, kabla hajasema point zake tayari anahisia kabisa mtu huyu si sahihi. You just feel it.
Iko hivi, Gut ni mkusanyiko wa mafunzo yote ya kimaamuzi tuliyowahi kuyapata. Kila taabu ulizo pata kwa sababu ya maamuzi mabovu utayafeel unapoenda kufanya maamuzi mabovu mengine. Unajua kabisa unaoa mtu sio, unajua kabisa safari yako jumanne ijayo itakuwa na kashkash, unajua kabisa bidhaa unayonunua itakuwa tu tatizo fulani, unajua kabisa.

Most of us tumekuwa wazuri sana katika kuipuuza hisia hii, inawezkana imewahi kutuinguza kwenye majaribu na ikatugharimu. Kwahiyo sasa tumekuwa wazee wa kufikiria, kukusanya ushahidi na takwimu, watumiaji wa high mentak power na kutembea kwa kutumia logic(Although we should) View attachment 2452350
Lakini tunapuuza msaada mkubwa tunaoupata kutoka kwenye sehemu iliyoko complicated functionally na constructively as it is the brain.

Yatupasa kuthubutu kualika our guts kwenye meza ya majadiliano na maamuzi, hatakama sio kwa ajili ya kuisikiliza bali walau kujua nini ilitaka na kisha kuitunza idea yake inayoonekana ya kipuuzi iliyokosa mahesabu kwa ajili ya majaribio ya karibu kwa wakati mwingine.

#3. DEATH.
...Jambo ni kubwa na uhakika ni asilimia miamoja, lakini tunalisahau kiurahisi zaidi nalo ni kuwa kila maamuzi tunayofanya yanahesabika kama masaa kufunguka na kufumuka katika kifaa kisichoacha kuhesabu huko kilipo, The Death Clock...

Inabidi sasa tusikilize milio yake na tuubebe ujumbe wake wa kutisha na kukatisha tamaa moyoni. Ni kifo ndicho hufanya maisha yetu yasiwe na maana bila kujali ni mazuri kiasi gani.

Katika maamuzi, wazo la kifo lazima litakukumbusha wajibu wako kwako mwenyewe na kuachana na kuishi maisha wanayokupangia watu wengine

(Achana na matumaini ya wazazi wako, Wewe sio wajibu wa boss wako, na katika mahusiano jali hisia zako na kuwa muwazi wa hisia zako, THERE IS NO TIME LEFT INDEED)

Kifo kinakuwinda muda wote, hata hapo ulipo ukigeuza shingo yako utaona njia milioni za kufa, huo mtungi wa gesi jikoni unaweza kulipuka muda wowote, na vipi kama unaugonjwa unaokutafuna bila kujua.
It is almost...comic.

Screenshot_20221220-082924_YouTube.jpg

Muda ni mchache sana kukaa na kujiwaza au kuogopa rejections.

Uoga wa kifo unaweza kutupa confidence kubwa sana ya kukabili changamoto kwa sababu hakuna kubwa zaidi ya hii only because we can't avoid it.

"Our lives won't be what it could be, unless we submit pretty much every choice we face to the arbiter of eternity and oblivion"

#4. CAUTION.
Katika kila kona ya meza yetu ya maamuzi lazima kuna sauti ya tahadhari. Imevaa nguo za kuchakaa na inaongea taratibu sana kwa kunong'oneza. Katika zama za Bravado na Bombast, bado imekosa majivuno.
Unafeel ni sawa kabisa kuvuka barabara taa nyekundu inapowaka japo ikiwa unahisi inakaribia kuzima, lakini huvuki, hatua ya uchumba inaonyesha kabisa huyu mtu ni mzuri lakini bado unasita. Tukumbuke kuwa Tahadhari anasafisha koo lake kutuambia kuwa, biashara nyingi zimefeli, miradi mingi imeishia kuwa janga, na mahusiano yoyote unayovunja leo ni kioo cha yale yanafuata kwenye future, yote ni yaleyale.

Kuna mengi sana tunakwenda kuyapoteza na ni wengi tutawaumiza.
Tahadhari anakukumbusha tu kuwa hata ufikirie vipi hakutakuwa na chaguo sahihi kwa 100% kwa kiumbe asiyemkamilifu.

#5 COURAGE.
Toka tu tulipozaliwa tunachofundishwa ni kufuata utaratibu na sheria, kufuata mstari na kufanya yale yanyotarajiwa na wakubwa wetu(kikazi au kiumri au kimamlaka)
Screenshot_20221220-085746_YouTube.jpg

Unafundishwa kuwa mtoto mzuri, ila imekuleta mpaka ulipo. Labda kungekuwa na njia zingine za kujifunza kuongea, kuendesha gari, kama kiongozi wa elimu kubadilisha mtaala wa shule zetu au kushika nafasi fulani kikazi.
Lakini sasa kuna risk, risk ya kuwa muaminifu sana kwa wakuu wetu kwa muda mrefu sana kuendea kwenye kaliba ambazo tunafanya bila interest zetu wenyewe bali kwa kupandikizwa, kwa sababu ndicho pekee tulichojifunza.

Sasa ni wakati tujifunze sanaa ya uthubutu. Kukumbuka kuwa maisha ya furaha kwa point fulani, watu walifanya jambo ambalo halikutegemewa na wakafuata njia ya tofauti kabisa, wakaicheza kamari ya maisha na wakashinda.
Muda mwingine Uthubutu ni aina ya uoga na udhaifu uliofungwa kwenye kasha la kujidanganya, Tahadhari na Uthubutu itabidi wapigane vita hii bila upendeleo wa upande mmoja.

Kila chaguo ni lazima litakuwa kasoro zake ila kwa kufikiri vizuri utano huu chance ni kubwa kwenda na chaguo bora zaidi ya mengine.

Ni zipi njia zako za ufanyaji maamuzi muhimu?
 
Maamuzi nafanya kulingana na baraza la ubongo wangu, sifanyi maamuzi kumfurahisha mtu, na siogopi jamii itasema nini juu yangu hata nikikosea ni juu yangu, hivyo nguvu yangu kubwa ni kuwa fearless, i take risks of all kinds.
 
Maamuzi nafanya kulingana na baraza la ubongo wangu, sifanyi maamuzi kumfurahisha mtu, na siogopi jamii itasema nini juu yangu hata nikikosea ni juu yangu, hivyo nguvu yangu kubwa ni kuwa fearless, i take risks of all kinds.
Appreciated
 
Maamuzi nafanya kulingana na baraza la ubongo wangu, sifanyi maamuzi kumfurahisha mtu, na siogopi jamii itasema nini juu yangu hata nikikosea ni juu yangu, hivyo nguvu yangu kubwa ni kuwa fearless, i take risks of all kinds.
 
Back
Top Bottom