Jimmy Carter: Marekani ni nchi ambayo daima ipo vitani

pauli jm

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
391
278
Sera za kijeshi na zakupenda vita za Marekani, zinakosolewa kote duniani na hivi sasa hata wakuu katika nchi hiyo wameanza kukosoa sera za nchi hiyo.

JIMMY CARTER.
Raisi wa zamani wa nchi hiyo kutoka mwaka 1977-1981, katika mahojiano na jarida la Time Anasema tokea kuanzishwa kwa umoja wa mataifa baada ya vita ya pili ya Dunia Marekani daima imekuwa vitani.

Rais huyo wa zamani wa Marekani ambae aliwahi kushinda tuzo ya amani ya "NOBEL", anasema tangu vilipomalizika vita vikuu vya pili vya Dunia Marekani imeanzisha vita katika nchi 30 Duniani.

Matamshi hayo ya rais huyo wa zamani wa Marekani, Ni dalili tosha yakuwa nchi hiyo haiwezi kutekeleza mipango yake ya kisiasa na uchumi bila yakutegemea Vita.

Kwa hakika Marekani katika muundo wake wa sasa, uliibuka katika nusu ya karne ya 18, baada ya kupigana vita ya uhuru na Ufalme wa Uingereza. Tokea wakati huo kimsingi nchi hiyo huwa vitani. Marekani ilipigana vita na Uingereza mwaka 1812.

Kisha ikapigana vita na Mexico mwaka 1846. Na vita na Uhispania mwaka 1898. Kisha ikaingia katika vita vikuu vya kwanza vya Dunia mwaka 1941.

Baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia Marekani iliendeleza, sera zake zakichochezi na vita kwa kile inachokiita kupigania uhuru wa Dunia.

Hapa tunaweza kutaja baadhi ya vita ambavyo Marekani inajihusisha navyo ambavyo ni;

Vita vya Korea mwaka 1950.

Vita vya Vietnam mwaka 1960.

Hujuma dhidi ya Kisiwa cha Grenada mwaka 1983.

Kukaliwa kijeshi Panama mwaka 1989.

Hujuma dhidi ya Iraq mwaka 2003.

Hujuma dhidi ya Libya mwaka 2011.

Hiyo ni mifano muhimu ya vita ambavyo Marekani imejihusisha navyo katika kipindi cha miaka 70 iliyopita. Mbali na hayo Marekani imejihusisha na operesheni kadhaa za kijeshi kila kona ya Dunia. Na kuchochea mapinduzi ya kijeshi katika mataifa kadhaa.

Mbali na hayo Marekani ilichochea na kuhusika na Vita baridi, na shirikisho la zamani la Soviet. Hivi sasa Marekani inahusika na Operesheni kadhaa kote Duniani katika kile inachodai nikupambana na Ugaidi. Lakini uhalisia ni uingiliaji wa masuala ya ndani ya nchi zingine.

Hata kama hakuna takwimu kamili zilizokusanywa za watu waliopoteza maisha kutokana na vita za Marekani. Lakini tunaweza kusema katika kipindi cha miaka 240 iliyopita mamilioni kwa mamilioni ya watu wamepoteza maisha yao kwa sababu ya uzandiki wa Marekani.

Hapa tunaweza kuashiria matukio mawili yaliyotokomeza, Nafsi za watu kama kuku. Kudondosha mabomu ya Atomiki katika miji ya Iroshima na Nagasaki nchini Japan.

Katika muda wa siku mbili ambapo watu 220,000 walipoteza maisha. Nchi nyingi Duniani zinashuhudia hasara ya vita au Operesheni za kijeshi za Marekani.

Utafiti umebaini kuwa uchumi wa Marekani, hauwezi kustawi ila kwa nchi hiyo kueneza vita sehemu mbalimbali Duniani.

Kwa msingi huo kwa Serikali ya Marekani na kwa vilevile wananchi wa Marekani weng , vita ni jambo lisiloepukika. Kwa muundo wa Taifa la Marekani kwa sasa.

Kwa hiyo ni vigumu mno kwa Marekani kusitisha sera zake za kichochezi na vita.
 
Back
Top Bottom