ELI COHEN
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 9,375
- 28,484
Mnamo Aprili 2, 2015, mwendo wa saa 11:30 alajiri, Chuo Kikuu cha Garissa kilichoko Garissa, Kenya, kilikumbwa na ugaidi pale watu wanne wenye silaha waliojifunika nyuso zao kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab walipovamia chuo hicho.
Washambuliaji hao, wakiwa na AK-47 na mikanda ya vilipuzi, walifanya shambulio la kikatili sana waliwapata wanafunzi wengi wakiwa wamelala kwenye mabweni yao au kujiandaa kwa sala ya asubuhi. Watu hao wenye silaha waliwaua walinzi wawili wasiokuwa na silaha kwenye lango kuu, kisha wakagawanyika katika makundi, wakilenga hosteli na madarasa.
Walifyatua risasi kiholela mwanzoni, lakini upesi wakaanza kuwatenganisha wanafunzi kwa msingi wa dini zao. Wanafunzi Waislamu waliachiliwa, huku Wakristo wakitengwa kwa ajili ya kuuliwa, wengine walipigwa risasi papo hapo, wengine kuchukuliwa mateka. Wanafunzi wa kikristo Walioshirikiana kuhudhuria maombi ya asubuhi waliuawa kinyama sana.
Walionusurika walisimulia matukio ya kutisha: wanafunzi walilazimishwa kulala kifudifudi na kuuawa, miili iliyotapakaa chuoni, huku magaidi wenye silaha wakidhihaki miili ya waathirika. Mwanafunzi mmoja, aliyejificha kwenye viguzo vya dari, alielezea kuvuka miili mingi ili kutoroka.
Ugaidi huo ulichukua karibia masaa 15. Vikosi vya usalama vya Kenya, wakiwemo Makomando wa Kikosi cha Recce, walizingira chuo hicho, wakijihusisha na milio ya risasi ya hapa na pale huku washambuliaji wakiwa wamejificha kwenye bweni.
Kufikia jioni, washambuliaji wote wanne waliuawa, mmoja akijifyatua ya vest ya vilipuzi ili ajitoe mhanga, na kuwajeruhi makomando.
Idadi ya mwisho ilikuwa mbaya sana: watu 148 waliuawa, ikiwemo wanafunzi 142, askari watatu, na maafisa watatu wa polisi, na 79 walijeruhiwa. Zaidi ya wanafunzi 500 walihamishwa, wengi wakiwa na trauma ya kile walicho shuhudia.
Al-Shabaab, kundi lenye makao yake nchini Somalia lenye uhusiano na Al-Qaeda, lilidai kuhusika, likitaja ushiriki wa Kenya wa kijeshi nchini Somalia (Operesheni Linda Nchi na AMISOM) kama nia yao ya kufanya hivyo.
Walipanga shambulio hilo kama kulipiza kisasi kwa "ukaaji" wa Kenya wa ardhi za Waislamu na kuwalenga Wakristo kupandikiza mgawanyiko wa kidini.
Hitilafu za kijasusi zilikuwa dhahiri. Tahadhari za uwezekano wa kutokea kwa shambulizi katika chuo kikuu kikuu zilikuwa zimesambaa siku zilizopita, hata hivyo usalama huko Garissa ulikuwa umelegea sana