Jinsi wa kuwakomesha watoto wa mjini

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,810
Njia kubwa ya kuwafanya watoto wa mjini wawe na adabu ni kusave pesa, hakikisha account yako haikosi milioni mbili ya dharura kila siku. Unafahamu faida yake??

Watoto wa mjini hupenda sana kununua vitu visivyovimudu na mwisho wa siku huishia kuviuza tu, sasa wewe unawasubiri wanunue kwa bei kubwa dukani kisha wakifulia wanauza kwa bei ya kutupa na hapo ndipo unapowanyoosha.

Mwaka jana kuna kijana alinunua subaru milioni 14, alikaa nayo miezi mitatu anataka kuiuza milioni 13 alipokuja kwangu analia lia nikamwambia mi nakupa milioni saba tu akagoma. Nikamwambia nenda, alipoondoka nikamtumia sms kuwa uwezo wangu wa mwisho ni milioni nane bado akasema haiwezekani amekaa siku mbili hana kitu alikuja ye mwenyewe na subaru yake nikanunua kwa milioni nane nikatafuta mteja taratibu nikauza kwa milioni 11.

Bado wale wa kununua iPhone 6 kwa milioni mbili akikaa mwezi mmoja hana pesa anauza hata kwa laki nane.

Vijana jifunzeni kuwa na pesa ya dharura kwenye account, kuna watu wao huweka pesa za dharura kwaajili ya kununua viwanja vya wenye shida kwa bei rahisi na kuviuza.

Kulingana na uwezo wako, unaweza kuwa upo chuo. Unasave pesa ili kusubiria wanafunzi wenzio wakifulia unanunua simu zao kwa bei ua kutupa kisha unaenda kuuza kwa faida, jiridhishe na ubora wa bidhaa.

Kwa heri 2015
 
Angalia lakini usije ukakwaa vya wizi. Pia kumbuka kulipa kodi ya TRA unaponunua gari kwa mtu ama kiwanja kwa mtu!
 
Wale wanaouza nyumba, wakitokea niletee nikupokee
 
Mimi nauza boti... million 175...
Hiyo boti imetengezwa kwa materials gani? Fibers au chuma? Ya abiria au mizigo? Ina Uwezo wa kubeba tani ngapi? Mashine ni Outboard au inboard? Mashine jina gani? Ina HP ngapi?hiyo boat inauwezo wa kukimbia speed knots ngapi?
Fafanua mkuu siyo unatangaza biashara bila maelezo yaliyonyooka.
 
Back
Top Bottom