Jifunze kusimamia lengo

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Wengi tunachanganya sehemu tunazotakiwa kuwa laini ndio tunakuwa wagumu na sehemu tunazotakiwa kuwa wagumu ndio tunakuwa laini.

Badilika jitambue kuwa na msimamo usikubali kuyumbishwa na mawazo ya kila mtu,kaa chini fikiria chuja chagua watu sahihi wa kukushauri kwa kila nyanja na usimshirikishe kila mtu tatizo lako...

Ili ufanikiwe vizuri lazima ufikie kiwango cha kuitwa,mbahili,anaringa,anajivuna,anajiona sana hela zake zina macho,kadha wa kadha lakini kwa upande wa pili hakikisha iwe ni ukiwa na jambo la msingi anakusaidia ana roho nzuri,anajituma,amepitia shida nyingi hadi kufika hapo,unavyomuona vile kapambana sana.

Maana yake ni kwamba sio wote watakupenda na kukuelewa kwa jambo lako lolote lile,unatakiwa kuwa ua kuwasikiliza lakini kama dharuba katika kufanya ulichokiamini.

Uwe na Siku njema.

Elisha Chuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo hata huu ushauri wako ni wa kupuuzwa, kila mtu aamini kivyake au tukuamini wewe pekee..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…