Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 255
Meya wa Kinondoni/ Jiji la DSM, mnaujua upuuzi huu unaoendelea kwenye miundombinu ya barabara zilizo chini ya tawala na mamlaka zenu?
Inasikitisha sana kuona almashauri inaagiza greda linaharibu miundombinu ya Maji, barabara zetu, tena linapita tu mara moja kwenda na kurudi, yaani ndani ya dk 5. Hakuna kushindiria, hakuna kurekebisha njia zinazoingia kwenye makazi ya watu, yanaachwa mabonge ya udongo, linatengenezwa tuta kubwa utadhani mnataka kupanda viazi....
Hii ni mifano ya picha za barabara 2 ambazo zimemalizika. Barabara ya kutoka (Makondeko) Ruguruni kuelekea ndani ikipitia Lapaz hotel na barabara ya kutokea Kibamba kwa Mangi kuelekea Mdidimua...
Tunajua bajeti ni ndogo lakini hii si sawa. Mnaumiza wananchi.
PSE, share mpaka imfikie Mbunge, Mameya wa almashauri manispaa za DSM na meya wa jiji.
Naamini tunahujumiwa.