Jinsi uchaguzi wa Serikali za Mtaa ulivyochafuliwa Iringa!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
19,751
37,187
Imenichukua muda mrefu sana kuandika uzi huu, nimekuwa nikiwaza kama wale waliohusika kuuchafua huu uchaguzi ni watu wenye akili timamu ama la. Wengi wanazungumzia uchaguzi huo kiujumla lakini mimi nizungumzie eneo la Manispaa ya Iringa nilipokuwepo.

Kwanza imeshangaza sana ilikuwaje wakati wa kuandikisha kila kituo kilikuwa na ulinzi lakini wakati wa kuchukua na kurudisha fomu ulinzi huo uliondolewa. Kitu gani kilikuwa kinalindwa wakati wa kuandikisha na ni jambo gani lilisababisha polisi waondolewa wakati wa kuchukua na kurudisha fomu.

Vurugu za kunyang'anya fomu zilifanyika kwenye Ofisi za watendaji wa kata, inakuwaje mtendaji wa kata ambaye ni mlinzi wa amani asitoe ripoti kwa polisi kwamba kwenye kituo chake kuna uvunjivu wa amani?

Kwenye kituo cha Mwangata "D" mwandikishaji wa Orodha ya wapiga kura aliondoka kituoni mara mbili kwa siku tofauti akiwa na daftari la wapiga kura na kurudi baadae na daftari lake baada ya masaa mawili. Ofisa wake alipopewa taarifa akadai ni lazima kuwe na Ushahidi, Inawezekanaje Ofisa wa Polisi anayelinda kituo hicho asione kama huo ni uhalifu?

Ofisi ya Kata Ipogolo aliyeingia kupora fomu alifahamika na kuripotiwa polisi ingawa hajakamatwa mpaka leo. Mwanachadema aliyemfukuzia mshirika wa mporaji fomu huyo yeye ndiye aliyekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa tuhuma ya kufanya shambulio la kudhuru mwili.

Kata ya Gangilonga kulikuwa na kundi la watu zaidi ya 30 walioshinda kwenye ofisi ya Kata hiyo kwa siku zote 7 na kuzuia watu wa vyama vingine kuchukua fomu. Tukio liliripotiwa Polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Siku ya Jumapili na Jumatatu karibu watendaji wa kata zote hawakuwepo Ofisini kwao. Inakuwaje Waziri ataje asilimia ya vyama kugombea wakati kwenye kata zingine vyama vingine vilizuiwa kuchukua fomu kwa njia za kihalifu na hajachukua hatua kwa watendaji waliofanya hivyo?
 
Izo ni moja ya changamoto zilizo jitokeza, ila kwa waliojiandikisha waende wakachague kiongozi kwakua awa viongozi wa serikali za mitaa ni muhimu na ndio tunaofanyanaokazi kilasiku uku kwenye mitaa yetu muhimu wao ni zaidi ata ya wabunge ambao tuna onana nao marachache sana katika miaka mitano ya utumishi wao.
 
Imenichukua muda mrefu sana kuandika uzi huu, nimekuwa nikiwaza kama wale waliohusika kuuchafua huu uchaguzi ni watu wenye akili timamu ama la. Wengi wanzungumzia uchaguzi huo kiujumla lakini mimi nizungumzie eneo la Manispaa ya Iringa nilipokuwepo.

Kwanza imeshangaza sana ilikuwaje wakati wa kuandikisha kila kituo kilikuwa na ulinzi lakini wakati wa kuchukua na kurudisha fomu ulinzi huo uliondolewa. Kitu gani kilikuwa kinalindwa wakati wa kuandikisha na ni jambo gani lilisababisha polisi waondolewa wakati wa kuchukua na kurudisha fomu.

Vurugu za kunyang'anya fomu zilifanyika kwenye Ofisi za watendaji wa kata, inakuwaje mtendaji wa kata ambaye ni mlinzi wa amani asitoe ripoti kwa polisi kwamba kwenye kituo chake kuna uvunjivu wa amani?

Kwenye kituo cha Mwangata "D" mwandikishaji wa Orodha ya wapiga kura aliondoka kituoni mara mbili kwa siku tofauti akiwa na daftari la wapiga kura na kurudi baadae na daftari lake baada ya masaa mawili. Ofisa wake alipopewa taarifa akadai ni lazima kuwe na Ushahidi, Inawezekanaje Ofisa wa Polisi anayelinda kituo hicho asione kama huo ni uhalifu?

Ofisi ya Kata Ipogolo aliyeingia kupora fomu alifahamika na kuripotiwa polisi ingawa hajakamatwa mpaka leo. Mwanachadema aliyemfukuzia mshirika wa mporaji fomu huyo yeye ndiye aliyekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa tuhuma ya kufanya shambulio la kudhuru mwili.

Kata ya Gangilonga kulikuwa na kundi la watu zaidi ya 30 walioshinda kwenye ofisi ya Kata hiyo kwa siku zote 7 na kuzuia watu wa vyama vingine kuchukua fomu. Tukio liliripotiwa Polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Siku ya Jumapili na Jumatatu karibu watendaji wa kata zote hawakuwepo Ofisini kwao. Inakuwaje Waziri ataje asilimia ya vyama kugombea wakati kwenye kata zingine vyama vingine vilizuiwa kuchukua fomu kwa njia za kihalifu na hajachukua hatua kwa watendaji waliofanya hivyo?
Mkuu Allen nyie si mmejitoa?!
 
Wapinzani hawakutumia busara kujitoa Wamekosea sana

Wafikirie upya
Waliobaki wanatosha kuendelea na uchaguzi, sio lazima kila chama kishiriki hizi chaguzi.

Kuna vyama viliamshwa usingizini vikatoa tamko kushiriki bila hata kuwa na wagombea, kwasababu tu CHADEMA ilijitoa.

Mbona uchaguzi mdogo singida hawakujali vyama vingine kutoshiriki?!

Waliopo waendelee tu.
 
Izo ni moja ya changamoto zilizo jitokeza, ila kwa waliojiandikisha waende wakachague kiongozi kwakua awa viongozi wa serikali za mitaa ni muhimu na ndio tunaofanyanaokazi kilasiku uku kwenye mitaa yetu muhimu wao ni zaidi ata ya wabunge ambao tuna onana nao marachache sana katika miaka mitano ya utumishi wao.
Umeongea pumba tena kama kada mkubwa tu wa chama tawala mnufaikaji
 
Mkuu Allen nyie si mmejitoa?!
Ukisoma vizuri ni wakati wa kuchukua na kurejesha fomu. Kata yetu ina mitaa 9 ambako CCM wamejitangazia kupita bila ya kupita. Hivi kupita bila ya kupingwa maana yakeni ni kupita bila ya kuzuiwa kutumia mabavu kwenye uchaguzi?

Domsel na Executive Diary Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya aliuliza swali la msingi sana. Kuwapiga hawa jamaa kutatusaidia kupata fomu ama wengi wetu watakamatwa na kushitakiwa mashitaka yasiyo na msingi na kusumbuliwa bure?
 
Back
Top Bottom