masimango
Member
- Dec 14, 2014
- 26
- 7
Habari za kazi wadau wa jukwaa hili
Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea salama kabisa na juhudi za kulijenga Taifa letu.
Leo naomba tushirikiane kwenye hiyo mada tajwa hapo juu ili tuweze kuboresha usomaji wetu, usomaji huo unaweza kuwa wa vitabu au majarida mbalimbali.
Naomba kujua kwa wale wazoefu wa usomaji vitabu ni mbinu gani ambazo mnazitumia ili kusoma kwa ufanisi, kwa maana ya kusoma kwa kuelewa mantinki na maana ya kitu unachokisoma.
Kwa upande wangu mimi ni mpenzi sana wa kutaka kuwa msomaji vitabu lakini mara nyingi nimekutana na changamoto mbalimbali wakati wa kusoma vitabu. Kwa mfano kupata usingizi baada ya kusoma kurasa chache, kukosa hamu ya kusoma, kurudia kusoma baada ya muda mwingi kupita (nikisoma leo labda nakuja kuendelea kusoma wiki ijayo, hii inapelekea kusahau ulichokisoma nyuma), na mengine mengi.
Kwahiyo nalileta kwenu ili tushirikiane mawazo ni jinsi gani ya kuboresha usomaji vitabu ili tuwe wasomaji wazuri wa vitabu na kuongeza maarifa katika maisha yetu ya kila siku.
Naomba kuwasilisha kwenu mada hii.
Asante