FUJISTU
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 261
- 93
Kama unatumia simu yenye android na hujui jinsi gani unaweza ku-upgrade simu yako basi soma hapa na utaelewa vitu karibu vyote na njia gani utaweza kufanya software upgrade ya simu yako.
Simu yako labda inatumia Android 2.1 Eclair au 2.2 Froyo au 2.3 Gingerbread au 4.0 Icecream Sandwich, au 4.1 au 4.2 Jelly bean au pia una 4.3 Jellybean na unataka ku-upgrade na kupata features nyingi zaidi?
Kwanza unatakiwa ujue vitu hivyi ambavyo wengi hudhani ni vigumu ila si hivyo.
Rom hili ndiyo inabeba operating system ya simu yako, kwa kawaida huwekwa katika file moja lililogandamizwa (compressed) (zip). Kuna Rom aina mbili:
Stock Rom ambayo huwa ni operating sysytem inayokuja na simu kutoka kwa makampuni yanayohusika na utengenezaji wa simu
Custom Rom ambayo hutengenezwa na wataalamu tofauti kutoka na uhuru wa matumizi ya Android (Open source), na kwa pamoja huitwa Android Open Source Project (AOSP). Hapa ndiyo kuna Cyanogenmod, SlimBean, Packman na nyingine nyingi tu zilizo na majina ambayo ukiona unaweza ukadhani ni kitu cha ajabu kama AOKP ni kazi ya Kang hivyo inaitwa (Android Open Kang Project).
kernel hii ni program maalumu inayotumika kuendesha hardware zote kwenye simu yako, display, camera, speaker, mic, battery n.k.
Recovery hii ni sehemu iliyotengwa maalum kwenye simu yako ambapo utaweza kuna program maalum itakayokupa uwezo wa kufanya marekebisho na kubadilisha operating system ya simu yako, kama kufany aupdate na factory reset(kufuta kila kitu na kurudisha simu katika hali iliyotoka nayo kiwandani{software}). Reovery pia zipo aina mbili kama zilivyo Rom, kuna stock Recovery na Custom Recovery kama CWM (ClockWork Mod)
Root hii ni sehemu ya simu yako inyoweka operating system na mafaili yote yanayoiwezesha simu yako kufanya kazi. Kwa kawaida sehemu hii ya simu huwezi kuitumia wala kubadilisha kitu ila unapofanya rooting ndipo unapata uwezo wa kubadilisha vitu humu kupitia application ya superuser.
Flash kuflash simu ni kuweka operating system mpya kwenye simu, hii inaweza kuwa ya zamani ina tatizo na ndiyo maana tunapeleka kwa mafundi au umemua kuibadilisha na kuweka nyingine.
Nandroid Backup hii ni njia ya kufanya backup ya kila kitu kwenye simu yako zikiwemo application na data zote na kuzihifadhi kwenye memory card kwa kutumia application ya nandroid manager
Bootloader hii ni part ya software katika simu yako inayofunguka kabla simu haijawaka na hutoa command kwa simu ili ijue pa kuanzia kusoma ili iwake. Kwa simu kama HTC sehemu hii huwa imefungwa hivyo utahitaji kufungua kabla ya kufanya chochote.
Kupata update mpya kwenye simu yako njia rahisi ni kuangalia kama kun updates kutoka kwa watengenezaji, hii utaangalia kwenye software updates iliyopo ndani ya simu yako.
Ila kama ungependa kufanya upgrades na kutumia Custom Roms basi utatumia njia ifuatao.
Zifuatazo ni general procedure za kufanya update katika simu, kunaweza kuwa na mabadiliko kulingana na simu:
Katika internet tafuta Custom Rom ya simu yako utakayotaka kuitumia kisha utaidownload katimka memory card yako, kisha tafuta gapps (google applications) za toleo la android kulingana na custom rom yako na utazidownload na kuzihifadhi sehemu moja na hiyo custom Rom
Root simu yako kila simu zina njia tofauti za kuroot ukitaka kujua jinsi ya kuroot ya kwako unaweza ukatafuta katika google root (jina na model ya simu yako) na utapata maelezo
Badilisha recovery kila simu zina recovery tofauti, pia ukigoogle recovery ya simu yako utapata maelezo ya jinsi ya kuibadilisha. Napendekeza zaidi CWM (Clockwork Mod Recovery)kwa kuwa inapatikana kwenye simu nyingi. Download Recovery manager ambayo itakusaidia kuwasha simu katika recovery kwa urahisi
Download Nandroid Manager an ufanye back-up ya data zote katika simu yako
Washa simu yako katika recovery (tajwa juu), kisha utafuta kila kitu kwa kufanya Factory reset alafu utatumia option ya install zip from sd card kutafuta na kuchagua file lako la Rom lilipo katika memory card yako, ukilichagua utakuwa umeflash simu yako, kwa kufwata njia hii pia utaweza kuistall application za google (gapps) kwa ajili ya toleo la Rom uliyodownload
Ikimaliza chagua Reboot System now, Hongera utauwa umefanikiwa ku-upgrade simu yako kwenda toleo la Adroid unalotaka. Sasa utadownload Nandroid manager tena na kurestore data zako katika simu
project2
ANGALIZO : Procedure nilizotaja hapo juu ni kwa ufupi, utahitaji kufanya vitu vidogo vidgogo kuzikamilisha, pamoja na hayo utahitaji kuwa mwangalifu katika kila hatua kwani kukosea kunaweza kukaiharibu simu yako kabisa.
source www.bongoelectronics.com