ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 644
Na
Augustino Chiwinga.
•KUMSHAMBULIA RAIS MAGUFULI.
Hii ndio sababu kubwa iliyopelekea CHADEMA na UKAWA kushindwa vibaya katika uchaguzi huu.Walidhani kwamba kumshambulia Rais kwa kumuita dikteta na mbinyaji demokrasia kungesaidia kumdhoofisha kwa wananchi.Wananchi hawauoni udikteta wa Rais Magufuli , unaposema Rais dikteta wananchi wanapata picha ya kina Hitler na Mussolini au Idd Amin kitu ambacho kwa Rais Magufuli hakipo kabisa.Matokeo yake wakaonekana kua ni wababaishaji tu wa kisiasa mbele ya macho ya wananchi.
Katika mikutano yao walimaliza muda na nguvu zao nyingi kumshambulia Rais Dr.Magufuli kwa maneno ya kebehi pasi na kujua kwamba wananchi wanamkubali na kuridhishwa na utendaji kazi wake uliotukuka .
Katika hili they missed a point!
•KUTOKUA NA AJENDA.
Kwenye kila mkutano wa kampeni walikua hawana ajenda ya kueleweka ya kuwaeleza wananchi.
Walikua wanarukia rukia ajenda moja baada ya nyingine mara njaa mara demokrasia mara Rais mbabe nk.
Walijikita katika kukejeli na kubeza zaidi badala ya kuongea ajenda zenye mantiki kwa wananchi Mathalani mikutano yao katika kata za Mateves na Ngarenanyuki walitumia muda mrefu kuelezea kuhusu kesi ya Lema na kusahau ajenda za wananchi, tofauti na CCM ambao walikua na ajenda zilizopangiliwa vyema zikigusa moja kwa moja matatizo na kero za wananchi.
Wananchi hawakuwaelewa kabisa CHADEMA!
•KUMTUMIA MZEE LOWASSA.
Hapa ndipo penye kosa kubwa la kiufundi lilipofanyika.
Mzee Lowassa katika mikutano ya udiwani alikua anajipigia yeye kampeni za urais.Mfano ni alipokua katika mkutano mmoja kule Kahama na Geita alisema anaomba wananchi wampigie kura awe rais kabla hajashtuliwa na wasaidizi wake kwamba huu sio uchaguzi wa Urais ndipo akamuombea kura Diwani wa CHADEMA.
Lowassa alitumia fursa hii kujijenga yeye binafsi katika mbio zake za kuwania urais 2020 badala ya kukijenga chama na wagombea wake.
Haikuzaa matunda!
•MPASUKO NDANI YA CHADEMA.
Ukweli ulio wazi ni kwamba kuna mpasuko mkubwa sana ndani ya CHADEMA unaoendelea na ambao kwa kiasi kikubwa umekigharimu chama hiko.
Tukianzia kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalumu ambao ulifanywa kwa upendeleo na ubabe kwa kuwateua wasiostahili na kuwaacha wanaostahili kwa hakika uliacha majeraha na maumivu makubwa ambayo yamechangia kukiangusha chama hiko katika uchaguzi huu mdogo.
Pia kuibuka kwa makundi kama vile kizazi cha kuhoji ni matokeo ya mpasuko huo ndani ya Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) .Hili ni kundi lilikosana na uongozi wa juu wa BAVICHA ndio maana wakaamua kuunda "BAVICHA" yao ndogo na wakaipa jina la kizazi cha kuhoji Tanzania kwa minajili ya kupambana na uongozi wa BAVICHA taifa.
Pia ndani ya chama hicho kuna makundi matatu,
1)CHADEMA BIASHARA (Mbowe na wenzie)
2)CHADEMA WAKUJA (Lowassa na aliohama nao)
3)CHADEMA ASILI (John Mnyika, Halima Mdee na wenzake)
Vita ya makundi haya matatu si ndogo wote wanawania kushika hatamu katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka 2019 .Hatua ya Ole Sosopi kukatwa katika kuwania nafasi ya uenyekiti kanda ya Nyasa ni matokeo ya vita hii na kushughulikiana huku kila kundi likidhamiria kulidhoofisha kundi moja ili kujiweka mguu sawa katika uchaguzi wa ndani mwaka 2019.
•UTENDAJI WA VIWANGO WA RAIS MAGUFULI.
Pasi na kupepesa macho utendaji wa viwango wa Rais Magufuli umeendeleea kuwakosha wanachi .Vita dhidi ya Rushwa, nidhamu kwa watumishi wa Umma utoaji wa elimu bure ununuaji wa ndege , kubana matumizi nk.ni mojawapo ya mambo ambayo yameendelea kumuweka juu Mh Rais Dr.Magufuli kwa watanzania.
Hivyo kampeni zote za njaa ,sukari UKUTA KATA FUNUA propaganda zote za mitandaoni za CHADEMA zimebuma kutokana na kutoaminiwa tena na wananchi kwa undumilakuwili wao wa kumpokea fisadi na kumpamba. Wananchi wameamua kuwapotezea na kuamua kuungana na Rais wao katika Sera yake ya Hapa Kazi tu kwa kuchapa kazi na kutowasikiliza Chadema nini wanachokisema.
Rais Magufuli bado ameendelea kubeba matumaini ya wanyonge na maskini wa Tanzania akitekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kasi na umahiri mkubwa.
Augustino chiwinga.