Fl1 nilikua nadhaniaga ww ni mtu wa vitenge zaidi kumbe tofauti.
mim kwa upande wa nywele,sijazitia dawa maana nina nywele nzuri ndefu za asili ila sometime naweka weaving nikijisikia kubadilika ila rasta sipendi .
napenda kujiremba ila sio kwa heavy make ups,
mavazi yangu makuu ni tight jeans ,leggings,jeggings na blause ninazovaa inategemea na mahala ninapoenda ila sipendi mablauzi makubwa makubwa.
Viatu vyangu vingi ni high heels tena lazima iwe ndefu hasa ila flats pia navaa sometimes.
Im allergic to perfum hivyo miaka yote kuna perfum ya aina moja tu ndio naitumia.
siwezi kutoka bila pochi begani.
Sipendi kuvaa ma accessories mengi kama mibangili ,mamikufu na mihereni ya rangi rangi hivyo ukikutana na mim aidha utaona nimevaa cheni simple ya white au yellow gold na vihereni vidogo mkononi napenda kuvaa saa mara nyingi,au no hereni sometimes,navaa hereni kubwa sometimes ila zaidi kama nimevaa gauni refu tight la usiku.
Mkorogo situmii ,miaka yote natumia nivea body milk na ndio inayosaidia niwe na ngozi laini kama ya mtoto mchanga lol.
nguo ambazo sipendi kuvaa ni BIKINi,(najua ni ushamba lkn hata nikienda beach bora niogelee na skin tight lkn ujasiri wa kuonyesha makalio yangu mbele ya raia sina). Pia sipendi vitenge na suti au kitu chochote ambacho kimepitwa na wakati au kilichopo kwenye fashion lakini hakiendani na heshima yangu kama mdada aliyempokea YESU.
kwa kweli napenda sana kupendeza hivyo kila ninachovaa lazima kinipe classy and glamorous appearance.